Tanzania imetangaza kuwa itauomba Umoja wa Mataifa ukipe mamlaka
makubwa zaidi kikosi cha kimataifa cha kulinda amani huko Darfur
(UNAMID) baada ya mauaji ya askari wa nchi hiyo wanauhudumu katika
kikosi hicho Jumamosi iliyopita.
Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Kapambala Mgawe amesema kuwa Dar es Salaam inafanya mazungumzo na Umoja wa Mataifa kuhusu uwezekano wa kikosi cha UNAMID kupewa mamlaka makubwa zaidi ya kuweza kujilinda dhidi ya makundi yanayobeba silaha huko Darfur, magharibi mwa Sudan.
Wakati huo huo kamanda wa kikosi cha UNAMID Mohammed Bin Shampas amesema watu waliofanya shambulizi la Jumamosi iliyopita dhidi ya askari wa kikosi hicho huko Darfur walikuwa wamejizatiti kwa silaha na ametoa wito wa kutazamwa upya uwezo na zana za kikosi hicho.
Askari saba wa Tanzania katika kikosi cha UNAMID waliuawa Jumamosi iliyopita na wengine 17 kujeruhiwa katika shambulizi la kushtukiza lililofanya na watu waliokuwa na silaha dhidi ya kikosi hicho.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni