Jumapili, 28 Julai 2013

Syria yaitaka UN kuwachukulia hatua magaidi


Syria imeutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kali dhidi ya jinai zilizofanywa na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za kigeni nchini humo, kufuatia kuuliwa kwa umati na magaidi hao, watu wasiopungua 123 huko katika mji wa Halab wa kaskazini mwa Syria. Shirika la habari la Syria (SANA) limeripoti kuwa, magaidi wenye silaha walioko nchini humo wameuwa watu wasiopungua 123 wengi wao wakiwa ni raia katika shambulizi walilolifanya huko Khan Assal, magharibi mwa mji wa Halab.  Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imemuandikia barua tofauti Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuutaka umoja huo uzizuie nchi zinazowaunga mkono magaidi hao baadhi yake zikiwa zinapakana na Syria, ili magaidi hao wasiendelee kufanya mauaji ya umati dhidi ya raia nchini humo. Barua hizo kwa Ban Ki Moon zimeeleza kuwa kundi hilo la magaidi la huko Syria linalojiita kwa jina la Brigedi ya Ansar al Khalifa, limekiri kuhusika na mauaji hayo ya Khan al Assal. Habari zinasema kuwa baada ya kuwauwa raia hao wa Syria, magaidi hao walikata miili ya wahanga na kuitupa katika shimo kubwa nje ya mji huo na pia kuichoma moto baadhi ya miili ya watu waliowauwa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria pia imezikosoa vikali baadhi ya nchi kwa misimamo yao ya undumakuwili kuhusiana na mapambano dhidi ya ugaidi.  Barua hizo tafauti za Syria kwa Umoja wa Mataifa pia zimeitaka taasisi hiyo kubwa ya kimataifa kuchukua hatua za kweli za kupambana na ugaidi huko Syria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni