Jumapili, 28 Julai 2013

Matukio ya Misri yanaonesha kina cha mwamko wa Kiislamu'


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, matukio ya nchini Misri yanaonesha kina cha mwamko wa Kiislamu katika nchi hiyo.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo jioni wakati alipoonana na wanachuo na wawakilishi wa asasi za kielimu, kiutamaduni, kisiasa n.k, za Vyuo Vikuu vyote vya Iran na kusisitiza kuwa, matukio yanayoendelea kushuhudiwa hivi sasa Misri yanaonesha kina na kilindi kirefu cha mwamko wa Kiislamu nchini humo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pia kuwa, mwamko wa Kiislamu haukuongozwa vizuri nchini Misri na kusisitiza kuwa, yanayotokea nchini Misri hivi sasa yanahuzunisha na kuumiza sana na hayo yote ni kutokana na kufanyika makosa katika kuongoza mwamko huo wa Kiislamu.
Pia amesema kutekeleza wajibu hakukinzani hata kidogo na wajibu wa kuangalia matokeo ya baadaye na inabidi kufuata njia sahihi kwa ajili ya kufikia kwenye matunda mazuri.
Habari zaidi kuhusu mkutano huo tutakuleteeni katika matangazo yetu yajayo, Inshaallah...

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni