Watoto wa familia ya mzee Athumani Mwenda wakiwa wamelala nje.
Tukio la kuvunjiwa nyumba lilitokea Mei 24, mwaka huu katika Kitongoji cha Mvuti, Ilala, Dar na inadaiwa kuwa ubomoaji huo ulifanyika chini ya mtu aliyejitambulisha kwa jina la Boatu Msuya ambaye ni dalali wa mahakama huku akiongozana na polisi sita wenye bunduki aina ya SMG.
Akielezea tukio hilo kwa masikitiko makubwa, mzee Mwenda ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sangara, Kata ya Msongora alikuwa na haya ya kusema:
“Sina mahala pa kwenda na hawa watoto, nani anaweza kutupa hifadhi, chakula na matibabu? Tunaishi kama wanyama porini.
Mazingira wanayopikia wanafamilia hao.
“Ni zaidi ya nusu ekari na ndiyo maana wamechukua na eneo la nyumba yangu na kuibomoa huku nikiwa nimelala ndani na wajukuu zangu, niliamshwa dakika za mwisho, nikaokolewa na wajukuu zangu, nusura tufunikwe na kifusi.
“Nilipotoka nje nilikuta kundi la vijana na askari, niliwauliza kwa nini wananibomolea nyumba, wakanijibu nikae kimya. Hakuna kiongozi yeyote wa serikali aliyekuja naye wala barua inayonitaka nihame au kubomoa nyumba.
Mzee Athumani Mwenda (80).
”Naamini kungekua na watendaji wa mahakama hapa au kiongozi yeyote wa serikali wa kusimamia zoezi hili haya yote yasingetokea, nimeonewa.
“Kwa sasa tunalala nje, mvua, jua na maradhi ni vyetu, nimeishi hapa tangu mwaka 1980 enzi hizo hapa likiwa pori, leo hii wameona lipo karibu na barabara ya lami wanaamua kujigawia, sikubali hata kidogo,” alisema.
Afisa Mtendaji wa kata hiyo, Omar Ali Khalfan alipoulizwa juu ya sakata hilo, alisema kwamba mzee huyo tayari ameshachukua hatua ya kuandika barua kwenda mahakama kuu na ameshaipitisha na kumgongea muhuri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni