
Rais wa Syria, Bashar Al Assad
worldpress.com
Rais wa Syria Bashar al-Assad amesema kuwa mgogoro wa Syria
unaweza kutatuliwa kwa kufutilia mbali ugaidi, akimaanisaha waasi
wanaopambana na serikali yake.
Katika hotuba yake nadra kwenye televisheni ya taifa hilo jana
Jumapili, Assad aliukosoa upinzani wa kisiasa dhidi ya utawala wake na
kuulezea kushindwa na kwamba hauna nafasi yoyote katika kutatua vita ya
kikatili nchini humoAssad ameongeza kuwa hakuna suluhu inayoweza kufikiwa pamoja na waasi isipokuwa kwa kupambana nao kwa ngumi ya chuma na kwamba hatua ya sasa si ya kutafuta suluhu bali kuwafutilia mbali.
Mnamo Machi 2011, maandamano makubwa yalienea maeneo mbalimbali kwa ajili ya wito wa mabadiliko ya kisiasa nchini Syria ambapo hadi hivi sasa maelfu ya raia wamepoteza maisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni