Kampuni kubwa zaidi ya ndege nchini Ujerumani, Lufthansa, imesema leo kuwa imeagiza ndege mpya 59 za safari ndefu, zinazotumia kiwango kidogo cha mafuta, zitakazoigharimu jumla ya euro bilioni 14.
Lufthansa imesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa imeagiza ndege 34 aina ya Boeing 777-9x na nyingine 25 aina ya A350-900 kutoka kampuni ya Airbus.
Agizo hilo, ambalo limeelezwa na Lufthansa kuwa uwekezaji mkubwa zaidi kuwahi kufanywa wakati mmoja na mwekezaji binafsi nchini Ujerumani, litaipatia kundi la ndege zinazotumia mafuta kidogo ili kukabiliana na ongezeko la bei za mafuta. Kampuni hiyo imesema ndege hizo zitaanza kuwasilishwa kuanzia mwaka 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni