Jumamosi, 21 Septemba 2013

Meli za kivita za Iran zinasheheni 'drone'

                                            
                        Drone ya Iran aina ya 'Karrar' (picha ya faili)
                        Drone ya Iran aina ya 'Karrar' (picha ya faili)

Meli zote za kivita za Jeshi la Wanamaji la Iran sasa zinasheheni ndege zisizo na rubani au drone zenye uwezo wa kuruka masafa marefu baharini.
Hayo yamedokezwa na Admeli Habibollah Sayyari kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran ambaye ameongeza kuwa katika miezi michache ijayo Iran itazindua nyambizi mpya ijulikanayo kama Fateh (mshindi).
Hadi sasa Iran imezindua nyambizi kadhaa za kisasa kabisa zilizoundwa hapa nchini huku ikijikarabatia kikamilifu zile zilizonunuliwa kutoka nje ya nchi.  Admeli Sayyari amenukuliwa akisema 'hivi sasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakaribia kujitosheleza kikamilifu katika uundaji na ukarabati wa nyambizi za kisasa zaidi duniani.' Katika miaka ya hivi karibuni Iran imepiga hatua kubwa katika kujitosheleza katika sekta ya ulinzi kwa kujitengenezea zana za kivita kama vile ndege, vifaru, manoari, nyambizi na rada.
Iran imesisitiza kuwa uwezo wake mkubwa wa kijeshi si tishio kwa nchi yoyote kwani sera yake ya ulinzi imejengeka katika msingi wa kujihami.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni