Ijumaa, 19 Julai 2013

Mugabe: Waafrika wanauawa bila hatia Marekani


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema kuwa Marekani imezama katika ubaguzi na ameitaka serikali ya Washington kuondoa pua yake katika masuala ya ndani ya nchi za Kiafrika.
"Marekani imepatwa na kichaa", amesisitiza Mugabe katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa rais kwenye mji wa Chinhoyi wa kaskazini mwa Zimbabwe. Amesema kuwa Marekani haina sifa ya kimaadili ya kuweza kuikemea Zimbabwe na kuongeza kuwa, jela za Marekani zimejaa raia wenye asili ya Afrika. Ameuliza iko wapi demokrasia nchini Marekani ambako amesisitiza, kumejaa ubaguzi.
Wakati wa safari yake nchini Afrika Kusini, Rais Barack Obama wa Marekani aliitaka Zimbabwe kufanya marekebisho kabla ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Hata hivyo Mugabe amewauliza viongozi wa Marekani akisema: Mumepata wapi ujasiri wa kuwapa nasaha Waafrika wakati nchi yenu imejaa ubaguzi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni