Rais Francois Hollande wa
Ufaransa amesema, kuna uwezekano mkubwa kuwa mwili uliopatikana hivi
karibuni kaskazini mwa Mali ni wa raia wa Ufaransa aliyetekwa nyara
nchini humo mwaka 2011.
Rais Hollande amesema, kuna uwezekano mkubwa kuwa mwili huo uliopatikana siku 10 zilizopita ni wa Philippe Verdon, raia wa Ufaransa, na jitihada zote zinafanyika ili kujua chanzo cha kifo hicho.
Verdon, akiwa na raia mwingine wa Ufaransa, walikuwa kwenye safari ya kibiashara walipotekwa nyara usiku wa Novemba 21 mwaka 2011 kutoka kwenye hoteli waliyofikia.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni