Jumatatu, 12 Agosti 2013

Bunge laanza kuchunguza mawaziri wa Rais Rohani


Majlisi ya Ushauri ya Kiislanu ya Iran leo imeanza kuchunguza majina yaliyowasilishwa na Rais Hassan Rohani kwa ajili ya nafasi za wizara katika serikali yake.
Akihutubia Bunge kabla ya kuanza kujadili majina na mawaziri waliopendekezwa, Dakta Hassan Rohani amesisitiza juu ya umuhimu wa ushirikiano wa Majlisi ya Kiislamu na Serikali na kusema amependekeza majina ya watu wenye uzoefu mkubwa katika masuala mbalimbali ya utawala.
Rais Rohani amesema kuwa, ili kuweza kukabiliana na matatizo mbalimbali serikali inawajibika kutilia maanani masuala mawili ambayo ni kushinda changamoto za kimataifa na kutafuta vyanzo mbalimbali vya pato la taifa na kulitumia kwa njia mwafaka.
Amesisitiza kuwa serikali yake haikujengeka kwa msingi wa mitazamo ta vyama na makundi ya kisiasa na kusema suala lililopewa kipaumbele zaidi katika kuteua mawaziri ni misimamo ya wastawi na ustahiki.
Vikao vya kuchunguza ustahiki wa majina ya waliopendekezwa bungeni na Rais Rohani kwa ajili ya nafasi za wizara mbalimbali vitaendelea kwa siku kadhaa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni