Maandamano ya wenye chuki dhidi ya Uislamu Uingereza
Wimbi la siasa za kuchafua sura safi ya Uislamu na kuyavunjia
heshima matukufu na maeneo ya Kiislamu nchini Uingereza linaonesha kasi
kubwa ya sera za chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) na kuidhihirisha
dini hiyo kuwa ni tishio.
Mlipuko uliotokea Ijuma iliyopita katika mji wa Tipton katika eneo la West Midlands katikati mwa Uingereza karibu na msikiti wa Waislamu wa eneo hilo wakati Waislamu waliokuwa kwenye ibada ya swaumu walipokuwa wakielekea msikitini hapo, uliwatia hofu kubwa wakazi wa maeneo hayo. Mlipuko huo ulitokea katika Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ripoti za tukio hilo hazikuweka wazi hasara zilizosababishwa na mlipuko huo wala sababu yake.
Wiki mbili kabla ya tukio hilo watu wenye sera za kuuhujumu Uislamu walishambulia msikiti wa Worcestershire huko magharibi mwa Uingereza na kuuvunjia heshima msikiti huo.
Kundci la watu liliuvamia msikiti huo na kupora vitu vyote vya thamani vilivyokuwemo baada ya kuuvunjia heshima. Watu hao pia walichora nembo ya kundi la chama kinachoeneza chuki na propaganda chafu dhdi ya Uislamu nchini Uingereza la EDL katika kuta za msikiti huo.
Hii ni mara ya pili msikiti huo wa Worcestershire kuvamiwa na wafuasi wa makundi yanayopiga vita Uislamu nchini Uingereaza.
Wakati huo huo katika siku chache zilizopita makundi yanayuhujumu Uislamu na vyama vya mrengo wa kulia na vyenye misimamo mikali vilipinga vikali uamuzi wa Kanali ya 4 ya Televisheni ya BBC ya Uingereza ya kurusha hewani adhana katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Mwanachama mmoja wa chama kinachojitegemea cha UKIP chenye mielekeo mikali ya mrengo wa kulia amemshambulia kwa maneno mkurugenzi wa kanali hiyo akimtuhumu kwamba amechukua hatua hiyo kwa shabaha ya ria na kujionesha.
Vilevile ripoti mpya zilizotolewa nchini Uingereza zinasema kuwa, baada ya matukio ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani, Waislamu wamekuwa wakishambuliwa na kukabiliwa na maudhi ya aina mbalimbali. Tangu wakati huo karibu nusu ya misikiti na vituo vyote 700 vya Kiislamu nchini Uingereza vimeshambuliwa na watu wenye sera za kuupiga vita Uislamu.
Ripoti hiyo imeendelea kusema kuwa, hujuma dhidi ya Uislamu na Waislamu pia imeshadidi mno katika mitandao ya intaneti. Wafuasi wa makundi hayo yanayohujumu Uislamu pia wamekuwa wakivihusisha vitendo vyote vya kigaidi na Uislamu kwa nia ya kuwapaka matope Waislamu na kutaka kuhalalisha ukatili na vitendo vyao viovu vya kushambulia misikiti na maeneo ya Kiislamu.
Matokeo ya uchunguzi uliofanywa na gazeti la Independent pia yameonesha kuwa tangu baada ya kuuawa mwanajeshi wa Uingereza Lee Rigby mwezi Mei mwaka huu, mashambulizi na hujuma dhidi ya Waislamu imeongezeka mara kumi. Tangu wakati huo Waislamu wamekuwa wakishambuliwa katika maeneo mbalimbali ya Uingereza na hata kutumiwa vichwa vya nguruwe mbele ya milango ya majumba yao.
Kutokuwepo azma thabiti kwa wanasiasa wa Uingereza ya kukabiliana na wimbi ya kuhujumu dhidi ya Uislamu na kasi ya kuchafua jina na sura ya Uislamu katika vyombo vya habari vya nchi hiyo vinawatia wasiwasi mkubwa wanaharakati wa haki za binadamu kuhusu uwezekano wa kushadidi ukatili na unyama dhidi ya wafuasi wa dini hiyo.
Arzu Mirali ambaye ni miongoni mwa wanaharakati wa haki za binadamu nchini Uingereza anasema, ripoti za hivi karibu kuhusu wimbi la hujuma dhidi ya Uislamu nchini humo zinaonesha kuwa, hujuma na mashambulizi dhidi ya Uislamu yanaongezeka kwa kasi kubwa. Mirali ameongeza kuwa, serikali ya Uingereza haijachukua hatua yoyote ya maana ya kupambana na vitendo vya kuuhujumu Uislamu na Waislamu nchini humo na si hayo tu, bali ushahidi unaonesha kuwa, wakati mwingine imekuwa ikifanya uchochezi dhidi ya Waislamu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni