Mahakama Kuu nchini Uturuki imemhukumu mkuu wa zamani wa jeshi la
nchi hiyo kifungo cha maisha jela baada ya kumpata na makosa ya
kushirikiana na wanajeshi waliopanga kuipindua serikali mwongo mmoja
uliopita. Ilker Basbug anadaiwa kushirikiana na zaidi ya wanajeshi 1000
kupanga mapinduzi ya kijeshi. Polisi wamelazimika kutumia gesi ya kutoa
machozi kuwatawanya wafuasi wa Basbug nje ya mahakama hiyo magharibi mwa
mji wa Istanbul. Watu wengine 21 wamefutiwa mashtaka kwenye kesi hiyo
huku wengine wakihukumiwa vifungo vya kati ya miaka 12 hadi 20 jela.
Wachambuzi wengi wanasema kuwa, Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip
Erdogan ametumia kesi hiyo kuwaandama na kuwanyamazisha wapinzani na
wakosoaji wa chama chake cha AKP.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni