Jumamosi, 30 Novemba 2013

Rice agundulika kuwa na saratani

Kocha msaidizi wa zamani wa Asenal, Pat Rice
Mchezaji wa zamani wa timu ya Ireland kaskazini na mlinzi wa zamani wa Arsenal Pat Rice amefikishwa hospitalini baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa wa Saratani.
Rice mwenye umri wa miaka 64 aliichezea mara 528 timu ya washika Bunduki wa London pia aliwahi kuwa Kocha msaidizi akimsaidia Arsene Wenger kwa kipindi cha miaka 16 kabla ya kustaafu mwaka 2012.
Taarifa ya klabu ya Arsenal imethibitisha kuwa Pat yu hospitali akipata matibabu na kumtumia salamu za pole na kumtakia heri apone haraka.
Rice aliichezea Gunners kwa kipindi cha zaidi ya misimu 14 baada ya kujiunga na timu ya vijana, ambapo timu yake ilichukua ubingwa wa Kombe la Ligi na FA mara mbili ,mwaka 1971, pia alikuwa nahodha wa Timu hiyo ambayo ilipata mafanikio makubwa kwenye michuano ya FA mwaka 1979.
Wenger amesifu jitihada na kazi ya Rice ambaye alikua akifanya nae kazi mpaka alipostaafu mwaka 2012.

Ndege yopotea Msumbiji yapatikana


Ndege hiyo ilitakiwa kutua kwenye uwanja wa Luanda.
Ndege iliyopotea tangu jana baada ya kuruka kwenye anga ya Msumbuji kuelekea Angola ikiwa na watu 34 imepatikana katika mbuga za wanyama Kaskazini Magharibi mwa Namibia.
Msemaji wa Polisi nchini Namibia amesema ndege hiyo iliteketea yote huku kukiwa hakuna aliyenusurika.

mabaki ya ndege hiyo iliyoteketea kabisa yamepatika kwenye mbuga ya wanyama Bwabwata karibu na mpaka wa Angola na Botswana.Ndege hiyo namba TM470 iliondoka Maputo nchini msumbiji tangu siku ya ijumaa na ilikuwa ikielekea Luanda nchini Angola.
"Ndege imeteketea yote yamebaki majivu tu hakuna hata mtu mmoja aliyenusurika," Naibu Kamishna wa Polisi nchini Namibia Willy Bampton amenukuliwa na shirika la habari la Reuters.
Inaelezwa kuwa masiliano ya mwisho na ndege hiyo yalikuwa ni wakati ndege hiiyo ilipofika kaskazini mwa Namibia.
Kwa mujibu wa shirika la ndege la Msumbiji abiria walipanda ndege hiyo ni raia 10 wa Msumbiji, Angola 9, Wareno 5, Mfaransa 1 , Mbrazili 1 na Mchina 1.
Jopo la watu waliokuwa akifanya kazi ya kuitafuta ndege hiyo walishindwa kuingia kwenye mbuga hiyo hapo jana baada ya mvua kubwa kunyesha kufanya barabara kushindwa kupitika.
Abiria 28 na wafanyakazi sita walikuwa kwenye ndege hiyo wakitoka Maputo kuelekea Luanda.

Mahakama Misri yakubali rufaa ya wasichana 21

Mahakama Misri yakubali rufaa ya wasichana 21
Majaji nchini Misri wamekubali rufaa ya wasichana 21 waliohukumiwa jela hivi karibuni nchini humo. Majaji hao wametangaza kuwa, mahakama ya nchi hiyo itasikiliza upya kesi ya wasichana hao mwanzoni mwa mwezi huu mkoani Alexandria. Siku ya Jumatano iliyopita mahakama moja nchini Misri iliwahukumu kifungo cha miaka 11 jela wasichana 14 wanaotajwa kuwa wafuasi wa Harakati ya Ikhwanul Muslimiin  kwa tuhuma za kushiriki katika maandamano dhidi ya serikali na kupambana na wafuasi wanaoiunga mkono serikali ya nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo wasichana wengine 18 pia walihukumiwa kifungo jela kwa tuhuma hizo hizo na kwamba wote kwa pamoja watafikishwa katika mahakama hiyo ya rufaa tarehe 7 ya mwezi huu. Tayari mashirika mbalimbali ya Kimataifa likiwemo Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International, yamelaani hatua ya kuwatia mbaroni wasichana kwa kushiriki katika maandamano dhidi ya serikali nchini humo na kuitaja hatua hiyo kuwa ni ukandamizaji dhidi ya wapinzani.

Wafungwa 40 wakimbia jela huko nchini Libya

Wafungwa 40 wakimbia jela huko nchini Libya
Duru za usalama nchini Libya zinaripoti kuwa, kwa akali watu 40 wametoroka katika moja ya jela za kusini mwa nchi hiyo. duru za usalama mjini Tripoli zimetangaza kuwa, tukio hilo lilitokea kufuatia shambulio la watu wenye silaha lililotekelezwa dhidi ya jela kuu ya mkoa wa Sabha kusini mwa Libya na kupelekea wafungwa 40 kutoroka. Mkuu wa jela hiyo Shaban Nasri amesema kuwa, baada ya watu wenye silaha kuvamia jela hiyo walifyatua risasi kwa wingi na kuingia katika seli za wafungwa. Ameongeza kuwa, watu hao walikuwa wanalengo la kumtorosha mmoja wa wafungwa aliyekuwa anashikiliwa katika jela hiyo ambapo baada ya kumkosa walianza kuwatishia wafungwa wengine kwa silaha ili wataje mahala alipo mtu wao, suala lililopelekea wafungwa wengine 40 kutoroka jela. Kufuatia tukio hilo, mkuu wa jela hiyo ameitaka Wizara ya Sheria nchini Libya kutoa msaada wa kimada na vikosi vya ulinzi kwa lengo la kuimarisha usalama na ulinzi katika jela kuu ya Sabha nchini humo.

Idadi ya watoto wanaokufa kwa ukimwi yaongezeka

Idadi ya watoto walio na umri kati ya miaka 10 na 19 wanaokufa kutokana na ukimwi duniani imeongezeka kufikia asilimia 50 kati ya mwaka 2005 na 2012.
Nyongeza ya ufadhili yahitajika kusaidia tatizo hilo-UNICEF.
Nyongeza ya ufadhili yahitajika kusaidia tatizo hilo-UNICEF.
Ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto-UNICEF imesema hali hiyo sasa ni ya kutisha na mpango wa haraka unahitajika kukabiliana na hilo, sambamba na kuongeza misaada kutatua tatizo hilo.
Ripoti hiyo imesema kuwa idadi ya watoto 71,000 walio na umri kati ya miaka 10 na 19 walifariki kutokana na ukimwi mwaka 2005, ambapo idadi hiyo ya vifo imeongezeka kufikia watoto 110,000 mwaka 2012, hali iliyoelezwa kuwa ni kutokana na kukosekana kwa vifaa vya upimaji na ushauri nasaha miongoni mwa vijana.
Kati ya vijana hao, ripoti hiyo imesema kuwa karibu asilimia 90 wanatoka katika nchi 22 duniani kote, lakini wengi kutoka katika Jangwa la Sahara.
Dola bilioni 5.5 zahitajika
Kutokana na matokeo ya utafiti huo, shirika hilo la UNICEF limesema kunahitajika nyongeza ya ufadhili wa dola bilioni 5.5 za Marekani ifikapao mwaka 2014, kwa ajili ya kusaidia kuwakinga watoto milioni 2 wasiambukizwe virusi vya Ukimwi katika miaka ijayo.
Wastani wa watoto milioni 2.1 walikadiriwa kuwa wanaishi na virusi vya Ukimwi duniani kote mwaka 2012.
Mkurugenzi wa shirika hilo, Anthony Lake anasema kwa sasa kunahitajika mpango wa haraka kuwafikia watoto ambao wapo hatarini zaidi kuambukizwa na kuwa mpango thabiti utakaoingilia kati hali hiyo utasiaidia katika kuleta matokeo mapya na kuibua maambukizi mapya ifikapo mwaka 2020.
Maambukizi toka kwa mama kwenda mtoto yapungua
Mpango wa kuzuia kunyonyesha umesaidia kupunguza maambukizi.Mpango wa kuzuia kunyonyesha umesaidia kupunguza maambukizi.
Kwa upande wa watoto wachanga, ripoti hiyo imeleta matokeo chanya, ambapo idadi ya vifo vya watoto wachanga wanaofariki kutokana na kuambukizwa virusi vya HIV kutoka kwa mama zao, imepungua kutoka vifo 540,000 mwaka 2005, kufikia vifo 260,000 mwaka 2012, kutokana na mpango wa kinga kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wa kuwakinga watoto wasiambukizwe virusi wanapozaliwa na wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi, na ule wa kuwazuia kunyonya.
Kwa hatua hiyo, mkurugenzi huyo wa UNICEF amepongeza juhudi zinazofanywa kuwaokoa watoto wanaozaliwa na kusema kuwa dunia sasa inashuhudia mafanikio ya kufikia taifa litakalokuwa huru dhidi ya maradhi ya ukimwi na watoto wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kunufaika na mafanikio hayo, na kuwa wa mwisho kunapotokea mapungufu.
Katika hatua nyingine, shirika la Afya duniani-WHO-limesema kuongezeka kwa idadi ya vijana wanaofariki kwa ukimwi ni kwa sababu ya kukosekana kwa huduma bora za afya miongoni mwa vijana, hasa kwa sababu hakuna huduma zinazowalenga vijana moja kwa moja.
Vijana wanahitaji kufuatiliwa kwa karibu
Watoto kati ya miaka 10 na 19 wapo hatarini zaidi kuambukizwa.
Watoto kati ya miaka 10 na 19 wapo hatarini zaidi kuambukizwa.
Mkurugenzi wa kitengo cha afya kinachoshughulikia maradhi hayo katika shirika hilo, Gottfried Hirnschall, amesema vijana wanahitaji huduma maalum za afya na ufuatiliaji wa karibu wa mahitaji yao kiafya.
Anasema nchi zilizopo katika ukanda wa Jangwa la Sahara zinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi, lakini ni asilimia 10 tu ya vijana wa kiume na asilimia 15 ya wasichana wanaofahamu juu ya hali zao kiafya ikiwa wameambukizwa virusi vya HIV au hawajaambukizwa, na kutoa ushauri mbali mbali, ikiwemo vijana hao kupimwa bila idhini ya wazazi wao, matumizi ya kondom na dawa za kuongeza muda wa kuishi.

Brazil yasisitiza itakuwa tayari kwa Kombe la Dunia

Mhandisi wa masuala ya usalama katika uwanja wa Sao Paolo ambako kreni kubwa iliporomoka inadaiwa alimwonya msimamizi wake kuhusu uwezekano wa kuwepo matatizo katika operesheni hiyo, na kisha ilani yake ikapuuzwa.
Watu wawili walipoteza maisha yao kutokana na ajali hiyo. Tukio hilo limezusha wasiwasi kuhusiana na uwezo wa Brazil kuandaa dimba hilo la mwaka ujao, pamoja na michezo ya Olimpiki mwaka wa 2016, ijapokuwa maafisa wanasisitiza kuwa nchi hiyo itakuwa tayari kwa matamasha hayo mawili.
Uwanja wa Sao Paolo Arena Corinthians ulitarajiwa kukamilishwa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa Desemba, na wafanyakazi wamedokeza kuwa kasi hiyo ilikuwa suala la kipau mbele katika ujenzi wa uwanaj huo, huku wengi wakifanya kazi kwa zamu za saa 12 na kunyimwa mapumziko.
Shirikisho la Soka duniani FIFA limesema linasubiri kufahamiswha kuhusu kiwango cha uharibifu kutokana na ajali hiyo ya Jumatano wiki hii. Maafisa wa FIFA pamoja na viongozi wengine wa kabumbu ulimwenguni wanatarajiwa kuwasili nchini Brazil wiki ijayo kwa ajili ya droo inayosubiriwa kwa hamu na ghamu ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia mjini Costa do Sauipe.
Viongozi wa FIFA wanasisitiza kuwa hakuna mpango mabadala kwa dimba hilo la mwaka ujao, na hasa kwa sababu karibu tikiti milioni moja za mechi hizo tayari zimeuzwa.

Timu ya soka Ujerumani kupewa zawadi nono

Wachezaji wa timu ya taifa ya kabumbu Ujerumani wameahidiwa marupurupu kama wataweza kufika katika robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Brazil. Hiyo ni kuwapa motisha ya kulileta kombe la dunia nyumbani
Shirikisho la soka la Ujerumani DFB limeahidi kutoa kiasi cha euro laki tatu (300,000) kwa kila mchezaji kama kikosi hicho kitashinda kombe la dunia.
Wachezaji pamoja na DFB walikubaliana jana Ijumaa kuhusu kile walichosema ni mfumo wa marupurupu ya mafanikio, sawa na yale waliyopata katika dimba la mwaka jana la Kombe la Mataifa ya Ulaya ambako walifika katika robo fainali.
Kila mchezaji atatia kibindoni euro 50,000 kama Ujerumani itafika robo fainali, laki moja katika nusu fainali na elfu mia moja hasmini kama watashindwa katika fainali. Mabingwa mara tatu wa Kombe la Dunia Ujerumani hawajalinyanyua kombe hillo tangu dimba la Euro 96. ukipewa ahadi kama hiyo huwa kunakuwa an msemo kuwa “heri punda afe lakini mzigo ufike”
Na wakati Ujerumani ikiahidi kuwapa marupurupu wachezaji wake, huko Barani Afrika, serikali ya Nigeria imeingilia kati pia kuyalipa madeni ya mshahara anaodai kocha wa timu ya taifa Stephen Keshi. Waziri wa michezo nchini Nigeria Bolaji Abdullahi amesema amepokea idhini kutoka kwa Rais Goodluck Jonathan kuyatatua masuala ya mishahara ya Keshi na wasaidizi wake, ambayo inafikia kiasi cha euro 357,000. Keshi, hajalipwa kwa karibu miezi mitano, hata baada ya kuisaidia timu ya taifa kunyakua kombe la Mataifa ya Afrika na kujikatia tikiti ya kucheza nchini Brazi

Maandamano kuendelea Ukraine

Upinzani nchini Ukraine unamatumaini kuwa waandamanaji hadi alfukumi watajitokeza leo(01.12.2013)Jumapili na kutoa msukumo mpya kudai rais Viktor Yanukovich ajiuzulu kutokana na mzozo wa uhusiano na Umoja wa Ulaya.
General view of Independence Square during a demonstration in support of EU integration, in Kiev November 29, 2013. Ukrainian President Viktor Yanukovich's decision to walk away from a deal that would have aligned his former Soviet republic more closely with the European Union sparked both anger and applause on the streets of Kiev on Friday. A sea of blue and gold, the colours of both the EU and Ukrainian flags, swept through the capital as people joined rival protests - one to celebrate closer ties with Russia, another to lament what they saw as a lost chance. REUTERS/Vasily Fedosenko (UKRAINE - Tags: POLITICS CIVIL UNREST CITYSCAPE)
Maandamano mjini Kiev
Vyama vikuu vitatu vya upinzani vimesema vinaanzisha , "kikosi cha taifa cha upinzani" baada ya polisi wa kuziwia ghasia kuwatawanya waandamanji kwa kutumia nguvu na kuwajeruhi watu kadha jana Jumamosi.
Mkutano huo wa waungaji mkono upinzani ulivunjwa na polisi waliotumia virungu ambao waliwashambulia kiasi ya waandamanaji 1,000 katika uwanja wa uhuru katika mji mkuu Kiev mapema jana Jumamosi asubuhi(30.11.2013).
 People supporting EU integration hold a rally in front of the Mikhailovsky Zlatoverkhy Cathedral (St. Michael's Golden-Domed Cathedral) in Kiev November 30, 2013. Ukraine's political opposition on Saturday said it would call a country-wide general strike to force the resignation of President Viktor Yanukovich's government after police used batons and stun grenades to break up pro-Europe protests. REUTERS/Vasily Fedosenko (UKRAINE - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)Maandamano mjini Kiev
Kiasi ya watu 10,000 walikusanyika katikati ya mji wa Kiev usiku wa Ijumaa na kusema Yanukovich ajiuzulu baada ya rais huyo kukataa kutia saini makubaliano ya kisiasa na kibiashara pamoja na Umoja wa Ulaya.


Maandamano zaidi
Upinzani umetoa wito wa kufanyika maandamano mapya leo katikati ya mji wa Kiev baada ya polisi kuzingira uwanja huo wa uhuru kwa kuweka uzio wa chuma.
"Tunaweza na tunapaswa kuwaondoa viongozi hawa," bingwa wa dunia wa ngumi Vitali Klitschko , kiongozi wa chama cha UDAR amewaambia waungaji mkono upinzani wapatao 10,000 siku ya jumamosi, na kutangaza maandamano mapya.
Ukrainian heavyweight boxing superstar Vitali Klitschko gives a thumbs up as he and his wife Natalya (R) leave a polling station after casting their ballots, in Kiev on October 28, 2012, during national parliamentary elections. Ukraine voted today in legislative polls seen as a test of democracy under President Viktor Yanukovych with jailed opposition leader Yulia Tymoshenko forced to watch from the sidelines. AFP PHOTO / ALEXANDER NEMENOV (Photo credit should read ALEXANDER NEMENOV/AFP/Getty Images) Vitali Klitschko kiongozi wa chama cha UDAR
"Tunapaswa kujitokeza na kuonesha kuwa hatutawaruhusu kutudhalilisha, tutasimama na kudai haki zetu," ameuambia mkusanyiko huo karibu wiki moja baada ya maandamano makubwa ya umma kuzuka nchini Ukraine kufuatia uamuzi wa maafisa kuachana na mpango wa kutia saini makubaliano na Umoja wa ulaya ambayo yangeiweka jamhuri hiyo ya zamani ya Umoja wa Kisovieti katika njia kuelekea kujiunga na Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya umeishutumu Urusi kwa kuipa mbinyo Ukraine, nchi ambayo inategemea kwa kiasi kikubwa gesi kutoka Urusi, na kujitoa kutoka katika makubaliano hayo.
Matumizi ya nguvu na vitisho
Jana Jumamosi , Lithuania ambayo inashikilia uongozi wa Umoja wa Ulaya kwa sasa imesema matumizi ya nguvu "hayavumiliki" na mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja huo Catherine Ashton pamoja na kamishna wa upanuzi wa Umoja huo Stefan Fuele wametoa wito wa kufanyika uchunguzi.
European Union High Representative for Foreign and Security Policy Catherine Ashton speaks to journalists prior to a meeting of Ministers for Foreign Affairs in the Palace of the Grand Dukes of Lithuania in Vilnius on September 6, 2013. AFP PHOTO / TOMAS LUKSYS (Photo credit should read TOMAS LUKSYS/AFP/Getty Images)Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa EU, Catherine Ashton
"Matumizi ya nguvu na vitisho havina nafasi katika Ukraine ya leo," ameongeza msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Marekani, Jen Psaki
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa maafisa nchini Ukraine kutimiza wajibu wao wa kulinda haki za binadamu.
Jana Jumamosi, Yanukovich alisema katika taarifa kuwa, "amefadhaishwa mno" na matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji na ameapa kuwa waliohusika wataadhibiwa.

Ijumaa, 29 Novemba 2013

Hii ndiyo kazi ya CC-CHADEMA kwa wale wenye kutoa matamko bila kuijua katiba .

Nimewiwa kuongezea hapa na huu mchango wa kamanda Lissu.



Ibara ya 5.4.3 inasema mwanachama wa CHADEMA anaweza kuachishwa au

kufukuzwa uanachama kwa kuwa na mwenendo usioendana na itikadi,

falsafa, madhumuni na maadili ya chama. Ibara ya 5.4.4 inaeleza kwamba

Kamati Kuu inaweza kumwachisha au kumfukuza mwanachama yeyote kwa

utaratibu uliowekwa na Kanuni za Chama. Kanuni za Chama ni pamoja na

Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama, Kanuni za Kusimamia Shughuli,

Mwenendo na Maadili ya Wabunge wa CHADEMA na Mwongozo wa Kutangaza

Kusudio la Kuwania Uongozi wa Chama, Mabaraza na Serikali.



Utaratibu wa hatua za kinidhamu uko kwenye kanuni ya 6.5.2 ikisomwa

pamoja na kanuni ya 6.5.6 na 6.5.7 ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za

Chama. Kwa kifupi, mtuhumiwa anatakiwa kupatiwa mashtaka ya maandishi

na kuambiwa ajitetee kwa maandishi sio pungufu ya wiki mbili na baada

ya hapo ana haki ya kujitetea mbele ya kikao husika cha nidhamu. Hata

hivyo, Kamati Kuu ya chama inaweza - kwa mujibu wa kanuni ya 6.5.2(d)

- kuchukua hatua stahiki za kinidhamu bila kujadili matakwa ya kanuni

zilizotajwa mwanzoni, endapo itaona kuna dharura na maslahi ya chama

yanaweza kuathirika kama hatua hizo hazijachukuliwa.



Nawaombeni msome kanuni ya 10 ya Kanuni za Uendeshaji inayohusu

maadili ya viongozi na wanachama; kanuni za 2(b), 3(b) na (f) za

Kanuni za Mwenendo na Maadili ya Wabunge; na kanuni za 2(d), (e) na

(g) za Mwongozo wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Uongozi wa Chama.

Mkakati wa Mabadiliko 2013 unapaswa kuangaliwa kwa macho ya vifungu

vyote hivi vya Katiba na Kanuni za Chama ili kuweza kuelewa the

thinking behind uamuzi wa Kamati Kuu. Kama masharti yote yaliyoko

kwenye vifungu hivi vya sheria za Chama hayakustahili kuheshimiwa basi

Kamati Kuu itakuwa imekosea sana katika maamuzi yake. Kama masharti

haya yalistahili kuheshimiwa then kosa la Kamati Kuu ni lipi hasa?



Alhamisi, 28 Novemba 2013

Mzozo wanukia kati ya China na Marekani kuhusu ulinzi wa anga

Ndege mbili za kijeshi za Marekani zimepita katika anga za China katika eneo linalozozaniwa kati ya China na Japan la visiwani bila ya kuiarifu na kupuuza agizo la China kutaka kuarifiwa mapema kutumika kwa anga zake.
Wataalamu wa masuala ya kidiplomasia wanaona ukiukaji huo wa masharti ya China kuhusu kutumika kwa anga zake kutoka kwa Japan na washirika wake Marekani kutachochea hata zaidi mzozo ulioko wa kusimamia eneo la visiwa kati ya Beijing na Tokyo na kuifanya China kuchukua hata hatua zaidi kusisitiza ubabe wake.
Mwishoni mwa wiki iliyopita China ilichapisha kanuni mpya za kuanzisha eneo maalum la ulinzi wa anga katika eneo lenye mzozo wa maji katika bahari ya China Mashariki na kutangaza kuwa ndege zinazopita katika eneo hilo la bahari, sharti zitii maagizo yake.
Ndege zitakazokuwa zikiingia katika eneo hilo zitatakiwa kutoa taarifa za awali kabla ya kupita katika eneo hilo na kudumisha mawasiliano kwa kujibu maswali yatakayohitajika kutoka kwa waongozaji ndege.
Chanzo cha mzozo ni visiwa
Eneo hilo la ulinzi linahusisha visiwa vya Senkaku na Diaoyu ambavyo vimekuwa chachu ya kuongezeka kwa mzozo baina ya mataifa hayo mawili. China imesema itadhibiti anga na visiwa vyake mashariki mwa nchi hiyo na kuonya kuwa itachukua hatua za dharura za kujilinda dhidi ya ndege yoyote itakayofeli kuzingatia sheria zake.
Chombo cha majini cha Kijeshi cha China kikishika doria Chombo cha majini cha Kijeshi cha China kikishika doria
Profesa Sun Zhe wa chuo kikuu cha Tsinghua mjini Beijing amesema iwapo Marekani itaendesha ndege zake mara mbili tatu kama ilivyofanya wakati huu, basi itailazimu China kuchukua hatua ambazo hazitakuwa za maneno matupu tu.
Wizara ya ulinzi ya China imesema ilifuatilia nyendo zote za ndege hizo za kijeshi za Marekani jana lakini msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani amesema ndege hizo hazikufuatiliwa wala hazikupokea mawasiliano yoyote kutoka China.
Shirika la ndege la Japan, ANA, limesema kufuatia ombi kutoka kwa serikali yake, limesitisha kutoa taarifa zozote za mipango ya safari za ndege zake kwa maafisa wa China na haijashuhudia matatizo yoyote wakati ikipita katika kanda hiyo na kuongeza hakuna kitisho kwa usalama wa abiria wake.
Japan yajiimarisha kukabiliana na vitisho
Hatua hiyo ya China pia inaonekana kutoa fursa kwa waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe, kupata mashiko ya hoja yake ya kupewa nguvu zaidi za kuboresha jeshi lake ili kukabiliana na vitisho vyovyote kutoka nje.
Rais wa Marekani Barrack Obama na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe Rais wa Marekani Barrack Obama na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe
Japan leo imeunda baraza la kitaifa la usalama ambalo limeidhinishwa na bunge linalompa waziri mkuu mamlaka zaidi kuhusu masuala ya kiusalama na sera za kigeni na ulinzi hatua inayoonekana kutokana na mzozo huu uliozuliwa upya na China.
Marekani ambayo ina mamia ya ndege za kijeshi katika kanda hiyo imesema haina nia ya kuzingatia kanuni mpya zilizowekwa na China huku Japan ikizitaja hatari na zisizokubalika. Taiwan na Korea Kusini ambazo pia ni washirika wa Marekani katika kanda hiyo pia zimetupilia mbali masharti hayo ya China.
Hata Australia imejiingiza katika mzozo huo kwa kumuita balozi wa China nchini humo kuelezea wasiwasi wao kuhusu maagizo hayo ya kudhibiti anga yake.

Wanachama wa ICC warekebisha baadhi ya sheria zake

Wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, wamerekebisha baadhi ya sheria za Mkataba wa mahakama hiyo hapo jana kutoa nafasi kwa washtakiwa kufuatilia kesi zao kupitia vidio.
Majaji katika mahakama ya ICC Majaji katika mahakama ya ICC
Marekebisho hayo pia yatakubali viongozi wanaoshikilia nyadhifa za juu kutohudhuria baadhi ya vikao katika mahakama hiyo. Hatua hii inasemekana kumlenga rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye kesi dhidi yake katika mahakama hiyo ya ICC inatarajiwa kuanza rasmi Februari mwaka ujao.
Mahakama hiyo iliyo na wanachama 122 ilifikia uamuzi huo katika mkutano wake wa kila mwaka, uliofanyika katika makao yake makuu, mjini The Hague, Uholanzi.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea mapigano katika ghasia za baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2007/2008 ambapo zaidi ya watu 1,200 waliuwawa. Hata hivyo Rais Kenyatta anaendelea kusisitiza kwamba hana hatia. Sasa inasubiriwa kuonekana athari itakayoletwa na uamu huo wa mataifa wanachama wa ICC.
Katika siku za nyuma, majaji wa mahakama ya ICC waliwahi kumuachia Naibu Rais William Ruto, anayeshitakiwa kwa kesi sawa na Rais Kenyatta, ya kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi, aendelee kuwepo nchini Kenya kwa baadhi ya kesi zake ili aweze kutimiza wajibu wake serikalini.
Marekani yaridhia mabadiliko
Mabadiliko yaliofanywa hapo jana yanaweza kuwa na maana kwa kwa washitakiwa waliojitolea kushirikiana na mahakama hiyo kama Uhuru na Ruto kuliko wale walioshikiliwa kwa nguvu na kuwekwa rumande.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power
Kwa upande wake Marekani ambaye sio mwanachama wa ICC imeyakaribisha mabadiliko hayo na kusema kwamba ICC inapambana na kesi ngumu kwa kuwa inajitayarisha kumshtaki rais ambaye yuko madarakani.
Samantha Power, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema uamuzi huo umewekwa katika hali ya kwamba unalinda haki ya washtakiwa na waathiriwa, huku ukitoa nafasi ya kesi hiyo kuendelea bila kupoteza wakati.
Rais Uhuru Kenyatta, makamu wake Wiiliam Ruto na mtangazaji wa Radio Moja nchini humo Joshua Arap Sang wote wanakabiliwa na mashtaka katika mahakama hiyo ya ICC.
Kenya yataka viongozi wanaoshtakiwa kupewa msamaha
Kenya imekuwa ikijihusisha na mipango ya kidiplomasia ya kusimamisha kwa muda kesi ya Uhuru na Ruto huku ikisema kuwa nchi hiyo na eneo la Afrika ya Mashariki kwa jumla linahitaji uongozi thabiti katika kupambana na wanamgambo wa al-Shabaab katika nchi jirani ya Somalia.
Kundi hilo la Al shabaab linalosemekana kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la al-Qaida.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Kenya Amina Mohammed Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Kenya Amina Mohammed
Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohammed, alisema nchi yake iko mbioni kujaribu kupata msamaha wa mahakama ya ICC kwa viongozi wake kutoshtakiwa wakiwa madarakani.
Thuluthi mbili ya wanachma 122 wa mahakama ya ICC wanapaswa kupigia kura uamuzi kama huo wa kubadilisha Mkataba wa Rome ulioiunda Mahakama hiyo na utaingia katika utekelezwaji mwaka mmoja baada ya sehemu kubwa ya nchi wanachama kuuridhia.
Hata hivyo katika hali nyengine iliojitokeza ni kwamba balozi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa Macharia Kamau amesema wanachokitaka wao sio kutumika kwa mfumo wa video katika kesi ila kuondoa kabisa mashtaka kwa viongozi walioko madarakani.

Jumatano, 27 Novemba 2013


Diamond awataja mademu zake wanne, lakini anampenda huyu


Penieli Mungilwa na Diamond 
  • Shoo ninayoweza kufanya kwa bei ya chini kabisa ni Sh 10 milioni za Kitanzania na hii labda nione anayeniomba nifanye shoo hiyo hayuko vizuri na pengine ni rafiki yangu na hawezi kuninyonya, si hivyo tu itategemea pia ni kampuni gani na ni watu wa aina gani ambao watanitaka nifanye nao kazi.


UKIFIKA katika mtaa anaoishi mwanamuziki Diamond maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam utaanza kuhisi kuwa kuna staa anayeishi maeneo hayo, macho ya wengi huanza kumtazama mtu anayeelekea katika geti la nyumba anayoishi msanii huyo.
Muda wote geti hilo limefungwa. Ili uweze kuingia ndani itakulazimu ubonyeze kengele itakayoashiria kuwa kuna mgeni nje anahitaji kuingia ndani. Hata hivyo hauwezi kupenya kirahisi ndani hadi uulizwe shida yako na kama hauna miadi na mtu yeyote anayeishi ndani ya nyumba hiyo haitakuwa rahisi kuingia.

 Diamond: Nilimpenda sana lakini aliniacha kabla ya kutoka. Mpenzi wangu wa kwanza alikuwa anaitwa Sarah Sadick, sijawahi kumuhonga na ndiye mwanamke niliyewahi kumpenda sana. Wakati huo Naseeb Abdul kabla sijawa Diamond nilikuwa nahaha kuhangaika ni vipi nitatoka kimuziki. Msichana huyu ndiye aliyenipa hasira za kufanya muziki kwa bidii zote baada ya kunitema na kuanza kuhangaika na wengine na aliniita majina mengi yasiyo mazuri, kisa sina fedha. Si kwamba nilimuacha bali yeye ndiye aliyeniacha kama zali baada ya wiki kadhaa nikatoka na wimbo Kamwambie, taratibu nikaanza kuwa staa naye akaanza kurudi ila nilishamuondoa moyoni mwangu.

 Diamond: Alinisumbua sana kutokana na ugumu wa maisha niliokua nao kwa kipindi cha nyuma hadi kufikia 2009. Nilimpenda sana huwezi amini nilikuwa silali usingizi kwa ajili yake. Nahisi ilitokana na mimi kukosa kazi ndiyo maana ilifikia hatua alinipotezea. Lakini baada ya kupata na kujulikana alinifuata lakini sikutaka tena hata baada ya kuniomba msamaha.

 Diamond: Sikumbuki kwa kweli wapo wengi mno, si unajua tena wapo walionitaka na kunilazimisha nifanye hivyo, lakini idadi kamili siwezi kukumbuka na kila siku nasumbuliwa na hawa wanawake.
 Diamond: Nimewahi kuwa na wapenzi wanne katika kipindi chote cha ustaa wangu na sikupenda kubadili ovyo ila wengi wao hawakuweza kutimiza haja ya moyo wangu.

 Diamond: Ndiyo ila wawili wanafahamika zaidi. Wa kwanza kabisa alikuwa anaitwa Sarah na wa pili alikuwa anaitwa Hawa yule msichana niliyeimba naye katika wimbo ‘Nitarejea’, huyu alizidiwa ujanja na Wema Sepetu ambaye naye alikuja kuondoka kwangu na baadaye nikawa na Penieli Mungilwa

 iamond: Mwanamke wangu wa kwanza Sarah Sadick huyu aliniingia sana moyoni sijajua ni kwanini. Lakini nahisi huenda kwa kuwa awali alinipenda kweli kwa kuwa wakati huo sikuwa na kitu. Hata hivyo nahisi ilitokana na mimi kutokuwa bize na wakati huo sikufikiria lolote zaidi ya yeye ilitokana na kutokuwa na kazi ya kufanya. Siku hizi sina mapenzi ya kivilee, nawaza zaidi pesa na ninaihangaikia na zaidi ni muziki wangu, hili ndilo la kwanza kabisa linalonifanya niwe bize mapenzi baadaye.

Diamond: Ndiyo, wengi sana tena kuna mmoja kati ya wanawake niliowahi kuwa nao alinitongoza yeye mwenyewe ndipo nikawa naye na nilikaa naye katika uhusiano kwa kipindi kirefu tu. Wanaweza kumfikiria mwanamke fulani lakini huwezi amini ukweli ninao mimi mwenyewe na katu hawawezi hata kumhisi.
 Ninatongozwa sana kwenye mitandao ya kijamii, facebook, whatsapp, Instagram na kwingineko na wapo wasichana ambao wanatafuta namba zangu za simu na kuanza kunisumbua.

Diamond: Kwanza ninahitaji aijue kazi yangu na ajue kwamba mimi ni mtu maarufu hivyo akubaliane na changamoto mbalimbali atakazokumbana nazo kwa kipindi atakachokuwa ndani ya ndoa, siyo siku mbili anafungasha virago. Pia ajue kwamba nitamsikiliza mama yangu kwanza kabla ya yeye hilo naliweka wazi, yeye ana nafasi yake katika maisha yangu lakini mama yangu nimempa kipaumbele, tatu awe tayari kuishi na mama yangu. Nne awe na akili na mwenye utambuzi na atakayeniongoza katika kazi zangu, sihitaji kuwa na mwanamke golikipa kila siku ategemee kutoka kwangu. Tano awe mzuri, nahitaji mke bwana…yule nitakayeweza kutoka naye out kwenye zulia jekundu, nikapita naye bila tatizo lolote awe mzuri.

SOURCE MWANASPORT GAZETI

Jumatatu, 25 Novemba 2013

Polisi wapambana na wavamizi Kenya

Polisi nchini Kenya wanaendesha operesheni dhidi ya wavamizi walioteka kijiji kimoja Kaskazini Magharibi mwa nchi.
Walisema kuwa wavamizi hao wamejihami kiasi cha haja na waliweza kukabiliana nao ingawa hali bado ni tete.
Kijiji hicho kiko katika eneo ambalo hukumbwa na makabiliano ya kila mara kati ya watu wa jamii ya Turkana na Pokot wakizozania mali asili.
Inaarifiwa washambuliaji waliwazuia watu 900 wengi wakiwa watoto na wanawake katika vijiji vinne, katika jimbo la Turkana Kusini kwa karibu wiki moja.
Polisi wa kupambana na ghasia na polisi wa kawaida wamekwenda katika eneo hilo wakiwa wamebeba chakula kufuatia ripoti kuwa mamia ya wanakijiji pamoja na kikosi cha polisi, hawana chakula na maji na hali imekuwa hivyo kwa karibia wiki moja.
Mmoja wa viongozi wa eneo hilo, alisema kuwa wavamizi hao waliwazuia watu wa jamii ya Turkana bada ya mzozo kuhusu umiliki wa ardhi inayokaliwa na jamii hiyo kudaiwa kuwa mali ya jamii ya Pokot.
Naibu kamishna wa jimbo hilo anasema kuwa mzozo huu huenda uliibuka baada ya kutolewa ramani mpya kuhusu mpaka kati ya eneo la Pokot Magharibi na jimbo la Turkana Kusini.
Polisi hata hivyo walikana ikiwa kuna watu waliotekwa nyara na washambuliaji hao katika kijiji cha Lorogon.
Polisi waliokwenda katika eneo hilo kudbihiti hali walisema walikutana na vijana karibu miambili kutoka jamii ya Pokot waliokuwa wamejihami na kuweka vizuizini barabarani.
Kulikuwa na makabiliano makali kati ya polisi na washambuliaji hao wikendi yoyote.
Duru zinasema kuwa mazungumzo kati ya jamii hizi mbili yalitarajiwa kuanza siku ya Jumapili lakini hakuna taarifa kuhusu ikiwa yalianza au la.
Wanasiasa katika jimbo hilo wanasema hali ya kibinadamu heunda ikawa mbaya zaidi hasa baada ya kijiji cha Lorogon kuzingirwa kwa siku nne sasa.

Jumamosi, 23 Novemba 2013

Zitto Kabwe



Mkutano na waandishi wa habari: Mhe Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo

Taarifa inatolewa kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe pamoja na Dk Kitila Mkumbo watakutana na wahariri na waandishi wa habari kesho siku ya Jumapili tarehe 24 Novemba 2013. Watatumia nafasi hii kutoa maoni na msimamo wao kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA ya hivi karibuni. 
Mkutano huu na waandishi wa habari utafanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kuanzia saa5.00 asubuhi.

Imetolewa na ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe, Dar es Salaam.
Jumamosi, 23 Novemba 2013. 
Dar es Salaam

Ijumaa, 22 Novemba 2013

Mjumbe wa AU asema huenda Kony anaumwa

Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda.(LRA)
Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda.(LRA)
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika amesema mbabe wa kivita  kutoka Uganda Joseph Kony  huenda  akawa mgonjwa sana na anatafuta hifadhi kwa wapiganaji wake wa kundi la Lord’s Resistance Army.

Fransisco Madeira mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika anayehusika na swala la kundi la waasi wa Uganda- LRA, alisema Jumatano  kwamba kiongozi wa Jamhuri ya Afrika Kati amewasiliana na Kony na anajaribu kufanya mashauriano naye ili kujisalimisha kwake.

Lakini Madeira anasema inawezekana Kony anaidanganya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ili inapofanya majadiliano, apate muda wa kufanya  mkakati  wa kuhamisha wapiganaji wake.

Mjumbe huyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu kuugua kwa Kony.


Sentensi tatu kuhusu Zitto Kabwe kuvuliwa nyadhifa zote Chadema.

ZKChama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemvua nyadhifa zote Naibu Katibu mkuu wake Zitto Kabwe ambae ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye makao makuu ya chama hicho, amesema Zitto na wenzake watatu wamebainika kukihujumu chama  kwa kuanzisha kitu kinaitwa Mkakati 2013 kinacholenga kukisambaratisha chama hicho ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu mkuu wake.
Nyadhifa alizovuliwa ni Unaibu katibu mkuu pamoja na Naibu kiongozi wa upinzani bungeni ambapo yeye, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba na mwingine mmoja Makao makuu wamepewa siku kumi na nne wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu ikiwemo kuvuliwa Uanachama.


SOURCE: MILLARD AYO.COM

Jumatano, 20 Novemba 2013


Rage ‘stop’, Kibadeni ‘out’


Ismail Aden RAGE
Sasa hii ni ukiukwaji wa katiba, hatuna imani naye na hata kama angekuwepo tungemweleza wazi kitendo chake hatukiafiki, tumemsimamisha mpaka Desemba mosi
Dar es Salaam. Wakati Kamati ya utendaji ya Simba ikimsimamisha Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage, imewafungashia virago makocha wake, Abdallah Kibadeni ‘King’ na msaidizi wake, Jamhuri Kiwehlo ‘Julio’ kuinoa timu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi.
Akizungumza Makao Makuu ya klabu hiyo jana, Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are ‘Kinesi’ alisema kikao cha Kamati ya Utendaji iliyokaa juzi usiku imefikia uamuzi wa kumsimamisha Mwenyekiti wao kwa kile walichoeleza kutokuwa na imani naye baada ya kushindwa kuitisha mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Rage, kusimamishwa ndani ya klabu hiyo, awali alisimamishwa Machi mwaka huu baada ya wanachama kufanya mapinduzi ya kumwondoa akiwa kwenye matibabu nchini India, hata hivyo aliporudi alisema hatambui mapinduzi hayo na kuitisha mkutano alioufanya kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi Oyestbay huku akiahidi kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa mabadiliko Agosti. Hata hivyo, aliahirisha kwa kile alichoeleza ni kupisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Hata hivyo, jana Kinesi alisema: “Mkutano mkuu wa mwaka ulikuwa ufanyike mwezi huu wa Novemba na ajenda kubwa ni mabadiliko ya katiba, lakini cha kushangaza Rage amewaambia wanachama hakuna mkutano mpaka mwakani na ameondoka yupo nje ya nchi.
“Sasa hii ni ukiukwaji wa katiba, hatuna imani naye na hata kama angekuwepo tungemweleza wazi kitendo chake hatukiafiki, tumemsimamisha mpaka Desemba mosi.
Kinesi alisema Desemba mosi ndiyo utafanyika mkutano mkuu wa wanachama na hatma ya Rage itajulikana kwenye mkutano huo iwapo wanachama wataridhia kumwondoa au wataamua adhabu yake ya kumsimamisha iendelee au arejeshwe kundini kumaliza muda wake ambao unafikia ukingoni Aprili mwakani.
Rage ambaye yuko Juba, Sudan Kusini na anayetarajiwa kurudi nchini Ijumaa, simu yake ilikuwa haipatikani na alitumiwa ujumbe juu ya maono yake kwa hatua hiyo, hakujibu.
Mbali na Rage, pia rungu hilo la Kamati ya utendaji limeangukia benchi ya ufundi la klabu hiyo baada ya kuwafungashia virago  ‘King’ na ‘Julio’ kutokana na mwenendo mbovu wa timu yao iliyomaliza mzunguko wa kwanza wa ligi ikiwa inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 24.
Kinesi alisema nafasi ya Kibadeni itachukuliwa na  aliyekuwa Kocha wa timu ya Gor Mahia, Zdravko Logarusic raia wa Crotia akisaidiwa na Seleman Matola.
Alisema kocha huyo atatua nchini Desemba mosi na timu itaanza rasmi mazoezi Desemba 2 kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza kwa njia ya simu baada ya uamuzi huo, Kibadeni alisema “Nashukuru kwa hatua hiyo, ni kazi nzito ya kuinoa Simba na kwa vile wamenifukuza timu iko juu wala sijali ingekuwa chini ningesikitika
.Alisema kwa sasa ataishughulikia familia yake na kuangalia afanye nini baadaye, lakini akasema ana mkataba wa miaka miwili Simba.
Julio alipotafutwa kwa njia ya simu alisema hawezi kuzungumza kwa njia hiyo atazungumza ana kwa ana.

RATING
Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM, Nape Nnauye PICHA|MAKTABA 
KWA UFUPI
Ni baada ya Nnauye kupendekeza kwa Msajili kukifuta kwa kukiuka katiba.Dar es Salaam.Siku moja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM, Nape Nnauye kumtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kukifuta Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kushindwa kusimamia katiba yake na kutofanya uchaguzi wa ndani kwa zaidi ya miaka 10, chama hicho kimesema hakijawahi kwenda kinyume na katiba yake na kinachozungumzwa na Nnauye ni uzushi wa kisiasa unastahili kupuuzwa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika alisema jana kuwa katika miaka 10 iliyopita chama chao kimefanya uchaguzi mara mbili kila baada ya miaka mitano kama katiba inavyoelekeza.
Chadema tumefanya uchaguzi mkuu wa ndani 2004 na 2009, mara baada ya kipindi cha miaka mitano kupita ya muda wa kawaida wa uongozi. Madai kwamba hatujafanya uchaguzi kipindi hicho hayana msingi,” alisema Mnyika.
“Msajili wa vyama vya siasa anapaswa kupuuza kauli hiyo ya Nape na CCM na kurejea Katiba ya Chadema ambayo ofisi yake inayo nakala yake.”Ni vyema msajili akaikemea CCM kwa kufanya siasa chafu za uongo na uzushi,” alisema.
Aliongeza: “Kauli ya Nape na CCM ni ishara ya chama hicho kutishwa na namna ambavyo Chadema kinajipanga kuanzia ngazi ya chini kujenga uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti mijini na vijijini kuanzia ngazi za chini kupitia Programu ya Chadema ni Msingi.”
Mnyika alisema Nape na CCM wanajaribu kupotosha umma unaounga mkono vuguvugu la mabadiliko (M4C) kupitia Operesheni za Kanda na kazi nyingine zinazoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Kamati Kuu ya Chadema itafanya mkutano wake wa kawaida kwa siku mbili jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 20 mpaka 21.
Ajenda za mkutano ni kupokea, kujadili na kufanya uamuzi mihutasari ya mikutano iliyopita na yatokanayo na mikutano hiyo, taarifa ya hali ya siasa na ripoti ya fedha.
Ajenda nyingine ni pamoja na taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba, taarifa ya utekelezaji wa Programu ya Chadema Msingi na shughuli za Kanda na taarifa ya utekelezaji wa Mpango Mkakati kuhusu maboresho.

Mashambulizi ya mabomu yatikisa mji mkuu wa Iraq, Baghdad

Mashambulizi ya mabomu yanayotekelezwa nchini Iraq
REUTERS/Wissm al-Okili

Na Flora Martin Mwano
Mashambulizi ya mabomu yaliyowalenga waumini wa Kishia nchini Iraq yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 30 na kujeruhi wengine zaidi ya 70. Kwa mujibu wa ripoti za idara ya usalama toka nchini humo milipuko nane imesikika katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu wa nchi hiyo, Baghdad.

Mlipuko mwingine umetokea jirani na eneo ambalo Washia walikusanyika kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kiongozi wao wa kiislamu, Imam Hussein.
Inahofiwa kuwa huenda idadi ya vifo itaongezeka zaidi kutokana na mashambulizi haya kufanyika siku ambayo ilitangazwa na serikali ya nchi hiyo kuwa ya mapumziko.
Hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulizi hilo, ingawa wanamgambo wa Kisunni wenye uhusiano na mtandao wa kigaidi duniani wa Al-Qaeda wananyooshewa kidole kutokana na kuwa na kawaida ya kufanya mashambulizi dhidi ya Washia.
Katika tukio jingine, Polisi nchini humo wameripoti kuwa mlinzi mkuu wa Rais wa nchi hiyo ameuawa katika mji wa Kaskazini wa Sulaimaniyah. Inaelezwa kuwa wavamizi walifika nyumbani kwa mlinzi huyo, Sarwat Rashid na kumpiga risasi mara tatu kichwani mbele ya mkewe.
Waziri Mkuu Nuri al-Maliki ametoa wito kwa serikali ya Washington kusaidia katika mfumo wa kijasusi na mfumo wa upatikanaji wa silaha mpya ili kukomesha mashambulizi hayo ambayo baadhi ya wanadiplomasia wanasema yanachochewa na mzozo wa nchi jirani ya Syria.
Hata hivyo wakosoaji wanasema serikali ya Iraq haijafanya jitihada za kutosha kutatua kiini cha mzozo huo baina ya waumini wa Kishia na Wasunni.
Bado hofu ya usalama ni kubwa hususani kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 Aprili mwaka ujao.

shambuliaji wa Westgate walivyopenya Kenya

Wanamgambo wanne wa kundi la Al Shabaab waliohusika na shambulizi la kigaidi dhidi ya jumba la Westgate nchini Kenya , waliingia nchini Kenya kupitia mpakani kutoka Somalia.

Mtaa huo una wahamiaji wengi wa Kisomali baadhi waliokimbia vita kutoka Somalia.Afisaa mmoja mkuu kutoka mojawapo ya nchi za Magharibi ameambia BBC kuwa wanamgambo hao waliingia nchini Kenya kupitia eneo ambalo hutumiwa na watu wengi kuingia Kenya na kisha kukita kambi katika mtaa wa Eastleigh, mjini Nairobi.
Washambuliaji wanasemekana waliishi Somalia kwa muda ambako walipata mafunzo yao.
Watu 67 waliuawa kwenye shambulizi la kigaidi lililofanywa na kundi la Al Shabaab dhidi ya jumba la maduka la Westgate katika mtaa wa Westlands mnamo mwezi Septemba.
Al Shabaab lilikiri kufanya shambulizi hilo kwa lengo la kulipiza kisasi dhidi ya serikali ya Kenya kwa kutuma majeshi yake nchini Somalia kupambana dhidi ya kundi hilo.
Hadi kufikia sasa raia wanne wa kigeni wamefikishwa mahakamani baada ya kuhusishwa na shambulizi hilo. Wanadaiwa na polisi kuwapa makao washambuliaji hao mjini Eastleigh.
Washukiwa hao, Mohammed Ahmed Abdi, Liban Abdullah, Adan Adan na Hussein Hassan wamekanusha madai ya kuwapa hifadhi magaidi na kuwasaidia kufanikisha mipango yao.
Afisaa huyo hata hivyo amesisitiza kuwa ni watu wanne pekee walioshambulia jengo hilo kama ambavyo serikali ya Kenya imekuwa ikisisitiza.
Wawili kati ya wale waliofanya shambulio hilo, wamejulikana kutokana na nyaraka za mahakani wakisemekana kuwa Hassan Dhuhulow, anayeaminika kuwa raia msomali mzaliwa wa Norway na Mohammed Abdinur Said.
Washambuliaji hao walikuwa na kile maafisa wa usalama wanasema ni msaada mkubwa ndani ya Kenya.
Lakini hakuna ushahidi kuonyesha kuwa mshukiwa mkuu wa ugaidi, Samantha Lewthwaite, mzaliwa wa Uingereza ambaye ni mjane wa mshambuluaji aliyeshambulia kituo cha treni mjini London Uingereza mwaka 2005, alihusika na shambjlizi hilo.
Taarifa hizi zinaweza kusaidia majasusi kujua uraia halisi wa washukiwa wa shambulizi hilo na uhusiano wao na kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Jumapili, 17 Novemba 2013



Libya yaombwa kukabidhi Saif al-Islam kwa ICC

Saif al-Islam,mwanawe kiongozi wa zamani  wa Libya Moammar Gadhafi, Julai 30, 2007.
Saif al-Islam,mwanawe kiongozi wa zamani wa Libya Moammar Gadhafi, Julai 30, 2007.

 
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa –ICC ametoa mwito kwa Libya kumsalimisha Saif al-Islam Ghadafi, mwanae  kiongozi wa zamani wa Libya aliyeuawa  Moammar Ghadafi, lakini mwakilishi wa Libya katika Umoja wa Mataifa amesema ombi hilo limekataliwa.

Mwendesha mashtaka huyo wa ICC, Fatou Bensouda anataka utawala wa Libya uikabidhi mahakama hiyo mwana wa kiume wa Ghadafi Saif al- Islam  kwa makosa mawili ya uhalifu dhdi ya binadamu; mauaji na mateso.

Bensouda alikuwa akizungumza na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Alhamis mjini New York akisistiza kuwa ikiwa hati ya kukamatwa kwa mtuhumiwa imetolewa sharti iheshimiwe na kwamba maswala ya kisiasa  hayana msingi katika sheria.

Lakini balozi wa Libya katika Umoja wa Mataifa Ibrahim Dabbashi aliliambia Baraza hilo la Usalama kwamba wananchi wa Libya wanataka kuona Saif al-Islam Ghadafi akishatkiwa nchini Libya.

Akizungumza kupitia mkalimani, balozi Dabbashi alisema hakuna serikali yoyote ile itakayokubali kesi hiyo kusikilizwa nje ya Libya kwa sababu itavuruga amani na uthabiti wa kijamii nchini Libya na kuleta hatari na vitisho zaidi kwa maisha ya wananchi.

ICC ilikubali kesi ya mtuhumiwa mwingine wa Libya ambaye zamani alikuwa mkuu wa idara ya kijasusi, Abdullah al-Senussi isikilizwe Libya na hivyo balozi  Dabbashi anasema  haoni kwani nini ICC isiiachie Libya kusikiliza kesi dhidi ya Saif.

Mandela sasa hawezi kuzungumza

Picha ya kale ya Nelson Mandela na Winnie kabla ya kuachana
Mke wa zamani wa Nelson Mandela, amesema rais huyo wa zamani hawezi kuzungumza, lakini anatumia uso kuwasiliana na watu.
Winnie Madikizela-Mandela alieleza kuwa Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 95, ni mgonjwa kweli lakini alikanusha tetesi kuwa mashini ndio inamsaidia kupumua.
Mwezi wa Septemba Bwana Mandela alirudi nyumbani baada ya kulazwa hospitali mjini Pretoria kwa karibu miezi mitatu akitibiwa ugonjwa wa mapafu.
Serikali ya Afrika Kusini imesema hali yake bado ni ya kutia wasi-wasi na wakati mwengine hubadilika.

Mapigano mapya yazuka Libya watu 40 wauawa

Mapigano mapya yamezuka mjini Tripoli Libya jana Jumamosi(16.11.2013) wakati idadi ya watu waliouawa katika mapigano wakati wa maandamano ya kupinga wanamgambo ikipanda na kufikia watu 43.
Protesters march during a demonstration calling on militiamen to leave, in Tripoli November 15, 2013. At least 10 people were wounded in Tripoli on Friday when militiamen opened fire on hundreds of protesters who had marched on their brigade headquarters to demand that they leave the Libyan capital, a Reuters witness said. Heavy smoke could be seen from the scene as Libyan police and armed local residents battled to control the militiamen in an area on the road to Tripoli's international airport. REUTERS/Ismail Zitouny (LIBYA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Waandamanaji mjini Tripoli
Zaidi ya watu 450 wamejeruhiwa wakati maandamano siku ya ijumaa yalipozusha mapigano katika mji huo mkuu baina ya makundi ya wanamgambo ambayo yaliendelea usiku kucha , amesema waziri wa sheria Salah al-Marghani.
Waziri mkuu Ali Zeidan, ambaye alitekwa nyara kwa muda na wanamgambo mwezi uliopita katika tukio ambalo linaelezea hali inayoongezeka ya kutokuwa na uthabiti , ametoa wito wa "kuvumiliana na kusitishwa kwa mapigano," akionya kuwa " muda unaokuja na siku zijazo zitakuwa muhimu katika historia ya nchi ya Libya".
Protesters march during a demonstration calling on militiamen to leave, in Tripoli November 15, 2013. At least 10 people were wounded in Tripoli on Friday when militiamen opened fire on hundreds of protesters who had marched on their brigade headquarters to demand that they leave the Libyan capital, a Reuters witness said. Heavy smoke could be seen from the scene as Libyan police and armed local residents battled to control the militiamen in an area on the road to Tripoli's international airport. REUTERS/Ismail Zitouny (LIBYA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)Mandamano yakiendelea mjini Tripoli
Maafisa watangaza mgomo
Usiku wa Jumamosi , maafisa wa mji wa Tripoli wametangaza , "mgomo wa nchi nzima wa siku tatu katika sekta ya umma na binafsi kuanzia Jumapili" ikiwa ni jibu kutokana na ghasia hizo. Nchi hiyo imeshuhudia ongezeko la hali isiyo tulivu wakati waasi wa zamani ambao walisaidia kuuangusha kutoka madarakani utawala wa Muammar Gaddafi uliodumu miongo kadha mwaka 2011, walipuuzia madai ya serikali ya kutaka waweke silaha zao chini.
Ghasia hizo mpya zilizuka wakati waandamanaji wakiwa wamebeba bendera nyeupe walioingia mitaani katika maeneo ya majengo ya kifahari ambayo yanatumika kama kituo cha kikosi cha Misrata, kinachoundwa na wapiganaji waliokomaa kwa vita kutoka mji wa magharibi wa Misrata, na wakidai kuwa wanamgambo hao waondoke mjini humo.
AUSSCHNITT
ATTENTION EDITORS - VISUAL COVERAGE OF SCENES OF INJURY OR DEATH
People carry a man who was injured when Libyan militiamen opened fire into a crowd of protesters in Tripoli November 15, 2013. Six people were killed and dozens more wounded in clashes between militiamen and armed residents in the capital Tripoli on Friday, state television said, in a further challenge to Libya's weak government. The bloodshed began when militiamen opened fire into hundreds of protesters demanding their eviction from the capital after they had repeatedly battled with other armed factions for control of parts of the capital. REUTERS/Stringer (LIBYA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST) TEMPLATE OUTWatu waliojeruhiwa baada ya kushambuliwa na wanamgambo
Watu wenye silaha walifyatua risasi kutoka ndani ya nyumba hizo katika eneo la Gharghour, na kuuwa waandamanaji kadha na kusababisha wanamgambo wa makundi mengine kushambulia kituo hicho cha wanamgambo wa Misrata, na kuchoma sehemu ya eneo hilo.
Mji wa pwani wa Misrata, ulioko kilomita 200 mashariki ya mji ya Tripoli, umeshuhudia mapigano makubwa kabisa kuwahi kutokea tangu vuguvugu la maandamano ya umma ya mwaka 2011.
Kikosi cha Misrata kilishambulia kambi ya jeshi mapema jana Jumamosi(16.11.2013) , na kuzusha duru nyingine ya mapambano ambapo mtu mmoja ameuwawa na wengine wanane wamejeruhiwa, kwa mujibu wa kanali Mosbah al-Harna, kamanda wa kikosi kingine ambacho kwa kawaida kiko chini ya mamlaka ya wizara ya ulinzi.
Harna amesema wanamgambo wa kikosi cha Misrata baadaye walipora kituo hicho cha jeshi, wakichukua magari, silaha na risasi.
Libya's Prime Minister Ali Zeidan places his hand on his forehead as he addresses a news conference after his release and arrival at the headquarters of the Prime Minister's Office in Tripoli October 10, 2013. Zeidan was seized and held for several hours on Thursday by former rebel militiamen angry at the weekend capture by U.S. special forces of a Libyan al Qaeda suspect in Tripoli. REUTERS/Ismail Zitouny (LIBYA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST TPX IMAGES OF THE DAY)Waziri mkuu wa Libya Ali Zeidan
Wapiganaji wengi zaidi kutoka Misrata walijaribu kuingia mjini Tripoli kutoka upande wa mashariki, na kuzusha mapigano na wanamgambo hasimu kabla ya mlolongo wa wanamgambo hao wa ziada kurejea nyuma kwa kilometa kadha.
Ngao ya Libya
Kikosi cha "Ngao ya Libya" ambacho ni kikosi kingine cha waasi wa zamani ambacho kilikuwa chini ya udhibiti wa serikali , baadaye kilitangaza kuwa kinalidhibiti eneo la Gharghour wakati wapiganaji wa Misrata wakijitoa katika eneo hilo.
Kikosi cha Ngao ya libya katika eneo lenye matatizo la mji wa mashariki wa Benghazi nacho kilikuwa lengo la maandamano mwezi Juni ambayo pia yalisababisha umwagikaji wa damu, ambapo watu zaidi ya 30 walipoteza maisha.
 Members of the Libyan security forces stand guard close to the headquarters of the General National Congress in Tripoli October 31, 2012. Protesters stormed Libya's national assembly on Tuesday, forcing the cancellation of a vote on a proposed coalition government named by the country's new prime minister just hours earlier. REUTERS/Ismail Zitouny (LIBYA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)Jeshi likilinda maeneo kuzuwia wapiganaji wa Misrata kuingia mjini Tripoli
Barabara kuelekea mji wa Tripoli kutoka upande wa mashariki imefungwa , amesema mwandishi mmoja wa shirika la habari la AFP,na mji huo sasa uko shwari hadi jana jumamosi, lakini shughuli nyingi za kibiashara na maduka zimefungwa.