Shirika moja la kutetea haki za binadamu nchini Italia limesema
kwenye ripoti yake kwamba, ubaguzi wa rangi barani Ulaya bado ni tatizo
sugu. Shirika hilo linalojiita I CARE limesema tukio la hivi karibuni la
kutupiwa ndizi waziri wa kwanza mweusi nchini humo limedhihirisha kuwa,
ubaguzi wa rangi Italia na barani Ulaya kwa ujumla bado ni tatizo kubwa
na lilanopaswa kukabiliwa vikali. Bi. Cecile Kyenge alitupiwa ndizi
wakati akihutubia siku ya Ijumaa katika mji wa Cervia mkoani Ravenna,
tukio linalonasibishwa na nyani au sokwe-mtu. Hii si mara ya kwanza kwa
waziri huyo kukumbana na hujuma hiyo ya ubaguzi wa rangi. Miezi kadhaa
iliyopita, Waziri Kyenge alizomewa na kundi la vijana mashariki mwa nchi
hiyo na baadhi yao pia kumtupia ndizi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni