
- Jambo baya zaidi kwake ni kuwa hana vyanzo vya mapato vya kueleweka.
- Anaendelea kusimulia kwamba wakati anaugua amekumbwa na mkasa wa binti yake (jina linahifadhiwa) kukatiza masomo kutokana na ujauzito.
WIKI iliyopita tulianza kuona namba
mwigizaji, msanii wa vichekesho ambaye pia ni mcheza ngoma za makabila
mbalimbali wa Tanzania, Small Wangamba ‘Mzee Small’ anavyosimulia mateso
yake ya sasa yanayotokana na maradhi ya kiharusi. Bado hajapata
matibabu ya maana kutokana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa kukosa uwezo
kifedha, endelea…
Mzee Samal anasema alihangaika maeneo tofauti
kupata tiba na kuna wakati shabiki wake mmoja aliwekeza fedha katika
zahanati moja (jina halikumbuki) iliyopo eneo la Kariakoo ambao alikuwa
anapata huduma ya kuchuliwa misuli.
“Huyo mtu alisikia naumwa akatafuta namba zangu za
simu kisha akanipigia na kunielekeza sehemu ya kwenda kuchuliwa kwani
nae aliwahi kukumbwa na tatizo kama hilo la kupooza mkono, lakini
alipata nafuu kidogo,” anasema.
Small anasema tiba hiyo ya kuchuliwa viungo ilimpa
nafuu kiasi lakini haikumuwezesha kurejea hali ya kawaida na siku za
karibuni mambo yamebadilika. Hivi sasa sehemu ya mkono inapoungana na
bega inaachana hali ambayo anasema inazidi kumchanganya.
Hali yake kiuchumi
“Mkono unakuwa kama unatengana na bega na mbaya
zaidi nazidi kuishiwa nguvu na sina uwezo walau wa kujikokota na
kutembea,” anasema na kuongeza kuwa hivi sasa hawezi kufanya shughuli
yoyote zaidi ya kula na kulala.
Jambo baya zaidi kwake ni kuwa hana vyanzo vya mapato vya kueleweka.
“Pesa pekee ambazo zinanisaidia kidogo ni za kuuza
maji, haponndiyo napata fedha ya kula na mke wangu Fatma Binti Saidi,”
anasema.
Anaendelea kusimulia kwamba wakati anaugua
amekumbwa na mkasa wa binti yake (jina linahifadhiwa) kukatiza masomo
kutokana na ujauzito.
Ilikuwa mwaka jana wakati binti hiyo akiwa Kidato cha Tatu.
“Watu wamemtia mimba mwanangu wa kike ambaye
alikuwa ni wa tatu, lakini bahati nzuri aliyefanya hivyo ameamua kumuoa,
basi sasa nitafanya nini na mimi hali yangu kama unavyoiona?” Anasema
na kuongeza kuwa hata hivyo hajakata tamaa.
source mwanasport
source mwanasport
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni