Jumanne, 16 Julai 2013

Makinda ahofia uchaguzi wa 2015 Tanzania

  Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda, amesema kuwa, kuna hatari ya uchaguzi wa mwaka 2015 kwa Tanzania Bara kutofanyika ikiwa mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba yaliyopendekezwa na Tume ya Katiba yatapita kama yalivyo. Makinda ambaye pia ni Mbunge wa Njombe Kusini (CCM) amesema kwamba, ikiwa mapendekezo hayo yatatipishwa na wananchi kama yalivyo, Tanzania Bara haitaweza kuingia katika uchaguzi kwa vile haitakuwa na katiba. Wakati Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza hayo, tayari Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeshatangaza kuandaa mfumo wa uendeshaji wa mikutano ya mabaraza kuanzia Julai 12 hadi Agosti 2, mwaka huu. Spika Makinda amewataka Watanzania kuisoma rasimu ya Katiba hiyo hiyo vizuri na kuonyesha wasiwasi wake juu ya taifa la Tanzania kuwa na serikali tatu.  Makinda amesema kwa mshangao juu ya maoni ya kuwa na serikali tatu na kusema,  nchi hii itakuwa na marais watatu, maspika watatu, mabunge matatu, majeshi matatu na benki kuu tatu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni