Televisheni ya al Alam imeripoti kuwa, wanajeshi wa Syria
wamefanikiwa kuteka ngome za mwisho za makundi ya waasi katika eneo la
al Khalidiyyah mjini Homs na kusema kuwa mapigano yanaendelea katika
viunga vya mji huo kati ya wanajeshi na waasi.
Televisheni hiyo imeongeza kuwa, jeshi la Syria limefanikiwa kuukomboa msikiti wa Khalid bin Walid katika eneo la al Khalidiyyah huko Homs na kunukuu habari zisizothibitishwa kuwa sehemu hiyo ilikuwa ndiyo ngome ya mwisho ya waasi katika eneo hilo.
Mwandishi wa al Alam aidha amesema kuwa, mapigano makali yameendelea kwa wiki kadhaa katika eneo hilo na kuongeza kuwa, kufanikiwa jeshi la Syria kudhibiti eneo hilo ni sawa na kuwasafisha waasi katika mji wa Homs hasa Homs ya Kale.
Vile vile mwandishi wa al Alam amesema kuwa kundi moja la magaidi lilijaribu kuingia kwenye kituo cha umeme kwenye eneo la al Abasiyyin katika viunga vya Damascus lakini jeshi limelidhibiti kundi hilo kama ambavyo mapigano makali yanaendelea katika maeneo ya Qabun, Juwabir na Barzi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni