Jumapili, 18 Agosti 2013

Ulimwengu waendelea kulaani mauaji ya Misri



  Huku nchi ya Misri ikiendelea kushuhudia maandamano na hali ya mchafukoge, ulimwengu umeendelea kulaani mauaji ya raia wasio na hatia yanayofanyika nchini humo.
William Hague Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amelaani vitendo vyote vya utumiaji nguvu nchini Misri vinavyosababisha umwagaji damu. Vilevile Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwa mara nyinmgine tena amekosoa utumiaji wa nguvu za ziada dhidi ya wafuasi wa rais aliyepinduliwa wa Misri Muhammad Mursi na ametoa wito wa kukomeshwa machafuko na umwagaji damu nchini humo. Wakati hayo yanaripotiwa mwanasiasa maarufu wa Italia Beppe Grillo amezikosoa nchi za Magharibi kwa uingiliaji wao kwa siri katika ukandamizaji wa raia nchini Misri na ametaka kuundwe korti ya kimataifa ya kuwahukumu waliohusika katika mauaji hayo.
Agosti 16 vikosi vya serikali vya Misri vilishambulia kambi za wafuasi wa Mursi na kuua mamia ya watu ambapo Harakati ya Ikhwanul Muslimin inasema kuwa watu 2,200 waliuawa.  Pia taarifa zinasema kwamba tangu Ijumaa waandamanaji wengine zaidi ya 170 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa na vikosi vya usalama vya Mis

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni