Idadi ya waliouawa Misri imefikia 51 na waliojeruhiwa ni zaidi ya
400.Ujerumani imetaka kufanywe uchunguzi huru kuhusiana na
mauaji hayo ya waandamanaji waliokuwa wanamuunga mkono rais
aliyeng'olewa madarakani nchini Misri, Muhammed Mursi, leo alfajiri
na jeshi la nchi hiyo. Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imetoa
taarifa leo mjini Berlin ikielezea kushitushwa kwake na mauaji hayo
na kuzitaka pande zote husika kujizuia kumwaga damu ikiongeza
inahofia ghasia hizo zinazidi. Kundi la Udugu wa Kiislamu limesema
wafuasi wake wameuawa na vikosi vya usalama walipokuwa
wakisali nje ya makao makuu ya jeshi mjini Cairo.Rais wa muda wa
Misri, Adly Mansour, pia ameitisha uchunguzi rasmi kuhusiana na
mauaji hayo ya leo. Msemaji wa serikali ametoa taarifa kuwa
mipango ya kuunda serikali ya muungano itaendelea licha ya matukio
hayo ya leo. Qatar nayo imeyalaani mauaji hayo na kutaka
kusitishwa kwa ghasia mara moja, huku Umoja wa Ulaya ukisema
unatathimini ahadi zake za kuipa nchi hiyo misaada ya mabilioni ya
euro kutokana hali tete iliyopo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni