Jumapili, 28 Julai 2013

Banyamulenge waishio DR Congo walilia usalama wao

Baadhi wa wapiganaji waasi wa M23 wakiwa kambini Rumangabo DRC waasi hawa wanatuhumiwa kukiuka haki za binadamu kwa kuwatesa raia
Baadhi wa wapiganaji waasi wa M23 wakiwa kambini Rumangabo DRC waasi hawa wanatuhumiwa kukiuka haki za binadamu kwa kuwatesa raia
Reuters/James Akena

Wakati mapigano yanaendelea Huko mashariki mwa Jamhuri Ya Kidemokrasia ya Congo,DRC Watu wanaozungumza lugha ya Kinyarwanda al maarufu kama Banyamulenge wamevilaumu vyombo vya usalama na raia kuendelea kuwanyanyasa huku Viongozi wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini wakisema watahakikisha usalama wa raia hao.

Katika mazungumzo na Gavana wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini raia hao kutoka kabila la Banyamulenge waliilaumu serikali ya Rwanda pamoja na waasi wa Kundi la M23,kutetea vita vya mashariki mwa Drc kuwa ni kwa lengo la kusaka maslahi ya wanyarwanda.
Kwa upande wao Viongozi wa serikali pamoja na wale wa kijeshi wamesema tayari wamefanikiwa kusuka mikakati iliyo thabiti ili kuhakikisha kwamba usalama wa Banyamulenge unazingatiwa katika Jimbo nzima la Kivu ya Kaskazini.
Hayo yanajiri wakati Hali ya wasi wasi inazidi kutanda katika mji wa Kiwanja ulioko umbali wa kilomita takribani hamsini kaskazini mwa Jiji la Goma ambapo imeripotiwa kuwa zaidi ya watu mia mbili waliozingirwa Wakati wa Mkutano wa Hadhara ulioshikiliwa na M23 Alhamisi iliyopita wanaendelea kushikiliwa,kupigwa na kuteswa katika Gereza la Nyongera.
Mashirika ya kimataifa na Asasi za kiraia Huko Kivu ya Kaskazini yanasema kuna Hofu kwamba huenda baadhi ya Watu watakuwa wameuawa,au kukumbwa na majeraha makali kufuatia Vichapo wanavyopigwa na Waasi waM23.
Hata Hivyo M23 Hawajathibitisha wala kukanusha taarifa zinazohusiana na kukamatwa kwa watu katika Mji wa Kiwanja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni