Jumapili, 28 Julai 2013

AMANDA, BWANA MISOSI WAMWAGANA

Na Gladness Mallya
HATIMAYE wale wapenzi waliong’aa hivi karibuni, mwigizaji Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’ na Mbongo Fleva, Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’ wanadaiwa kumwagana rasmi, Ijumaa limetonywa.
Tamrina Poshi ‘Amanda’ akiwa na mpenzi wake wanayedaiwa kumwagana naye, Emmannuel Rushau ‘Bwana Misosi’.
Habari kutoka chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wapenzi hao, zilieleza kuwa Amanda na Bwana Misosi walishamwagana kimyakimya ikiwa ni baada ya kushindwa kuelewana kitabia.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Amanda ili aelezee ukweli kuhusu habari hizo ambapo alikiri kuwa ni kweli wameshaachana na hii ni baada ya kushindwana kitabia.
Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda.
“Mimi na (Bwana) Misosi tumeachana muda mrefu tangu mwezi wa pili  baada ya kushindwana na katika uhusiano wa kimapenzi, nimejifunza kuwa wanaume siyo watu wa kuwaamini asilimia mia moja kwani baadaye unaweza kujuta,” alisema Amanda.
Kwa upande wake Bwana Misosi hakuweza kujibu moja kwa moja swali aliloulizwa bali alianza kwa kujikanyagakanyaga
“Kwanza niko safarini, je, ni nani aliyekuambia hizo habari….hebu ngoja nimpigie huyo Amanda nimuulize nani aliyetoa siri hiyo,” alisema Misosi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni