Hali ya taharuki yatanda nchini Misri

Maafisa wa Afya Misri wamesema
takriban watu 42 wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Cairo nje ya kambi ya
kijeshi ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi
walikua wamekusanyika na wanaamini anazuiliwa hapo. Watu wengine 300
wamejeruhiwa.
Kundi la Muslima Brotherhood limewataka raia wa
Misri kuwapinga wale linawaita wanaopokonya raia uhuru na demokrasia.
Brotherhood imelaumu jeshi kwa kuwaua raia wake.Haya yanajiri huku ghasia zikiendelea baada ya kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi.
Waandamanaji hao wanasema vikosi maalum viliwafyatua risasi baada ya swala ya fajir huku wengine wakishambuliwa walipokusanyika nje ya makao ambako bwana Morsi anadhaniwa kuzuiliwa wakitaka watawala kumwachilia huru.
Msemaji wa chama cha Muslim brotherhood amesema kuwa idadi ya waliofariki katika ghasia hizo imefikia 30 huku zaidi ya watu 500 wakijeruhiwa.
Lakini katika taarifa yake, jeshi la nchi hiyo limesema kuwa kundi moja la kigaidi lilikuwa likijaribu kuingia katika kambi hiyo na kumuua mwanajeshi mmoja.
Limeongezea zaidi ya watu 200 walitiwa mbaroni wakimiliki silaha kama vile visu.
Duru kutoka wizara ya afya zilisema kuwa afisaa mmoja wa jeshi aliuawa.
Bwana Morsi, aliyekuwa rais wa kwanza wa kiisilamu kuchaguliwa kidemopkrasia Misri, aling'olewa mamlakani na jeshi, siku ya Jumatano baada ya kufanyika maandamano makubwa.
Mmoja wa waandamanaji Mahmud al-Shilli, aliambia shirika la habari la AFP kuwa wanajeshi waliwarushia gesi ya kutoa machozi lakini kikundi cha wanaume waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia ndio waliwafyatulia risasi.
Katika taarifa iliyosomwa kwenye vyombo vya yhabari vya serikali, jeshi lililaumu kikundi cha watu wlaiokuwa wamejihami ambao limesma ni mgaidi waliokuwa na njama ya kuvamia kambi ya jesh
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni