Niaje maanko, shwari?
Mie niko poa, kimtindo naendelea kukomaa kitaa, si unajua tena nilishachemsha skuli? Ila hili bwana sitakaa ninyamaze, kiukweli lazima niwaambie, maisha magumu sana mtaani, hasa ikiwa kichwa chako kitupu, kimejaa mabua!
Kama kawa, ile gazeti limetoka tu wiki jana, nikampata mdau mwingine. Si mnakumbuka mada yetu iliyopita, ilihusu vile enzi zetu tulivyokuwa tunasoma kwa makundi. Tofauti na mdau aliyenipigia wiki mbili zilizopita, ambaye tulikuwa tunafahamiana, huyu jamaa hatukuwahi kukutana kabla, ila tunaongea lugha moja.
Lugha moja kwa maana kwamba baada ya kukutana, tukagundua kwamba tulisoma enzi moja, ingawa yeye ni mkubwa kidogo, aliniacha madarasa kama mawili hivi. Basi tulipokuwa tumekaa tukibadilishana mawazo, mada zilipoanza kuchanganya, tukajikuta tunarejea kwenye kijiwe chetu cha madenti.
Mshkaji aliniambia mbona kila siku nawashambulia tu madenti na sisemi lolote kuhusu maticha, ambao nao kimtindo wanaboa? Kweli bwana, nikakumbuka enzi zetu, walimu walivyokuwa wakitunyanyasa, hasa sisi wavulana, pale walipohisi masilahi yao yanaguswa!

Leo nitajaribu kidogo kugusia kuhusu kasoro za walimu, ingawa hata hivyo, hawa wako kwa kiasi kidogo sana tofauti na wengi wanaofuata maadili.
Kipindi hicho pale shuleni kwetu kulikuwa na walimu kama wawili hivi, wakati ule hawakuitwa masharobaro kama tunavyoweza kuwaita sasa, bali tuliwaita macheckbob na mmoja wa kawaida tu, ila alikuwa na uchu ile mbaya kwa mabinti!

Wale macheckbob pamoja na kwamba walikuwa ni walimu na wakubwa wetu, lakini kimtindo hawakuwa wakubwa kihivyoo, kwa hiyo tuliwachukulia kama washkaji tu. Sasa hao jamaa kila mmoja alikuwa na wasichana wake wanafunzi na sisi tulikuwa tunajua. Wakati huo sisi tulikuwa wanasoka wazuri, kwa hiyo mpira ulitufanya tuwe marafiki wa wanafunzi wa jinsia zote.
Sasa huyo mwalimu mmoja akaona mshkaji wetu kama anamfuatilia msichana wake, akamuita na kuanza kumpiga mkwara mbuzi.
Sasa huyo mwalimu mmoja akaona mshkaji wetu kama anamfuatilia msichana wake, akamuita na kuanza kumpiga mkwara mbuzi.
Kwa kuwa alijua anapigwa mkwara kwa sababu ya demu, mshkaji naye akaja juu, akatishia kumdunda yule ticha au kwenda kumsemea kwa mkuu wa shule. Jamaa akanywea, baadaye akatufuata washkaji zake na kuomba apatanishwe na mchizi ili wamalize bifu. Ikawa hivyo.
Ni afadhali kidogo sisi tulikuwa wabishi wakati ule, lakini wenzetu ambao walikuwa wanyonge, walipata shida sana kutoka kwa walimu endapo nyendo zao zilionekana kugusa masilahi yao kwa wasichana.
Na ubaya ni kwamba wao wanatumia kazi zao. Wanawatishia wadada kuwapa adhabu, kuwakata maksi au kuwaandikia ripoti mbaya ingawa wakati mwingine wanawapa fedha. Wasichana kwa sababu ya uoga wao, wanakubali kirahisi.

Wasichana wanaokataa wanakutana na wakati mgumu sana shuleni, hawana raha. Wanatafutiwa makosa yasiyo na kichwa wala miguu, lakini wanapotimiza matakwa yao, hubaki salama. Enzi zetu, mabinti wengi tu walitoa mimba za walimu.
Walimu wanatengeneza bifu na wanafunzi wa kiume kwa sababu ya wasichana, matokeo yake wanashindwa kwenda sawa, kwa sababu madenti hawawezi kuwafuata kwa ajili ya msaada wa kimasomo.
Walimu wanatengeneza bifu na wanafunzi wa kiume kwa sababu ya wasichana, matokeo yake wanashindwa kwenda sawa, kwa sababu madenti hawawezi kuwafuata kwa ajili ya msaada wa kimasomo.
Matokeo yake taaluma inashuka. Walimu, ingawa wenyewe wanajua ni siri, ni lazima wajue kuwa wanafunzi wanajua kuwa wanajihusisha kimapenzi na wanafunzi wao. Mara nyingi wasichana wenyewe ndiyo husema kwa lengo la kujisifu au kuwanyamazisha wenzao.
Hii inawapunguzia heshima, kwani hata endapo walimu hao watatoa adhabu kwa wanafunzi wapenzi wao, wenzao hucheka kimya kimya na kauli kama “Eti anajifanya kumchapa, muone anavyozuga.”
Ni jambo zuri kwa waalimu kutambua kwamba wana majukumu makubwa kwa sababu wao ni walezi mbadala, vitendo vyao vinaharibu sura nzuri ya taaluma yao, ambayo ni muhimu kuliko zote, kwa vile bila walimu, hatuwezi kupata madaktari, mainjinia, maprofesa, wataalamu wa kilimo wala fani nyingine yo yote.
Hey, maticha vicheche, acheni hizo bhana!!!!
Hey, maticha vicheche, acheni hizo bhana!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni