Waislamu wa Mombasa Kenya katika Sala ya Idul Fitr mwaka 2013
Serikali ya Kenya imeitangaza Ijumaa ijayo kuwa sikukuu rasmi ya kitaifa kwa mnasaba wa Idul Fitr.Katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mawaziri Francis Kimemia, Ijumaa tarehe tisa Agosti itaadhimishwa kama Sikukuu ya Idul Fitr kwa mnasaba wa kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Nchi kadhaa za Kiislamu ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zinaaza kuutafuta mwezi mwandamo kesho Jumatano na iwapo mwezi wa Shawwal utaandama Alkhamisi itakuwa Idul Fitr la sivyo Ijumaa ndiyo itakayokuwa tarehe Mosi Shawwal baada ya kutimizwa siku 30 za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
source iran swahili radio
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni