Ijumaa, 20 Septemba 2013

Kimbuga Manuel chapungua kasi

Kimbuga Manuel kilichoipiga pwani ya magharibi ya Mexiko kimepungua makali na kugeuka dhoruba ya kitropiki, inayoambatana na mvua kubwa pamoja na upepo mkali. Mexiko inaomboleza vifo vya watu 80 waliouawa na mafuriko yaliyosababishwa na vimbunga, na bado watu 58 hawajulikani waliko.
Kituo cha kuchunguza vimbunga kilicho Miami nchini Marekani, kimesema upepo wa kimbunga Manuel ulikuwa ukivuma kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa, huku kasi hiyo ikitegemewa kupungua zaidi leo Ijumaa.
Rais wa Mexiko, Enrique Pena Nieto, amesema nyumba kadhaa katika jimbo la milima la Pintada zilifukiwa na tope, na kuna hofu kuwa watu 58 wasiojulikana waliko huenda wakawa ndani ya nyumba hizo.
   

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni