Idadi ya vifo vilivyotokana na
mapambano ya ijumaa kati ya wafuasi na wapinzani wa rais aliyeondolewa
madarakani wa Misri Mohammed Morsi imeongezeka na kufikia 139. Kwa
mujibu wa taarifa ya chama cha Muslim Brotherhood, watu 120 wameuawa na
wengine zaidi ya 4,500 kujeruhiwa katika mapambano kati ya wafuasi wa
Morsi na maafisa wa usalama karibu na msikiti wa Rabaa al-Adaweya mjini
Nasr. Muslim Brotherhood imesema wengi wa wahanga hao walikuwa na
majeraha ya risasi kichwani, shingoni na kifuani ambayo walipata kutoka
kwa walenga shabaha.Vikosi vya polisi vinadaiwa kufyatua risasi
kutawanya umati wa wafuasi wa Morsi waliokuwa wamekusanyika katika kambi
ya kijeshi katika mtaa wa Naser. Ijumaa, mapambano makali kati ya
wafuasi na wapinzani wa Mohammed Morsi yalitokea katika mkoa wa
Alexandria na mikoa mingine nchini Misri na kusababisha vifo vya watu
19.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni