Chama cha Wananchi, CUF, Zanzibar nchini Tanzania kimeelezea
kushtushwa na tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa Uingereza
katika maeneo ya Mji Mkongwe Zanzibar. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo
vya habari na Salim Biman, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari,
Uenezi, Mawasiliano na Umma imesema CUF inalaani kwa nguvu zote tukio
hilo la kikatili la kuwamwagia tindi wageni hao ,na kinawataka polisi
Zanzibar kufanya uchunguzi wa kina na waharaka pamoja na kuhakikisha
kuwa wale wote waliohusika na tukio hilo la kikatili wanakamatwa na
kufikishwa katika vyombo vya sheria. Taarifa ya Chama cha CUF imesema
kama ninavyonukuu, “hii ni dalili mbaya kwa Zanzibar kwani matukio haya
ya tindikali yamekuwa yanaonekana kama ni masuala ya kawaida jambo
ambalo linatishia uchumi wa Visiwa vyetu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni