Kamanda wa Vikosi vya Nchi Kavu vya Jeshi la Iran amesema kuwa, jeshi la taifa hili limejiandaa kikamilifu kwa ajili ya kukabiliana na tishio la aina yoyote ile iwe ni la anga au la nchi kavu na hata ikiwa ni katika mazingira magumu kabisa. Brigedia Jenerali Ahmad-Reza Pourdastan ameashiria moyo na ari kubwa liliyonayo jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kubainisha kwamba, vikosi hivi viko tayari kujibu chokochoko za aina yoyote ile za adui. Brigedia Jenerali Ahmad-Reza Pourdastan amesema bayana kwamba, jeshi la Iran linafuatilia kwa karibu matukio yanayojiri katika eneo na nje ya eneo hili. Kamanda huyo wa ngazi za juu wa jeshi la nchi kavu la Iran ameashiria kuwadia Wiki ya Kujihami Kutakatifu hapa nchini na kutangaza kwamba, katika wiki hiyo jeshi la Iran vikiwemo vikosi vya nchi kavu vitaonesha vifaa na zana za kisasa zilizotengenezwa hapa nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni