
Hakuna kipato bila baiskeli
Mara nyingi watu wanahitaji muda wa masaa mengi kwenda shuleni au kwenda kuchota maji, kutafuta kuni au chakula. Katika maeneo mengi hakuna usafiri wa umma, magari yanauzwa kwa bei kubwa sana. Hivyo wakati mwingine watu wanashindwa kusafirisha bidhaa zao. Lakini mkulima huyu amepata suluhisho. Anaweza kupeleka bidhaa zake sokoni kwa kutumia baiskel

MATUMIZI YA BAISKELI AFRIKA
Bidhaa za dukani
Mtu anayemiliki duka bila kuwa na gari la kusafirishia mizigo lazima atafute mbinu ya kubeba bidhaa mpya kwa ajili ya duka lake. Nchini Tanzania bidhaa hizo hutolewa mijini na kupelekwa sehemu za ndani kabisa vijijini. Waafrika wengi wanapenda kunywa coca cola hivyo muuzaji anayeweza kubeba masanduku mengi ya kinywaji hicho atafaidika.
Safari na familia Malawi
Katika nchi nyingi za Kiafrika baiskeli hutumiwa kama teksi. Kiti cha nyuma cha kubebea mizigo hutengenezwa vizuri ili abiria aweze kukaa. Baskeli hizo zina majina tofauti. Tanzania, Kenya na Uganda zinaitwa "boda boda", jina linalotokana na maneno ya kiingereza "border to border" - mpaka hadi mpaka. Hii ni kwa sababu katika miaka ya 1960 zilitumika zaidi kwenye maeneo ya mipakani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni