Ijumaa, 23 Agosti 2013

Wakaazi wa Goma, Kongo wakabiliwa na hali mbaya'


'Wakaazi wa Goma, Kongo wakabiliwa na hali mbaya'
Mkuu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Kongo, amesisitizia udharura wa kuongezwa ulinzi kwa ajili ya wakaazi wa mji wa Goma. Martin Kobler, aliyechaguliwa hivi karibuni kuongoza vikosi hivyo vya Umoja wa Mataifa MONUSCO huko nchini Kongo, ameashiria machafuko ya hivi karibuni katika mji huo ambao ni makao makuu ya mkoa wa Kivu kaskazini na mashariki mwa Kongo kwa ujumla na kusema kuwa, kuna udharura wa kuchukuliwa hatua za lazima za kuwalinda wakazi na kuzuia kusonga mbele wanamgambo wa waasi wa Harakati ya M23. Katika upande mwingine Msemaji wa vikosi vya MONUSCO kanali Prosper Basse, amesema kuwa, kutokana na kuongezeka mashambulizi ya M23 katika viunga vya mji wa Goma, vikosi hivyo vitaendelea kushirikiana bega kwa bega na jeshi la Kongo FARDC katika kupambana na waasi hao. Takwimu mpya zinaeleza kuwa, mashambulizi ya jana Alkhamisi katika vijiji vya karibu na mji wa Goma, yamepelekea raia wanne kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Novemba mwaka jana, waasi wa M23 waliudhibiti mji huo hadi Desemba Mosi mwaka huo, na kulazimika kuondoka mjini hapo, kufuatia mashinikizo ya nchi za eneo la Ukanda wa Maziwa Makuu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni