Mvua nzito nchini Pakistan zimesababisha vifo vya watu wapatao 58 na
na majeruhi kwa watu 30, kwa mujibu wa mamlaka ya udhibiti wa majanga
nchini humo. Wakati huo huo, vijiji 13 vimeathiriwa na mafuriko nchini
Afghanistan. George Njogopa na taarifa kamili:
(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)
Mvua hiyo pia imeleta uharibifu mkubwa katika maeneo mengine ikiwemo
kusababisha mamia ya watu kukosa makazi baada ya nyumba zao
kuharibiwa.Mashamba pamoja na miundo mbinu ni baadhi ya maeneo mengine
ambayo pia yamevurugwa na mvua hiyo.
Ripoti zinasema kuwa, mvua inazidi kuendelea na taarifa za watabiri
wa hali ya hewa zinaonyesha kwamba kiwango cha mvua hiyo kinatazamiwa
kuongezeka katika kipindi cha mwezi huu wa Ogosti. Serikali ya Pakistan
tayari imeanzisha jitihada za uokozi kwenye maeneo yaliyoathiriwa
lakini hata hivyo haijaonyesha dalili ya kuomba msaada kutoka kwa
jumuiya ya kimataifa.
Mashirika ya kimataifa ya utoaji msaada wa usamaria mwema ikiwemo
lile la OCHA yamesema kuwa yanaendelea kufuatilia kwa karibu hali ilivyo
nchini humo, na pindi itapoona kuna ulazima wa kutoa msaada itafanya
hivyo mara moja. UM watilia shaka ustawi wa watoto walioko kwenye
makambi nchini Syria. Umoja huo umesema kuwa makambi mengi yanayohifadhi
watoto nchini Syria yanatia shaka kwani mengi yao hayana ulinzi huku
wengine wakilazimika kujiingiza kwenye kazi ili kuzisaidia familia zao.
Kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, baadhi ya watoto wa kike
wanaolewa wakiwa katika umri mdogo na wengine wanachukuliwa na
kuingizwa kwenye makambi ya kijeshi na kugezwa wapiganaji. Mashirika
hayo lile la kuhudumia watoto UNICEF na lile linalohusika na wakimbizi
UNHCR yameanzisha juhudi za kutambua matatizo hayo ili hatimaye
kuyatafutia ufumbuzi.
Kwa upande wake UNHCR imesema kuwa inafanya kila liwezekanalo ili
kuhakikisha kwamba wanawake wajawazito wanafikiwa na huduma bora za
kiafya wakati wa kujifungua.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni