Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hakuna kibali chochote kimataifa cha kuingilia kijeshi nchini Syria. Abbas Araqchi ameyasema hayo kufuatia matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel kwamba nchi yake inachunguza machaguo kadhaa kwa ajili ya kuingilia kijeshi nchini Syria. Araqchi amesema Iran imeshatangaza mara kadhaa kuwa hakuna njia yoyote ya utumiaji nguvu za kijeshi itakayoweza kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria na kwamba matokeo ya kauli na hatua za kichochezi ni kuifanya hali ya eneo iwe tata na ya wasiwasi zaidi. Radiamali ya Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran inafuatia matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Ulinzi wa Marekani kwamba baada ya Rais wa nchi hiyo Barack Obama kuchunguza machaguo mbalimbali Washington inaweza kuchukua hatua ya kuishambulia kijeshi Syria. Hayo yamejiri baada ya kanali za televisheni zinazoendesha vita vya kipropaganda dhidi ya Syria ikiwemo al Arabiyyah, Al Jazeera na Sky News kutangaza habari siku ya Jumatano iliyopita kuwa eti jeshi la Syria limetumia silaha za kemikali katika eneo la al Ghautah ya Mashariki katika mkoa wa Ruf Dimashq huko kusini mwa Syria. Sambamba na kulaani aina yoyote ya utumiaji silaha za kemikali, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kutumiwa silaha hizo wakati mmoja na kuwepo wataalamu wa silaha za kemikali wa Umoja wa Mataifa nchini Syria kunaonyesha wazi kuwa kuna njama zinazofanywa za kuielekezea serikali ya Damascus tuhuma za utumiaji silaha hizo…/
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni