Hitilafu na mizozo baina ya makundi ya kigaidi nchini Syria
imeshadidi zaidi na waasi hao wameendelea kupigana na kuuana wenyewe kwa
wenyewe. Taarifa nchini Syria zinasema kuwa, mapigano hayo yaliyojiri
baina ya magaidi wa Jeshi Huru la Syria na Jabhat an-Nasra yamepelekea
makumi ya magaidi wa pande mbili kuuawa. Mapigano hayo yanaripotiwa
kutokea katika maeneo mbalimbali ya mji wa Idlib ulioko kaskazini
magharibi mwa Syria. Hitilafu hizo ambazo katika siku za hivi karibuni
zimeshadidi mno chanzo chake kinatajwa kuwa ni juhudi zao za kuwania
madaraka na uongozi wa kusimamia makundi yote ya magaidi nchini humo.
Hivi karibuni Muadh al Khatib mkuu aliyejiuzulu wa muungano wa wapinzani
wa Syria, alikiri kuongezeka mpasuko kati ya wapinzani na kusema kuwa,
baadhi yao hawakubaliani na mapendekezo ya muungano huo bali
wanachokipigania wao ni madaraka na maslahi yao binafsi. Wakati huo huo,
magaidi 120 wa Syria wameuawa katika maeneo mbalimbali ya kaskazini mwa
nchi hiyo kufuatia mashambulio ya jeshi la nchi hiyo katika ngome za
magaidi hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni