Jumapili, 8 Desemba 2013

UCHUMBA WA MAYA, KIGOGO

KUFUATIA kuzagaa kwa ujumbe wa kumhamasisha muigizaji Mayasa Mrisho ‘Maya’ atulie ili aolewe, imebainika kuwa uchumba wa staa huyo na kigogo ambaye ni mume wa mtu, umevunjika.
Mayasa Mrisho ‘Maya’.
Ujumbe huo ulisomeka hivi: “Ndugu zangu Mayasa ni dada yetu na rafiki yetu, tumeshindwa kumshauri atulie aolewe atuletee heshima Bongo Movie mwanamke ni vituko kila siku.”
Baada ya ujumbe huo ambao aliyeusambaza hakuwa akipokea simu za dawati la Amani, paparazi wetu alimsaka Maya ambapo alisema anayesambaza ujumbe huo ana nia ya kumchafua ingawa alikiri kuwa kwa sasa hana mchumba bila kufafanua zaidi kuhusu kigogo (mume wa mtu) aliyewahi kuripotiwa kuwa naye


SOURCE--GLOBAL PUBLISHERS

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni