Ijumaa, 16 Agosti 2013

Maandamano ya Ijumaa ya ghadhabu kufanyika leo Cairo

Harakati ya Kutetea Serikali Halali ya Misri imetoa wito wa kufanyika maandamano ya Ijumaa ya Ghadhabu hii leo baada ya Swala ya Ijumaa mjini Cairo. Harakati hiyo imewataka wafuasi wote wa kiongozi aliyeondolewa madarakani nchini Misri Muhammad Mursi wakusanyike katika Medani ya Ramsis katikati mwa jiji la Cairo.
Wito huo wa maandamano ya mamilino ya Wamisri umetolewa siku chache tu baada ya kikosi cha usalama cha Misri kushambulia ngome za wafuasi wa Mursi na kuua mamia ya watu katika Medani za Rabia al Adawiyyah na al Nahdha. Wizara ya Afya ya Misri imetangaza kuwa watu 640 waliuawa katika machafuko hayo na wengine zaidi ya 4000 kujeruhia, lakini Harakati ya Ikhwanul Muslimina inasisitiza kuwa, watu waliouawa na jeshi la Misri ni zaidi ya elfu mbili.
Wakati huo huo serikali ya Misri imetangaza kuwa jeshi la nchi hiyo litakabiliana kwa nguvu zote na maandamano ya aina yoyote
sikiliza hapa

http://www.dw.de/popups/mediaplayer/mediaId_4128445

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni