Jumanne, 11 Juni 2013

UNAFAHAMU KWAMBA CCM NI MTOTO WA NANI?

 
 
ULIKUWA na miaka mingapi Februari 5, 1977? Hivi uliwahi kujiuliza Chama Cha Mapinduzi ambacho leo kwa kifupi tunakiita CCM kilitokana na nini?

Hebu soma yafuatayo:
Hapo kale kule visiwani Zanzibar kulikuwa na chama kilichokuwa kikiitwa Afro-Shiraz Party (ASP), kikijumuisha Waafrika na watu wa asili ya Shiraz waliotoka Arabuni walioamua kuishi huko baada ya misafara ya kibiashara.  
 

Ndiyo maana  Zanzibar ya leo ina watu wengi wa asili ya Arabuni.
Nchini Tanganyika ambayo ni Tanzania Bara, kulikuwa na chama kilichokuwa kikitawala tangu 1961 kilichoitwa Tanu, yaani Tanganyika African National Union.

Baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, Aprili 26, wanasiasa, wakiongozwa na fikra za Mwalimu Julius Nyerere,  walikubaliana kuviunganisha vyama hivi viwili.  
Hivyo ASP na Tanu wakakaa chini na kuanzisha chama kimoja walichokipa jina la Chama Cha Mapinduzi ambacho watu wazima na vijana leo hii wanakifahamu kama (CCM).

Kwa mahesabu ya haraka CCM imetawala nchi hii kwa miaka ipatayo 36, na ukichukulia ASP na Tanu pamoja, nchi hii imetawaliwa na fikra za wanasiasa wa vyama hivyo kwa miaka ipatayo 50.
Hiyo ndiyo CCM ambayo ndiyo Chama Cha Mapinduzi kilichoko madarakani unaposoma hapa
 
Chanzo: global publishers

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni