Edward Snowden anatafutwa na Marekani kwa kuvujisha taarifa za siri juu ya miradi ya siri ya kijasusi ya Marekani
Reuters
Serikali ya Rais wa Marekani,Barack Obama ilikuwa na matumaini
ya kurejesha uhusiano uliokuwa ukiyumba, lakini Rais wa Urusi, Vladmir
Putin ameelezwa kuwa amekuwa mgumu katika jitihada za kurejesha
mahusiano mazuri.
Snowden anatafutwa na Marekani kwa kuvujisha taarifa za siri juu ya miradi ya siri ya kijasusi ya Marekani na alikuwa amekwama katika uwanja wa ndege wa jijini Moscow kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Urusi imekataa kumkabidhi Snowden kwa Marekani, zaidi, hapo jana Urusi ilimpatia Snowden hifadhi ya kipindi cha mwaka mmoja, hatua iliyoighadhabisha Marekani huku ikielezwa kuwa nchi hiyo imeharibu uhusiano ambao tayari ulikuwa na dosari juu ya tofauti za misimamo juu ya syria kati ya nchi hizo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni