Jumatatu, 10 Juni 2013

Kuuawa kwa Osama Bin Laden


Kwa ufupi

Jina lake likawa maarufu kupita kiasi na majarida kwa majarida yakaandika kumhusu. Kwenye hadithi hii iliyotafsiriwa kwa Kiswahili na Mussa Shimba, tunapata kufahamu mtiririko wa mambo hadi ikapatikana hatima ya Bin Laden ambaye alikamatwa na kuuawa akiwa katika maficho nchini Pakistan.



Osama bin Laden aliitikisa dunia ingawaje ni kwa kipindi kifupi tu. Kwa kutumia kundi lake la Al Qaeda, Osama alihusishwa kwenye mashambulizi kadhaa mabaya sehemu mbalimbali duniani yaliyosababisha vifo vya watu kwa maelfu ikiwa ni pamoja na lile la Septemba 11, 2001, lililotokea nchini Marekani. Kutokana na hali hii Osama akawa mwanadamu anayesakwa kwa udi na uvumba.



Jina lake likawa maarufu kupita kiasi na majarida kwa majarida yakaandika kumhusu. Kwenye hadithi hii iliyotafsiriwa kwa Kiswahili na MIKI TASSENI, tunapata kufahamu mtiririko wa mambo hadi ikapatikana hatima ya Bin Laden ambaye alikamatwa na kuuawa akiwa katika maficho nchini Pakistan.



Wiki iliyopita tuliona jinsi Maafisa wa Usalama wa Taifa wa Marekani walivyokuwa wameshaanza kupata dodoso la wapi Bin Laden alipo, waliendelea kufanya uchunguzi wa jumba alilokuwa akiishi Bin Laden (Sheikh, huko Abbottabad nchini Pakistan...



Kuta zilizozunguka jengo hilo zilikuwa ndefu kuliko kawaida, zikiongezewa na futi mbili za senyenge. Kulikuwa na kuta za ziada kuzunguka ukumbi wa jengo hilo ulioko nyuma ya ghorofa ya tatu.



Hapakuwa na jinsi ya kuona ndani ya nyumba yenyewe, kutoka ardhini au angani. Madirisha yalikuwa ya kioo kinachorudisha mwanga.



CIA iligundua kuwa siyo tu kuwa Abu Ahmad na familia yake walikuwa wanaishi hapo, lakini pia kaka yake Abrar na familia yake.



Walikuwa wakitumia majina ya kubandika mtaani, Ibrahim akijiita Arshad Khan na ndugu yake akijiita Tareq Khan. Wote walikuwa wamezaliwa Kuwait, lakini kikabila ni Wapashtun wa Pakistan. Walikuwa hawajawahi kuwa matajiri, lakini jengo lao lilionekana kuwa ni la gharama kubwa.



Pamoja na kuta ndefu, ilielekea ndugu hao walikuwa wanafuata taratibu kali kupita kawaida za usalama. Walikuwa kwa mfano wanachoma taka zao katika uwanja wa jengo hilo.



Mbali na kuhudhuria shule ya kidini, watoto wao walikuwa hawaondoki jengoni. Wakipiga simu kwa ndugu zao walio mbali, walikuwa wakifanya hivyo kutoka maeneo mbali na nyumbani kwao. Walikuwa kamwe hawasemi wanakokaa.



CIA ilikuwa inashindwa kutafsiri vitu vingi, lakini kitu kimoja ilichokuwa ikikijua kwa undani ni tahadhari ya hali ya juu katika operesheni zake.



CIA ilikuwa inapeleleza jengo hilo na harakati za wanaoishi humo, kimyakimya, ikichukua picha kutoka juu na kulipeleleza kwa kutumia watu wanaopita hapo ambao wasingeweza kuona ndani lakini wanauliza maswali ya kawaida watu wanaokaa karibu na hapo, huku wakichukua tahadhari wasionekane wana shauku kubwa mno ya kujua.



“Nani anayekaa katika jengo hili kubwa? Je,watu wanaokaa humo wanafanya nini?” Maswali ambayo, pamoja na kunasa mawasiliano ya simu yaliwezesha ugunduzi wa mambo mawili katika wiki kadhaa zilizotangulia ambayo CIA ilikuwa inaona ni muhimu sana, na kumshauri Panetta kuwa anahitaji kuleta ugunduzi huo mbele ya rais.




Cha kwanza ni kuwa wanaokaa katika ghorofa mbili za juu ni familia tatu. Hakuna mtu wa familia hiyo ambaye alikuwa anatoka humo. Watoto wao walikuwa hawatoki kwenda shule pamoja na wale wengine.



Majirani hapo Abbottabad ambao walikuwa wanawafahamu akina Khan na familia zao walikuwa hawajawahi kusikia kuna familia ya tatu. Na kulikuwa na dalili kuwa ndugu hao, ambao kimsingi walikuwa wanamiliki jumba hilo, walikuwa wanatumikia familia hiyo iliyojificha. Mmoja wa ndugu hao muda wote alikuwapo, hivyo familia hiyo ya tatu kamwe haikuachwa peke yake.



Ibrahim Ahmad na familia yake walikuwa wakitumia nyumba iliyopo langoni; ndugu yake Abrar na familia yake walikuwa wanakaa ghorofa ya kwanza ya nyumba kubwa.



Ugunduzi wa pili ulikuwa kwamba inaelekea Ibrahim Ahmad bado anaitumikia Al Qaeda.



Licha ya kuwa alikuwa anafahamika kuwa karibu na Bin Laden, CIA ilikuwa haina ushahidi kuwa alikuwa ameendelea na uhusiano huo. Baadhi ya wafungwa waliohojiwa kabla walisema alikuwa ameondoka kwenye mtandao wa Al Qaeda, ambayo ina maana kuwa hivi sasa alikuwa anafanya kazi na mtu yeyote aliyekuwa na sababu ya kujificha.



Ni haramia wa biashara haramu? Mtu tajiri mwenye maadui wa kisiasa? Milionea wa Kisaudia mwenye kimada au nyumba ndogo ya siri? Lakini katika msimu aliyopiga kwa rafiki wa zamani miezi ya kiangazi (mwaka 2009), simu ambayo Marekani iliisikiliza, Ahmad alifululiziwa maswali ya kawaida, “Unafanya nini sasa? Una malengo gani?”



Mwanzoni hakujibu, aliyakwepa maswali. Lakini rafiki yake akang’ang’ania, hivyo mwishowe akakiri, licha ya kufanya hivyo kwa kificho. “Niko na wale wale kama mwanzo,” alisema. Rafiki yake alielekea kuelewa mara moja kauli hiyo ilikuwa na maana gani, na baada ya kusema “Allah awe nawe,” suala hilo liliishia hapo. Hiyo ilikuwa na maana kuwa yeyote ambaye Ahmad na ndugu yake walikuwa wanamjali hapo Abbottabad alikuwa mtu wa Al Qaeda.



Haya ndiyo maelezo yaliyofikishwa kwa rais.



“Hii ndiyo taarifa nzuri zaidi tuliyopata kuwa nayo kuhusu Bin Laden tangu aondoke Tora Bora,” alisema John.



Obama alikuwa anafahamu maisha ya Bin Laden vya kutosha na alikuwa muda mrefu ameacha kumfikiria akiwa amejikunyata katika pango au amekaa katika kambi kwenye kilele cha mlima fulani.



Lakini kumkuta ndani ya jumba la kifahari katika mtaa wenye hadhi unaofahamika kwa mikusanyiko ya kucheza gofu na upepo mwanana wa kiangazi cha baridi - hilo liliwashangaza wote. Hata hivyo rais hakuwa na matumaini makubwa.



Alijua alikuwa ameisukuma mno CIA kuja na kitu fulani, akitaka taarifa za ufuatiliaji, hivyo alikuwa akitazamia kuwa watampa kipande chochote kinachopatikana. Aliona taarifa hiyo inazingua kidogo, lakini katika hali ya jumla. Uhusiano na Bin Laden ulikuwa wa uibahatisha tu. Alimhimiza Panetta kuendelea kupambanua.





Alitaka uhakika wa familia hiyo iliyojificha ni kina nani upatikane. Pia alitaka kielelezo hicho kibanwe, ambayo ina maana kisiondolewe machoni pake. Hakuna mtu mwingine katika jeshi au mtandao wa ujasusi angeingizwa katika suala hilo bado. Na wasiwahusishe kabisa Wapakistani au kuonyesha kujali sana kinachotokea mjengoni.




Rais alibakia na chaguo la kuwasiliana na wanaodhaniwa ni washirika wake wa Pakistan pale watakapokuwa wanajua zaidi. Katika wakati uliopo, alikuwa akitaka taarifa za kila wakati za maendeleo ya (upelelezi huo).



“Kwa hisia tu,” Obama alisema, “sikuwa na matumaini makubwa kuhusu jambo hilo. Nadhani nilikuwa mwangalifu sana nisianze kuweweseka kuhusu uwezekano huo wa kufanikiwa katika jambo hili.”



Wakati huo, rais alikuwa akitoa amri za mashambulizi ya drone na operesheni maalum kuua viongozi wa Al Qaeda kwa takriban miezi 20. Ujuzi wa mitandao ya ujasusi ya Marekani na majeshi yake, kutokana na miaka tisa ya vita, ulikuwa umempa uwezo ambao hakuna rais wa Marekani aliyewahi kuwa navyo.



Mikutano ya Baraza la Usalama la Taifa haikuwa tu ya kujadili sera, ilikuwa inagusa mara kwa mara masuala ya uhai na kifo kwa walengwa kadhaa.



Uwezo uliojengwa katika muongo uliopita ulimpa rais nafasi za haraka za kuchagua kuhusu walengwa - watu ambao walikuwa wametafutwa na kuonekana, na sasa wako katika ncha ya unywele ya Marekani. Wangeweza kuuawa kwa amri yake bila kuweka mashakani usalama wa Mmarekani hata mmoja. Kulikuwa na mashambulio ya drone 53 katika Pakistani pekee katika mwaka wa kwanza wa utawala wake.



Mwaka 2010 idadi ya mashambulio ilikuwa zaidi ya mara mbili(yalikuwa 117). Idadi ya mashambulio Yemen, licha ya kuwa machache zaidi, yalikuwa yakiongezeka, kutoka mawili mwaka 2009 hadi manne mwaka 2010, na yalikuwa yafikie kumi mwaka unaofuata. Karibu kila siku rais alikuwa anahitaji kufanya uamuzi kuhusu mashambulizi.



Uamuzi wa kuisambaratisha Al-Qaeda haukuwa uamuzi mwepesi hata kidogo. Pamoja na kwamba marais kadhaa wa Marekani walishapitisha uamuzi mgumu katika kulinusuru taifa hilo,



lakini uamuzi wa mara hii ambao kimsingi ulikuwa ukimsaka kwa udi na uvumba mtu mmoja, ulikuwa uamuzi mgumu pengine kuliko ule wa kuingia katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia.



Usikose kusoma stratejia zilizopangwa kumkamata Osama Bin Laden kesho katika.



                                             "  NITAREJEA"








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni