Argentina na hatua za kukinga watoto wa kike dhidi ya kansa ya kizazi

Mtoto wa kike akipatiwa chanjo dhidi ya kirusi cha HPV
Nchini Argentina, utoaji wa chanjo dhidi ya kirusi cha Human
Papillomavirus, HPV kwa watoto wa kike kuanzia umri wa miaka 11 ili
kuhakikisha pindi wanapobalehe wanakuwa tayari wameshapatiwa kinga dhidi
ya kirusi hicho kinachosababisha kansa ya kizazi. Mpango huo
uliopendekezwa na pia kuungwa mkono na shirika la afya duniani, WHO
umekuwa wa mafanikio katika nchi hiyo ambayo utoaji wa chanjo yoyote
haungalii hadhi ya mtu katika jamii bali kila mtu ana haki ya kupatiwa
chanjo ili kuepusha magonjwa. Mkuu wa ofisi ya WHO kanda ya Amerika,
Pier Paolo Balladeli amesema wanatumia ili kuhakikisha kila mtoto wa
kike anapata chanjo hiyo hususan maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo
ambako kiwango cha ugonjwa wa kansa ya kizazi ni cha juu. Argentina
ilijumuisha chanjo ya HPV katika mpango wa kitafai mwaka 2011 ambapo
watoto wa kike huchanjwa mara tatu na katika miaka miwili ya mwazoni
dozi ya kwanza imeshafikia asiilmia 80, dozi ya pili asilimia 60 na dozi
ya tatu asilimia 50. Kirusi aina ya HPV husababisha zaidi ya wagonjwa
wapya Elfu Tatu kila mwaka wa kansa ya kizazi nchini Argentina na kati
yao Elfu Moja Mia Nane hufariki dunia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni