Jumapili, 18 Agosti 2013

Wafuasi wa Mursi kuendelea kuandamana Misri

\
Wananchi wanaomuunga mkono Muhammad Musri rais aliyepinduliwa wa Misri kwa mara nyingine wamepanga kuandamana hii leo katika mji mkuu wa nchi hiyo Cairo, huku harakati ya Ikhwanul Muslimin ikitoa wito wa kujitokeza kwa wingi wananchi kwenye maandamano hayo. Taarifa iliyotolewa na 'Muungano wa Kupinga Mapinduzi ya Kijeshi' imesema kuwa, maandamano kadhaa yamepangwa kufanyika leo katika maeneo mbalimbali ya Cairo katika kuendeleza kupinga watawala wa kijeshi nchini Misri.
Hayo yanajiri katika hali ambayo Baraza la Mawaziri la Misri linapanga kujadili mgogoro wa nchi hiyo huku Rais Adly Mansour wa serikali ya mpito akitoa pendekezo la kupigwa marufuku Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya nchi hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni