Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kukomeshwa
machafuko na ghasia nchini Misri baada ya mauaji ya mamia ya
waandamanaji Jumatano iliyopita.
Baraza la Usalama pia limezitaka pande zote husika kuwa na ustahamilivu na kusisitiza kwamba wanachama wote wa baraza hilo anasikitishwa na mauaji ya watu na ametoa mkono wa pole kwa familia za wahanga hao.
Balozi wa Argentina katika Umoja wa Mataifa ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa Baraza la Usalama Maria Cristina Perceval amesema baada ya kikao cha baraza hilo kilichomalizika alfajiri ya leo kujadili hali ya Misri kwamba wanachama wote wanasisitiza juu ya udharura wa kukomeshwa machafuko nchini humo na kuwa na kiwango cha juu ya ustahamilivu. Amesema kuna udharura wa kufanyika mapatano ya kitaifa nchini Misri.
Jamii ya kimataifa imeendelea kulaani mauaji yaliyofanywa na askari usalama wa Misri dhidi ya waandamanaji katika mji wa Cairo na maeneo mengine ya Misri. Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa ikisema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalaani vikali mauaji hayo na inatahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea vita vya ndani nchini Misri.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni