Wafungwa zaidi ya 1,000 wametoroka jela karibu na mji
wa Benghazi Mashariki mwa Libya huku waandamanaji wakiendelea kuvamia
ofisi za vyama vya kisiasa nchini humo.
Maafisa wa usalama wanasema wafungwa hao walitoroka Jela ya
al Kweifiya siku ya Jumamosi. Imedaiwa kuwa waliotoroka ni pamoja na
raia kadhaa wa kigeni kutoka nchi za Afrika waliohusishwa na utawala
uliotimuliwa madarakani wa Muammar Gaddafi.
Waziri Mkuu wa Libya Ali Zeidan amethibitisha kutokea tukio
hilo na kusema wakaazi wa eneo hilo ndio waliowasaidia wafungwa
kutoroka kwa sababu hawataki jela karibu na nyumba zao.
Hadi sasa wafungwa 18 waliotoroka wamekamatwa huku baadhi
wakirejea wenyewe gerezani. Katika siku za hivi karibuni kumeibuka
maandamano makubwa nchini Libya kufuatia mauaji ya mwanaharakati ambaye
alikuwa mkosoaji wa Harakati ya Ikwanul Muslimin. Ofisi kadhaa za
harakati hiyo zimeteketezwa moto mjini Benghazi na katika miji mingine
ya Libya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni