Suala la kuishambulia kijeshi Syria imeendelea kuwa kaa la moto kwa serikali ya Rais Barack Obama wa Marekani huku kadhia hiyo ikionekana kuigawa kamati inayoshughulikia sera za nje na usalama wa taifa katika bunge la Seneti la nchi hiyo. Hapo jana kamati hiyo ilijadili ombi la Obama la kutaka kuivamia kijeshi Syria na ingawa idadi kubwa ya maseneta kwenye kamati hiyo waliunga mkono, kuna wale waliopinga na kuapa kuwashawishi wajumbe wa Congress kupinga pendekezo hilo. Balozi wa zamani wa Marekani katika Shirika la kijeshi la NATO, Kurt Volker amesema ingawa Seneti inaonekana kuwa na msimamo mmoja, huenda kukawa na mpasuko mkubwa miongoni mwa wajumbe wa Congress punde watakaporudi kutoka likizo Septemba 9. Huku hayo yakijiri, Rais Vladmir Putin wa Russia kwa mara nyingine tena ameionya Marekani juu ya kuchukua uamuzi wa upande mmoja wa kuishambulia kijeshi Syria akisema hatua kama hiyo itakuwa na madhara ya muda mrefu kwa Washington. Putin amesema hatua yoyote sharti iidhinishwe na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo Russia ni mwanachama.
Nini nawazo yako tuandikie hapo chini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni