Jumatatu, 2 Desemba 2013

WAZICHAPA WAKIGOMBEA POMBE...

AMA kweli duniani kuna vitimbi! Huwezi amini, wanaume wawili waliotajwa kwa jina mojamoja, Ndalo (45) na Songoro (62) wamenaswa wakizichapa kavukavu kabla ya kutumbukizana kwenye kinyesi wakigombea pombe ya kienyeji.
Ndalo na Songoro wakiamuliwa na msamaria mwema baada ya kutumbukia kwenye kinyesi.
Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni Maeneo ya Stendi ya Mabatini jijini dar hapa ambapo kwa mujibu wa mashuhuda wa sinema hiyo ya bure, wawili hao walipewa ofa ya pombe ya kienyeji aina ya kindi na rafiki yao aliyeondoka mapema eneo hilo.
Songoro akisindikizwa kwenda mto Mabatini kunawa baada ya kuzipiga na Ndalo.
...Songoro akinawa.
Mashuhuda hao walitiririka kuwa kabla ya kuanza kuinywa pombe hiyo ambayo hunywewa kwa kupokezana kwenye kikombe kikubwa (koronto), Ndalo aliitwa na mteja kuelekea kwenye kibanda chake kumhudumia ambapo inadaiwa kuwa alitumia muda mrefu huko wakati Songoro akikamata fursa kwa kuigida pombe yote bila kubakisha hata tone.
Ndalo naye akinawa kwenye mto Mabatini baada ya kupigana na Songoro.
Ilielezwa kuwa baada ya kurudi na kukuta pombe yote imeisha, Ndalo alianzisha timbwili kiasi cha kushikana mashati na Songoro ambaye muda huo alikuwa chakari kutokana na pombe hiyo ya ofa.
Songoro akifua shati lake lililokuwa limejaa kinyesi.
Wawili hao walizichapa kavukavu na kutumbukia kwenye tope la mtaro wenye kinyesi huku Songoro akionekana kuzidiwa nguvu na kukandamizwa almanusura apoteze uhai.
Wananchi wakiwashuhudia jamaa hao.
Hata hivyo, wawili hao walitenganishwa na wasamaria wema.
Songoro akisalimiana na mwananchi baada ya kuoga na kufua shati.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni