Bagamoyo Pwani
MSICHANA
Rehema Athumani Mpendae, ameuawa kikatili kwa kunyongwa na mtu
anayedhaniwa kuwa ni mpenzi wake huku chanzo cha kufanyiwa unyama huo
kikiwa hakijulikani.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu waliopanga
katika nyumba moja na marehemu, wamekadiria kuwa Rehema alinyongwa saa
12 jioni kwenye nyumba aliyokuwa akiishi katika eneo la Majani Mapana
wilayani hapo.
Alisema baada ya polisi kupata taarifa walifika katika eneo
la tukio na kukuta msichana huyo akiwa amedhalilishwa na kuuawa kinyama
kisha wakamuita.
“Baada ya kufika kwenye nyumba hiyo nikatakiwa na
polisi kuingia ndani ili kujua kama kuna mtu katika chumba cha
marehemu,” alisema Matata.
Aliongeza kuwa mara baada ya kuingia ndani
aliukuta mwili wa binti huyo ukiwa umelazwa kitandani bila ya nguo huku
ukiwa umefunikwa, mdomoni akiwa amezibwa kwa kanga.
Mmoja wa
wapangaji wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Fauzia Abdallah
(20), alisema kuwa mara ya mwisho kumuona Rehema ilikuwa ni Ijumaa jioni
ya Julai 19, mwaka huu.
“Siku hiyo ilipofika jioni nilimsikia
akizungumza kwa simu huku akimtaka mtu ambaye inaonekana alikuwa mpenzi
wake na hakuwa mbali na hapa akimwambia amsubiri ili waonane.
“Alitoka
ndani na baada ya muda nilimsikia akiingia na mtu ambaye alikuwa na
sauti ya kiume lakini kwa sababu nilikuwa ndani kwangu nikiangalia TV,
sikuweza kumuona au kumfahamu,” alisema Fauzia.
Alifafanua kuwa kama
saa 12 hivi jioni alisikia wakiwa wanabishana lakini hakuweza kujua
walibishania kitu gani na baadaye kukawa kimya na hawakuonana tena hadi
aliposikia kesho yake kuwa ameuawa kikatili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni