Misri imetangaza kuanza
uchunguzi wa makosa ya jinai kwa rais Mohamed Morsi aliyeondolewa
madarakani. Idara ya uendeshaji mashitaka ilisema Morsi ameripotiwa
kuhusika na vitendo vya ujasusi, kuchochea matukio ya kimabavu na
kuharibu uchumi.
Habari kutoka kituo cha televisheni cha Al-Jazeera zimesema ofisi ya mwendesha mashitaka ya serikali ya Misri imepata ripoti dhidi ya Morsi na viongozi wengine wanane akiwemo wa Chama cha Muslim Brotherhood Bw. Mohamed Badie. Idara ya uendeshaji mashitaka itaamua kama itawashitaki watu hao baada ya matokeo ya uchunguzi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni