Serikali ya Rwanda imeamua kupandisha ushuru wa magari ya mizigo yanayopita katika mpaka wa nchi hiyo na Tanzania kutoka dola 152 za Marekani hadi 500 kuanzia tarehe 9 Septemba mwaka huu.
Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Silas Gwakabamba amesema ushuru huo mpya utaanza kutekelezwa baadaye wiki ijayo ili kuruhusu wafanyabiashara waliokuwa wamekwama mpakani humo kuweza kuendelea na safari zao. Inaripotiwa kuwa magari yapatayo 200 ya mizigo yamekwama katika eneo la Rusumo mpakani mwa Rwanda na Tanzania baada ya kutangaziwa kodi hiyo mpya. Waziri huyo wa Rwanda amesema magari hayo yataachiwa kwa sasa. Waziri Gwakabamba amesema makubaliano ya kuondolewa vikwazo vya kibiashara yaliyofikiwa mjini Mombasa, Kenya hivi majuzi hayakuishirikisha Tanzania. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa, Kigali imechukua uamuzi huo ili kulipiza kisasi hatua ya Tanzania ya kuwafukuza maelfu ya Wanyarwanda nchini humo majuma mawili yaliyopita

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni