Jumatatu, 12 Agosti 2013

Sijali maneno ya wanaopinga ushindi wangu

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe leo amehutubia taifa kwa mara ya kwanza baada ya kutangazwa mshindi katika ushaguzi mkuu uliofanyika Julai 31 mwaka huu.
Mugabe ameashairia upinzani wa Morgan Tsvangirai dhidi ya ushindi wake na kusisitiza kuwa, atashikilia nafasi yake kama mshindi wa uchaguzi wa Julai 31 mbele ya madai ya wapinzani.
Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe ilitangaza kuwa Robert Mugabe alimshinda mpinzani wake mkuu Morgan Tsvangirai katika uchaguzi huo kwa kupata asilimia 61 ya kura zilizopigwa.
Kiongozi wa chama cha MDC Morgan Tsvangirai amesema kulifanyika udanganyifu mkubwa katika uchaguzi huo na amesusia sherehe za kuapishwa Rais Mugabe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni