MAMA ALEA MIMBA MIEZI 8, AITOA, AMTUPA MTOTO CHOONI
AMANDA Hein, 27, mkazi wa Pennsylvania, Marekani ameshtakiwa kwa kosa la kutoa mimba ya miezi nane na kumtupa mtoto chooni kisha kurudi kutazama mieleka ukumbini kana kwamba hakufanya unyama huo.
Watetea haki za binadamu nchini humo wamesema Hein anastahili adhabu ya kifo kwani alimuua mtoto huyo kwa makusudi.
Tukio hilo lililotokea Agosti mwaka huu, linafuatiliwa kwa karibu na watetea haki za binadamu katika mji wa Pennsylvania.
Tukio hilo lililotokea Agosti mwaka huu, linafuatiliwa kwa karibu na watetea haki za binadamu katika mji wa Pennsylvania.
Siku ya tukio, Hein alikuwa na marafiki zake watatu wa kiume, akawaaga kuwa anakwenda chooni ndipo alipokwenda kutekeleza unyama huo akidaiwa kunywa dawa ya kutoa mimba, kisha akamtumbukiza mtoto chooni na kufunika mfuniko wa choo.
Mmoja wa marafiki hao walipoona anachelewa, walimtumia ujumbe kumuuliza kama alipatwa na matatizo. Hakujibu.
Mmoja wa marafiki zake, Luis Riviera amewaambia polisi kuwa, Hein aliporudi kutoka chooni, alionekana akiwa na damu lakini hakutaka kuelezea chochote wala hakuhitaji msaada wowote, akiwa na lake moyoni.

Watetea haki za binadamu walikazia adhabu hiyo wakidai Hein anastahili adhabu kali kwani alirejea katika sehemu waliyokuwa wamekaa na marafiki zake kutazama mieleka kwa takriban saa moja mbele.
Wafanyakazi wa usafi, walikikuta kichanga hicho siku iliyofuata baada ya kubaini choo kinashindwa kupitisha uchafu.
Uongozi wa ukumbi huo ulidai Hein alikaa chooni humo kwa takriban dakika 40, akajifungua kichanga hicho kilichobakiza wiki 4 hadi 7 kabla ya kujifungua kisha kukitupia katika sinki la choo.
Uongozi wa ukumbi huo ulidai Hein alikaa chooni humo kwa takriban dakika 40, akajifungua kichanga hicho kilichobakiza wiki 4 hadi 7 kabla ya kujifungua kisha kukitupia katika sinki la choo.
Wapelelezi walifuatilia matone ya damu kutoka chooni hadi alipokaa ndipo walipojiridhisha kuwa Hein ametenda unyama huo.
Mama mzazi wa Hein, Giasen alisema alichanganyikiwa kwa kuwa alifanya tukio hilo kuwa siri yake.
“Nilitarajia angeweza hata kunitumia ujumbe wa kuniomba msaada lakini hakufanya hivyo.
Mama mzazi wa Hein, Giasen alisema alichanganyikiwa kwa kuwa alifanya tukio hilo kuwa siri yake.
“Nilitarajia angeweza hata kunitumia ujumbe wa kuniomba msaada lakini hakufanya hivyo.
“Mimi ni mama yake, kinachouumiza moyo wangu ni kwamba, hakuwahi kuja kuniomba msaada.
Giasen alisema bintiye ambaye hakuwahi kuwa na makosa yoyote, alimshangaa kwa hilo.
“Alifikiri namchukia na wala sikuwahi kumchukia. Nampenda,” alisema mama huyo.
Giasen alisema bintiye ambaye hakuwahi kuwa na makosa yoyote, alimshangaa kwa hilo.
“Alifikiri namchukia na wala sikuwahi kumchukia. Nampenda,” alisema mama huyo.
Alijaribu kumshauri kuhusiana na maswala ya uzazi lakini kwa kiasi fulani aliamini binti yake ni mtu mzima hivyo kumpa uhuru.
Giasen ambaye ni mlokole, alisema yeye na mwanaye huyo hawakuwahi kuvunjiana heshima na hata mpenzi wake hakuwahi kumfahamu.
Giasen ambaye ni mlokole, alisema yeye na mwanaye huyo hawakuwahi kuvunjiana heshima na hata mpenzi wake hakuwahi kumfahamu.
“Sikujua kuhusu ujauzito wake sababu hakuwahi kuniambia, aliishi kivyakevyake.
Siku ya tukio, mama wa kufikia wa Hein, Louiseann Hein alisema alikuwa akiishi na Hein katika mji wa Allen miezi sita kabla hajafanya unyama huo.
Siku ya tukio, mama wa kufikia wa Hein, Louiseann Hein alisema alikuwa akiishi na Hein katika mji wa Allen miezi sita kabla hajafanya unyama huo.
Hata yeye hakuwahi kumhisi kama Hein (26) alikuwa mjamzito hadi siku alipotumiwa ujumbe na watu wa uzazi wa mpango ndipo alipowataarifu kuwa anaishi naye kisha wakamtia nguvuni. Kesi inaendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni