Jumamosi, 29 Juni 2013

Pinda aisaliti kauli yake, aruhusu tena sherehe



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, 
Na Habel Chidawali, Mwananchi 

Kwa ufupi
  • Juzi ilikuwa ni siku ya pili mfululizo kwa Pinda kushirikia warsha katika viwanja hivyo, siku iliyotangulia alikuwa ameshiriki  sherehe kubwa iliyoandaliwa na Bunge kumwaga Spika Mstaafu ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye alitumikia nafasi ya Uspika kwa miaka mitano 2005/10.Sh

Dodoma. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amewaagiza Watanzania kuwa na uzalendo wa kuwaenzi na kuwakumbuka wenzao ambao wamefanya kazi  muda mrefu kwa kuthamini mchango wao.
Pinda alitoa kauli hiyo juzi katika viwanja vya Bunge, aliposhiriki hafla ya kuwaaga wafanyakazi waliostaafu utumishi na wale waliohamishwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuanzia 2010.
Hata hivyo, Pinda alisema  yeye ndiye aliyemwagiza Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia kuandaa hafla hiyo ili kuwatunuku zawadi na kula nao chakula pamoja na watumishi hao, ambao idadi yao ilikuwa 59 kutoka sehemu mbalimbali nchini. Hata hivyo walihudhuria 35.
Juzi ilikuwa ni siku ya pili mfululizo kwa Pinda kushirikia warsha katika viwanja hivyo, siku iliyotangulia alikuwa ameshiriki  sherehe kubwa iliyoandaliwa na Bunge kumwaga Spika Mstaafu ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye alitumikia nafasi ya Uspika kwa miaka mitano 2005/10.
 Sherehe ya juzi ambayo iliandaliwa kwa agizo la Pinda, inapingana na kauli na maagizo yake ambayo amekuwa akitoa kwa nyakati tofauti kwamba, makongamano na warsha zisizo na tija ni ufujaji fedha za umma.
“Mimi ndiye niliyeamua kufanya hivi na huu ni ubinadamu tu nikaona nimtume mama Ghasia afanye maandalizi hayo, lengo kuu la hapa ni kukaa pamoja na wenzetu na kuwaambia kuwa tunashukuru kwa kazi yenu nzuri na pia tunathamini michango yenu,” alisema Pinda.
Alisema huo ulikuwa ni mwanzo, lakini Tamisemi itakuwa ikifanya hivyo kila mwaka  kuwaaga watu wanaostaafu na wanaohamia wizara zingine.
Kuhusu wastaafu hao, alisema Serikali inapaswa kuwathamini na kutambua michango yao wakati wote kuliko kuwatelekeza kama ilivyo sasa.
Alisema kustaafu kwa mtu sio kwamba anakuwa amepungukiwa hekima na maarifa, bali ni utaratibu ukifika wakati fulani anatakiwa kupumzika.
Licha ya hilo,  aliwaagiza viongozi wa Tamisemi kuangalia uwezekano wa kuwasaidia watu wanaojiandaa kustaafu ili wajenge nyumba za kufikia na familia zao, kwani wengine humaliza muda  na kushindwa  kujenga. 
Tangu kuingia ateuliwe, Pinda amekuwa akipiga vita sherehe na ununuzi wa magari ya kifahari kwa madai kuwa, ni ubadhirifu wa fedha za umma.
Hatua hiyo inaonyesha ameanza kubariki fedha hizo kufanya sherehe.

Ijumaa, 28 Juni 2013

Wakesha wakimuombea Mzee Mandela


Mandela bado anaugua sana hospitalini
Raia wa Afrika kusini wamekesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika.
Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu.
Awali mwanawe wa kike, Makaziwe amesema afya ya babaake inaendelea kuwa njema.
Aidha Makaziwe amevikashifu vyombo vya habari kwa kukita kambi nje ya hospitali alikolazwa shujaa huyo akisema wanahabari wanapaswa kumheshimu babaake.
Rais Jacob Zuma alisema Alhamisi kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado yuko hali mahututi.
"leo angalau yuko sawa kidogo kuliko nilivyomwacha jana usiku,'' alisema Rais Zuma baada ya kuongea na madakatari wanaomtibu Mandela.
Bwana Zuma alifutilia mbali safari yake ya Msumbiji ili kumtembelea Mandela hospitalini.
Wakati huohuo mwanawe Mandela Makaziwe alisema Mzee 'bado yupo' na kuwa anaweza kuhisi mtu akimgusa.

Alhamisi, 27 Juni 2013

Familia ya Mandela yakosoa wanahabari


Ujumbe kwa Nelson Mandela
Taarifa kutoka Ikulu ya Afrika Kusini zinasema kuwa hali ya kiafya ya rais mstaafu Nelson Mandela sio nzuri na kuwa imezorota katika saa 48 zilizopita.
Baada ya kumtembelea hospitalini, mwanawe mkubwa wa kike Makaziwa, alisema hali inaonekana kuwa mbaya lakini akaongeza kuwa Mandela anaweza kuwasikia jamaa zake wanapomuita huku akijaribu kufungua macho yake.
Makaziwe amesema “Nimekasirishwa sana. Kwa sababu Mandela ni kiongozi mashuhuri duniani, haimaanishi utu wake udhalilishwe pamoja na kuvuka mipaka kuingilia mambo yake binafsi Hapa naona kuna ubaguzi wa rangi, huku vyombo vingi vya kimataifa vikivuka mipaka, ni kama ndega aina ya Tai au Vulture wanaosubiri Simba kumla mnyama aliomuwinda kisha wakimbilie mzoga.
Wamevuka mipaka ya maadili. Wakati hayati Margaret Thatcher alipokuwa mgonjwa mbona sikuona, ukaribu wa vyombo vya habari kiasi ninachokiona kwa banangu? Ni kwa sababu hii ni nchi ya kiafrika. wanahisi kuwa hapa wanaweza kuvuka mipaka wanavyotaka, '' alisema Makaziwe
Mapema leo, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alifutilia mbali ziara yake ya kwenda Musumbiji baada ya kumtembelea hospitalini aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Rais Zuma amesema kuwa Bwana Mandela yuko katika hali mbali ya afya.
Msemaji wa Zuma Mac Maharaj alisema kuwa hali yake imedorora zaidi
Mandela ambaye, ni rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amelazwa hospitalini tangu tarehe 8 mwezi Juni akiugua maradhi ya mapafu.
Madaktari wanasemekana kufanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa Mandela anapona.
Vikundi vya watu wenye huzuni mkubwa kuhusu hali ya afya ya Mandela, walikusanyika nje ya hospitali alikolazwa, wakiwa na ujumbe wa ugua pole kwa Mandela
Wadadisi wanasema kuwa wananchi wa Afrika Kusini wanaonekana kuwa tayari kwa habari zozote sasa kuhusu hali ya Mandela.
"tutasikitika sana ikiwa tutapata habari za kifo chake, lakini pia tutakuwa tunasherehekea maisha yake. Amefanya mambo mengi zaidi kwa nchi yetu,'' alisema kijana John Ndlovu, mwenye umri wa miaka 25.
Zuma alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa marais nchini Msumbiji, hii leo lakini akaamua kuakhirisha safari yake.
Taarifa kutoka kwa ofisi yake ilisema kuwa anaendelea kuwapongeza wananchi wa Afrika Kusini wanaoendelea kuiombea familia ya Madiba.
Uamuzi wa Rais Zuma kufutilia mbali ziara yake ambako alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa kikanda kuhusu uekezaji anaonyesha wazi kuwa hali ya Mandela inaendelea kuzorota zaidi kulingana na mwandishi wa BBC mjini Johannesburg Mike Wooldridge.

Zaidi ya watu milioni 7 sasa wanapata matibabu dhidi ya HIV Afrika: UNAIDS


Vita dhidi ya Ukimwi
Wakati Muungano wa nchi za Afrika (AU) unapoanza mkutano wake wa 21 na kuadhimisha miaka 50 ya kuungana kwa bara Afrika, Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu virusi vya HIV na UKIMWI (UNAIDS), umetoa ripoti mpya inayoonyesha hatua zilizopigwa katika kupiga vita UKIMWI barani humo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya watu wanaopokea matibabu ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV imeongezeka na kufikia milioni 7.1 mwaka 2012, wakati idadi hiyo ilikuwa chini ya milioni 1 mnamo mwaka 2005. Mwaka uliopita pekee, idadi hiyo ilipanda kwa watu milioni moja.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya UNAIDS, vifo kutokana na UKIMWI pia vimeendelea kupungua- viwango vya vifo vikishuka kwa asilimia 32 kati ya 2005 na 2011, huku viwango vya maambukizi mapya ya virusi vya HIV vikishuka kwa asilimia 33 kati ya 2001 na 2011.
Ripoti hiyo inasema ufanisi huu umetokana na uongozi imara na wajibu wa ushirikiano barani Afrika na katika jamii ya kimataifa, huku ikitoa wito kuwepo juhudi endelevu ili kuhakikisha bara Afrika linafikia lengo la kutokomeza maambukizi, ubaguzi na vifo vitokananvyo na UKIMWI.

Ibua mbinu kuboresha afya na si kubuni dawa mpya za kulevya: UNODC

Ujumbe katika kuadhimisha siku ya leo
Fanya afya kipaumbele chako na siyo madawa ya kulevya, ni ujumbe mahsusi wa Umoja wa Mataifa hii leo ambayo ni siku ya kimataifa dhidi ya matumizi na usafirishaji wa madawa ya kulevya. Ripoti ya Flora Nducha inafafanua zaidi.(Ripoti ya Flora)
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti madawa ya kulevya na uhalifu UNODC inaeleza bayana kuwa matumizi ya madawa yanaharibu afya na ustawi wa binadamu huku ikionyesha wasiwasi kutokana na kuibuka kwa tatizo jipya la ongezeko la mahitaji ya madawa yasiyo chini ya udhibiti wa kimataifa ambayo huchanganywa na watumiaji hulewa, madawa ambayo ni tofauti na yale yaliyozoeleka ambayo ni Cocaine, Heroine na bangi.
Mkuu wa maabara ya kisayansi ya UNODC Justice Tettey anasema kuwa madawa hayo yanauzwa kihalali kabisa lakini mchanganyiko wake hujipatia majina ya mtaani kama vile SPICE au Meow-Meow na vijana kudhani kuwa hayana madhara.
(SAUTI YA Tettey)
Fatma Musa Juma ni mmiliki wa moja ya makazi ya kusaidia watumiaji wa madawa ya kulevya huko Tanzania Zanzibar kurejea katika maisha ya kawaida. Je vijana hupataje fedha za kununua madawa hayo?
(SAUTI YA FATMA)

Umuhimu wa chanjo kwa watoto

Mamilioni ya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano wamepewa chanjo katika wiki ya mwisho ya mwezi Aprili kote duniani.
Mtoto akipewa chanjo ya Polio
Mtoto akipewa chanjo ya Polio

ukubwa wa habari
Josephat Kioko
Kenya imekamilisha wiki moja ya Chanjo ya kitaifa kwa watoto ambayo kulingana na shirika la afya duniani W.H.O. Chanjo hiyo inatolewa katika wiki ya mwisho ya mwezi Aprili. Wiki ya mwisho ya mwezi Aprili imeshuhudia mamillioni ya watoto kote duniani wakipokea chanjo dhidi ya magonjwa mbali mbali, yanayoathiri watoto.

Wiki hii ya chanjo inatambuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto-UNICEF. Shirika la afya duniani-W.H.O. linakadiria kuwa watoto wachanga million 22 hawapati chanjo inayostahili, ambapo zaidi ya million 1.5 walio na umri chini ya miaka 5 hufariki kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuiwa kupitia chanjo.

Chanjo ina tiba ya kuaminika, na wataalamu wanasema inaweza kuzuia vifo kati ya million 2 na million 3 kila mwaka. Lakini ripoti ya takwimu za UNICEF inasema kwa kifupi mtoto mmoja kati ya 5 hajapokea chanjo, hasa katika mataifa yanayokabiliwa na changamoto nyingi au mgogoro wa kisiasa.

Utafiti unaonyesha kuwa watoto kutoka familia zenye kipato cha juu, au matajiri, wanapata huduma bora za matibabu, pamoja na chanjo na dawa nyingine za kutibu magonjwa. Serikali ya Kenya inajaribu kuondoa au kupunguza tofauti hiyo ya kitabaka, kwa kuhakikisha kila mtoto anapata huduma bora.

Shirika la UNICEF linasisitiza kuwa kila nchi inahitaji mchango wa kisiasa katika kusambaza huduma za chanjo kwa watoto wengi, hasa katika familia maskini na sehemu kame zaidi.

Huko Kenya kampeni hiyo imefanikishwa kupitia mashirika ya kijamii na Vyombo vya habari, ili kusaidia kuondoa jamii nyingi kutoka mila na tamaduni potofu ambazo hukataa au kupuuza  manufaa ya Chanjo.

Kenya imo katika hatua za mwanzo za mfumo mpya wa serikali za ugatuzi, ambazo zimepewa jukumu pia la kuboresha elimu na afya kwa kila mwananchi.
Chanjo kwa kila mtoto aliye na umri chini ya miaka mitano ni kati ya mikakati hiyo, ambapo maudhui kuu ya mwaka huu ni kuhamasisha kina mama umuhimu wa kuwapa watoto wao  Chanjo.

Kongamano la kimataifa kuhusu chanjo pia limekuwa likiendelea Abu Dhabi, ambako shinikizo limetolewa kwa wahusika kushauriana na wanaotengeneza dawa za chanjo, kupunguza gharama kubwa iliyopo ili kuwafikia wasio na uwezo duniani.

Familia yakutana kujadilia hali ya afya ya Madiba.



Familia yakutana kujadilia hali ya afya ya Madiba huku askofu mkuu akimwombea amani katika siku zake za mwisho.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela nyumbani kwake Qunu, akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake Julai 18, 2012.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela nyumbani kwake Qunu, akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake Julai 18, 2012.
ukubwa wa habari
Rais wa Afrika Kusini Jacob zuma ameahirisha safari yake ya Msumbiji wakati rais wa zamani Nelson Mandela akiwa bado katika hali mbaya ya afya katika hospitali moja mjini Pretoria. Madaktari wanasema rais huyo wa zamani amewekewa mashine za kumsaidia kupumua.

Kiongozi huyo wa zamani ambaye alipigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo amelazwa katika hospitali kwa takriban wiki tatu sasa kutokana na maambukizo ya mapafu.

Askofu mkuu wa Capetown Thabo Makgoba Jumanne aliongoza maombi ya bwana Mandela rais wa kwanza mweusi na kutakia amani  na utulivu katika siku zake za mwisho.

Jamii ya bwana Mandela imekusanyika katika nyumba yake katika kijiji cha Qunu mashariki mwa jimbo la Cape na vyombo vya habari vya Afrika Kusini vinaripoti kwamba watoto wake waliitisha mkutano ili kujadili masuala muhimu ya kifamilia.

Rais wa Marekani Barack Obama anategemewa kuwasili Afrika Kusini Ijumaa hii kama sehemu ya ziara yake ya wiki nzima barani Afrika. Atatembelea kisiwa cha Robben ambako bwana Mandela alifungwa jela kwa miaka 27.

Rais Obama atua Senegal kwa ziara Afrika


Hi ni ziara ya pili ya Rais Obama Afrika
Rais Barack Obama amewasili Senegal katika ziara yake ya wiki moja barani Afrika na anatarajia kuzuru Afrika Kusini na Tanzania akilenga kustawisha demokrasia na masuala ya uchumi.
Hii ni ziara ya pili ya Obama barani Afrika tangu achaguliwe Rais mwaka 2008.
Hata hivyo ziara yake inatarajiwa kufifishwa na hali mbaya ya afya inayomkabili aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela. Ikulu ya white house imesema kuwa itategemea uamuzi wa familia ya Bwana Mandela iwapo Rais Obama anaweza kumtembelea hospitalini.
Katika mkutano wake wa leo na rais wa nchi hiyo, Mackey Sall, Rais Obama anatajiriwa kuipa heko Senegal kwa rekodi yake nzuri ya uthabiti ikizingatiwa iko kwenya kanda yenya misukosuko ya kisiasa.
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa muhimu katika ziara ya Obama ni kustawisha demokarsia na nchi zote tatu anazotembelea ziko na demokasria thabiti.
Ni ziara ya pili ya Obama katika bara la Afrika tangu kuwa rais wa Marekani mwaka 2008.

Hali ya Mzee Mandela inaendelea kuzorota


Ujumbe kwa Nelson Mandela
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefutilia mbali ziara yake ya kwenda Musumbiji baada ya kumtembelea hospitalini aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Rais Zuma amesema kuwa Bwana Mandela yuko katika hali mbali ya afya.
Msemaji wa Zuma Mac Maharaj amesema kuwa hali yake imedorora zaidi katika saa 48 zilizopita.
Mandela ambaye, ni rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amelazwa hospitalini tangu tarehe 8 mwezi Juni akiugua maradhi ya mapafu.
Madaktari wanasemekana kufanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa Mandela anapona.
Vikundi vya watu wenye huzuni mkubwa kuhusu hali ya afya ya Mandela, walikusanyika nje ya hospitali alikolazwa, wakiwa na ujumbe wa ugua pole kwa Mandela
Wadadisi wanasema kuwa wananchi wa Afrika Kusini wanaonekana kuwa tayari kwa habari zozote sasa kuhusu hali ya Mandela.
"tutasikitika sana ikiwa tutapata habari za kifo chake, lakini pia tutakuwa tunasherehekea maisha yake. Amefanya mambo mengi zaidi kwa nchi yetu,'' alisema kijana John Ndlovu, mwenye umri wa miaka 25.
Zuma alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa marais nchini Msumbiji, hii leo lakini akaamua kuakhirisha safari yake.
Taarifa kutoka kwa ofisi yake ilisema kuwa anaendelea kuwapongeza wananchi wa Afrika Kusini wanaoendelea kuiombea familia ya Madiba.
Uamuzi wa Rais Zuma kufutilia mbali ziara yake ambako alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa kikanda kuhusu uekezaji anaonyesha wazi kuwa hali ya Mandela inaendelea kuzorota zaidi kulingana na mwandishi wa BBC mjini Johannesburg Mike Wooldridge.

Watu saba wauwawa Afghanistan

 
 
Watu 7 wameuwawa, wakiwemo walinzi 3 wa makaazi ya rais wa Afghanistan na wanamgambo 4 wa Taliban katika shambulio lililotokea nje ya Ikulu ya rais, ambayo pia yapo karibu na ofisi za shirika la kijasusi la Marekani CIA.
Mkuu wa Jeshi la Polisi mjini Kabul, Ayoub Salangi ameliambia shirika la habari la Ujerumani DPA, wanamgambo wanne walikuwemo katika gari ambao walikuwa na vitambulisho bandia, waligunduliwa na vikosi vya usalama na waliuwawa kabla ya kutimiza lengo lao.
Nae msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan Sediq Sediqqi amesema walinzi watatu kutoka kikosi maalum cha kinachuhusika na ulinzi wa rais (PPS) wameuwawa katika purukushani za kufyatuliana risasi.
Smoke rises from the site of an attack in Kabul June 25, 2013. The Taliban claimed responsibility on Tuesday for the early morning attack on the presidential palace and nearby government and other buildings as fighting raged in the area. REUTERS/Mohammad Ismail (AFGHANISTAN - Tags: POLITICS CIVIL UNREST) / li  
Moshi wa miripuko kutoka karibu na makazi ya rais
PPS ni kikosi maalumu chenye dhamana ya ulinzi wa makazi ya rais, mazingira, ofisi zilizopo ndani ya makazi hayo pamojo na ulinzi wa rais Hamid Karzai mwenyewe na familia yake.
Tayari waasi wa Taliban wamedai kuhusika na shambulio hilo kwa kusema malengo yao yalikuwa makazi ya rais, ofisi za CIA zilizopo karibu na makazi hayo pamoja na Wizara ya Ulinzi. Msemaji wa wanamgambo hao Zabihullah Mujahid amesema idadi kadhaa ya raia wa kigeni na wanajeshi wa Afghanistan wameuwawa katika shambulio hilo.
Kwa mujibu wa taarifa za serikali ya Afganistan, kwa kutumia vitambulisho baandia wanamgambo hao waliweza kufika mpaka katika eneo la mbele lenye ulinzi mkali la karibu na makazi ya rais lakini hawakuweza kufikika katika jengo lenyewe.
Mmoja wa watu walioshuhudia amesema wanamgambo hao walitoka katika gari walililokuwemo wakiwa wamevaa sare za kijeshi na kuanza kuwafyatulia risasi walinzi walikuwepo katika eneo hilo. Amesema tukio hilo la kufyatuliana risasi kati ya wanamgambo na walinzi lililodumu kwa karibu masaa mawili limetokea umbali wa meta 20 kutoka katika lango kuu la kuingia katika makazi ya rais.
Takribani miripuko 16 na milio ya risasi ilisikika mapema leo na moshi mkubwa kuonekana ukifuka kutoka katika eneo la makazi ya hayo. Maafisa wa makazi hayo wamesema mapigano hayo yametokea wakati rais Karzai akiwa ndani ya makazi yake. Wanamgambo hao walikabilina vikali na walinzi wa eneo hilo pamoja na maafisa wa Marekani karibu na ofisi ya CIA kabla hawajauwawa.
Shambulio hilo limetokea muda mfupi kabla ya Karzai kufanya mkutano wake na waandishi habari. Kundi la waandishi hao pamoja na wanafunzi waliokuwepo nje ya lango hilo walilazwa chini wakati wa tukio hilo ingawa hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa. Kiongozi huyo vilevile alipangiwa kwenda kuzindua mkutano wa kitaifa kuhusu sera ya vijana mjini Kabul, ambao baadae uliendelea pasipo uwepo wake.
Aidha shambulio hilio linatokea ikiwa imetimia wiki moja tu baada ya Taliban kufungua ofisi ya mazungumzo ya kisiasa mjini Doha, Qatar, ikiwa na lengo la kufanya majadiliano na wawikilisha wa Marekani na serikali ya Afghanistan. Wanamgambo hao wameasema wataendelea na mazungumzo sambamba na kuendeleza mapigano.
Mwandishi: Sudi Mnette DPA
Mhariri:Yusuf Saumu

Jumatano, 26 Juni 2013

Mandela aifunika ziara ya Obama

Rais Barack Obama anaanza ziara iliyosubiriwa kwa hamu barani Afrika, huku hali ya Nelson Mandela ikionekana kuiziba ziara hiyo, kwani macho na masikio yote yameelekezwa Afrika ya Kusini ambako Mandela yu mahututi.
Familia ya Rais Obama inaondoka leo (26.06.2013) kwa ziara ya wiki moja barani Afrika itakayoifikisha nchini Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania kwa kile ambacho Ikulu ya Marekani inasema ni kuhamasisha demokrasia na fursa za kiuchumi kwenye bara hilo lililo asili ya wazazi wa familia hiyo.
Lakini hali inayozidi kuzorota ya afya ya Mandela inaonekana kuitanda ziara ya Obama.
Shaka kwamba kiongozi huyo ambaye ni alama ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi duniani anaweza kuiaga dunia ndani ya siku chache zijazo, imezusha wasiwasi juu ya ratiba ya Rais Obama.
Tayari Ikulu ya Marekani imesema kwamba itashauriana na familia ya kiongozi huyo wa ukombozi nchini Afrika ya Kusini kuona ikiwa familia ya Obama inaweza kumtembelea hospitalini.
Mandela ni shujaa wa Obama
Mzee Nelson Mandela katika sherehe yake ya kuzaliwa miaka minne iliyopita. Mzee Nelson Mandela katika sherehe yake ya kuzaliwa miaka minne iliyopita.
Binafsi, Obama amewahi kumtaja Mandela mara kadhaa kama shujaa wake wa kisiasa, lakini tayari Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika ya Kusini, Maite Nkoane Mashebane, ameshasema kwamba ombi hilo halitawezekana kutekelezwa kwa kuwa Mandela yuko kwenye hali mbaya.
Mara ya mwisho Obama kuonana na Mandela ilikuwa ni mwaka 2005, pale Mandela alipokuwa mjini Washington, Marekani, na Obama akiwa ndio kwanza amechaguliwa kuwa seneta.
Hata hivyo, viongozi hao wawili wamewahi kuzungumza kwa njia ya simu mara kadhaa baada ya hapo, ingawa hapajawahi kuwapo kwa mazungumzo ya ana kwa ana kati ya maraisi hao wawili wa kwanza weusi kwa mataifa yao, tangu Obama kuingia madarakani mwaka 2008.
Ikulu ya Marekani inaichukulia ziara hii ya Obama kama nafasi ya kufidia muda mrefu ambao Rais Obama ameshindwa kupanga safari ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Mara ya mwisho Obama kutembelea sehemu hiyo ya Afrika, ilikuwa ni pale aliposimama kwa muda nchini Ghana, mwaka 2009.
Fadhaa za Waafrika dhidi ya Obama
Wakati Nelson Mandela alipotoka jela mwaka 1990. Wakati Nelson Mandela alipotoka jela mwaka 1990.
Tangu mwanzo baadhi ya wachambuzi waliichukulia ziara hii ya Obama kama yenye lengo la kupunguza fadhaa za Waafrika kwa kiongozi huyo wa taifa kubwa duniani na mwenye asili ya bara hilo, lakini aliyeonekana kulipuuzia kwenye awamu ya kwanza ya uraisi wake.
Tayari ratiba ya Obama barani Afrika imeitenga Kenya na kuwakera wengi nchini humo, nchi ambayo ni nyumbani kwa baba mzazi wa Obama na ambako ndiko pia waliko ndugu zake wake wa ubabani.
Na sasa, ikiwa afya ya Mandela ndiyo itakayoamua jaala ya ziara ya Obama barani Afrika, na kwa hivyo kutokea uwezekano wa kushindwa kuzitembelea baadhi ya sehemu, kwa kushindwa kurefusha ratiba yake, hilo litaongeza fadhaa zaidi.
Mwandishi: Mohammed Khelef/AP/AFP
Mhariri: Josephat Charo

Kenya: Ziara ya Obama Afrika

Rais wa Marekani Barack Obama anaanza ziara yake ya pili barani Afrika wiki hii katika nchi tatu,Senegal,Afrika Kusini na Tanzania.
Kwa mara nyingine tena Obama ambaye babake ni mzaliwa wa Kenya hataizuru nchi hiyo na badala yake amechagua nchi jirani ya Tanzania,suala hili limezua mjadala mkali nchini Kenya hasa ikizingatiwa naye Rais Uhuru Kenyatta wiki hii pia anaanza ziara barani Asia na kuzua hoja ya je ni wakati wa Kenya kuelekeza macho yake Mashariki. Caro Robi amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya Herman Manyora na kwanza alimuuliza nini mtazamo wake kuhusiana na suala hili? Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Afya ya mandera kutoathiri ziara ya Obama


Zuma amesema yeye na makamu wa rais wa chama cha Africa National Congress, ANC, Cyril Ramaphosa walimtembelea Mandela usiku wa kuamkia leo. Lakini amekataa kutoa maelezo zaidi kuhusu afya ya Mandela, zaidi ya kusema kuwa yuko katika hali mbaya sana. Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kufanya ziara nchini Afrika Kusini wiki hii, lakini Zuma amesema kuwa kudorora kwa afya ya Mandela hakutaathiri ziara hiyo.
Kudorora kwa afya ya Mandela wikendi hii, ikiwa ni wiki mbili tangu alipolazwa akiwa katika hali mbaya lakini imara, kumeibadili hali kutoka kwenye kumuombea kupona haraka hadi kwenye kuanza maandalizi ya kumuaga. "Kama ni wakati wa yeye kuondoka, anaweza kuondoka, namuombea kwa Mungu ampokee vyema," alisema Petunia Mafuyeka, ambaye ni Nesi wakati akielekea kazini mjini Johannesburg.

Mzee Mandela afanyiwa maombi maalum



 Mandela anaendelea kupokea matibabu hospitalini

Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town, Afrika Kusini, Thabo Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anaugua sana hospitalini.
Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia.
Jamaa za Nelson Mandela wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria.
Afya ya Bwana Mandela ilikuwa mbaya zaidi Jumapili.
Maombi hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo kumtembelea Mandela hospitalini ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa akilazwa kwa wiki mbili na nusu zilizopita baada ya kuugua mapafu.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa wajukuu wa rais huyo wa zamani wa Afrika kusini wanakutana nyumbani kwake kijijini katika mkoa wa Eastern Cape province, ambako viongozi wa kitamaduni wamealikwa.
Halikopta ya jeshi kadhalika zilionekana zikipaa karibu nyumbani kwa mandela. Afisi ya Rais jacob Zuma ilitangaza jumapili kuwa hali ya mzee Mandela ya afya ilikuwa mbaya sana.


Hali ya wasiwasi kuhusu afya ya Mandela



Mzee Nelson Mandela

Wananchi wa Afrika Kusini hii leo wamekuwa na wasiwasi baada ya rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kutangaza kuwa hali ya afya ya rais mstaafu Nelson Mandela sio nzuri sana.
Asubuhi waliamkia kwenda kazini wasijue taarifa watakazopokea hii leo baada ya rais Zuma kutoa taarifa hiyo.
Taarifa kutoka ikulu ya rais zilisema Jumapili jioni kuwa Mandela alikuwa amezidiwa ingawa madaktari wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa anapata afueni.
Afisaa mmoja mkuu alisema kuwa raia wa Afrika Kusini wasiwe na matumaini kupita kiasi.
Mandela ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, akiwa na umri wa miaka 94,alipelekwa hospitalini mapema mwezi huu, ikiwa ni mara ya tatu kwake kulazwa hospitalini akiugua ugonjwa wa mapafu mwaka huu.
Rais Jacob Zuma alisema Jumapili kuwa alimzuru Mandela Hospitalini na kuzungumza na mkewe kuhusu hali ya rais mstaafu.
Madaktari wanaomtibu Mzee Nelson Mandela wamesema hali yake imekuwa sio nzuri kwa saa ishirini na nne zilizopita na sasa ni mahututi.
Habari hizo zimekuja kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ya Afrika Kusini.
Taarifa hiyo imesema bado Mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.
Rais Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela na pia kuzungumza na jopo la matabibu wanaomtibu.
Baadaye bwana Zuma alirejea kauli yake ya kulitaka taifa na dunia kumuombea Mzee Mandela apate nafuu.


Jumamosi, 22 Juni 2013

Nyerer eHe was Baba wa taifa, father of the nation.

Nyerere the Father of Southern African Liberation

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere was the father of southern African liberation, and one of the founding fathers of the Southern African Development Community. Born in Butiama near Lake Victoria on 13 April 1922, when he passed away 10 years ago on 14 October 1999, Africans everywhere shared the sense of loss felt by Tanzanians.
15 October 2009

He was Baba wa taifa, father of the nation, the moving force for the independence of Tanganyika on 9 December 1961 and for its unity with Zanzibar on 26 April 1964 to create the United Republic of Tanzania. A charismatic leader of sharp intellect and great personal integrity, he welded a country and a national identity from over 120 ethnic groups, united by their language Swahili and by a social harmony constructed on the ideals of peace, justice, unity and personal commitment.

His firm support for equality and tolerance ranged across all diversity of race, religion, class and gender. He encouraged Tanzanian women to play a leadership role in society and adopted a parliamentary system that has guaranteed seats for women. His pursuit of an equitable socio-economic society through collective self-reliance was more difficult than he had envisaged, and he once said that "we are very good at sharing the wealth in Tanzania but I only wish we had made more wealth to share."

Tanganyika's independence in 1961 was an inspiration to those who believed that political independence could be achieved by non-violent means and he worked tirelessly in support of this goal for Zambia (1964), Malawi (1964), Botswana (1966), Lesotho (1966), Mauritius (1968), Swaziland (1968) and Seychelles (1976). When the other countries of southern Africa were forced into wars of liberation to eventually achieve the same end, Tanzania provided political, material and moral support until independence and majority rule were achieved in 1975 (Mozambique, Angola), 1980 (Zimbabwe), 1990 (Namibia) and finally, 1994 (South Africa). Nyerere pursued the ideals of liberation, democracy and common humanity into the rest of the continent and, with the leaders of the other few African countries that were independent in 1963, established the Organisation of African Unity (OAU), which later became the African Union. The main objective was political liberation for the rest of the continent.

Their tool for achieving this, the OAU Liberation Committee, was hosted by Tanzania, and most liberation movements were based there at one time or another. Nyerere was one of nine leaders who came together in 1980 to establish the Southern Africa Development Coordination Conference (SADCC), which later became the Southern African Development Community (SADC). The leaders of Tanzania, Zambia and Botswana formed the Front Line States in 1974 to work together in a united front for common security and for majority rule in neighbouring countries, under the chairmanship of Nyerere, and this was a forerunner of the SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation.

The political changes in Namibia and South Africa in 1990 and 1994, changed the face and future of the African continent, and completed the work of the OAU Liberation Committee, but socio-economic development has remained a vision. Through Nyerere's leadership, all Tanzanians were able to take pride in their contribution to the liberation of the region, through "people-to-people" support in hosting refugees, contributing food, clothing, and shillings.

One very successful campaign drew a voluntary contribution of one shilling each to support Mozambique. Although the decision to initiate the SADCC was taken in Arusha, Tanzania and the launch was in Lusaka, Zambia, the organization was hosted by Botswana, and Nyerere used any occasion to give credit for its formation to his colleague and close friend, the late President Seretse Khama of Botswana. When the SADCC was formed in April 1980, Khama saw the difficulties ahead when he predicted that, "The struggle for economic liberation will be as bitterly contested as has been the struggle for political liberation." SADC, formally established by the Windhoek Treaty in 1992, has turned its vision of free trade into a formal agreement launched in 2008, and most member states have developed a national Vision of where they want to be by 2016 or 2020. The Lagos Plan of Action for socio-economic development of Africa was the OAU's plan of action 1980-2000.

Meeting in Lagos in April 1980 just after the SADCC was launched, African leaders inspired by Nyerere and Khama, reaffirmed their commitment to set up an African Economic Community by the year 2000, "so as to ensure the economic, social and cultural integration of our continent." The aim of this community, in the terminology popularized by Nyerere, "shall be to promote collective, accelerated, self-reliant and self-sustaining development of Member States; co-operation among these States; and their integration in the economic, social and cultural fields." Nyerere retired as president of Tanzania in 1985 and as chairman of the party Chama Cha Mapinduzi in 1990.

Tanzania has had three presidential transitions since then, first to Ali Hassan Mwinyi for two five-year terms, in 1995 to Benjamin Mkapa for two five-year terms, and then in 2005 to the current President, Jakaya Kikwete, who will seek re-election in 2010. After leaving office, Nyerere devoted his vision to mechanisms to strengthen developmental links between developing countries of the South. He chaired the South Commission 1987-90, and dedicated the next decade to the service of the South Centre, tirelessly fund-raising for a capital fund and operating costs. Mwalimu often said that his generation had achieved at least one goal, that of the political liberation of Africa, and that the next generations must take up the next goals. A long memorial verse by his close friend and colleague, Dr Kenneth Kaunda, the former President of Zambia, reminds us all that, "The best way of mourning him is to carry on where he has left."

Kwa nini Mwalimu Nyerere hakupenda serikali tatu?

Mwalimu Nyerere


 
Kwa ufupi
  • Tukirudi kwenye Serikali tatu, wiki iliyopita nilitaja utata wa kwanza katika Muungano ambapo ziliundwa Serikali mbili, yaani ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Wiki iliyopita nilieleza msimamo aliokuwa nao Baba wa Taifa kuhusu utawala wa Serikali tatu, ambao sasa umependekezwa katika rasimu ya Katiba.
Pamoja na kuwashukuru wasomaji kwa kutuma ujumbe wa simu, naona kuna watu hawakunielewa.
Katika makala ile nilikuwa natoa historia ilivyokuwa hadi tukawa na Serikali mbili. Sikumaanisha kwamba kila alichokiamini Nyerere ndiyo Watanzania wakifuate.
Kwanza ieleweke kwamba, tangu tunapata uhuru hatukuwahi kuwa na utawala unaowashirikisha wananchi kikamilifu, hata kama kulikuwa na chaguzi kila baada ya miaka mitano.
Tukirudi kwenye Serikali tatu, wiki iliyopita nilitaja utata wa kwanza katika Muungano ambapo ziliundwa Serikali mbili, yaani ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Watu walijiuliza, iko wapi Serikali ya Tanganyika? Jibu la swali hilo alikuwa nalo Nyerere peke yake na hakutaka watu waendelee kuuliza. Huu nao ulikuwa utata mwingine.
Kumbuka tangu mwaka 1962 baada ya Mwalimu Nyerere kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, mabadiliko makubwa yalifanyika ikiwa ni pamoja na kudhoofisha utendaji wa asasi za kiraia, vyombo vya habari na ilipofika mwaka 1965, mfumo wa vyama vingi ukafutwa rasmi.
Hapo ndipo Chama cha TANU kikashika hatamu za uongozi. Hakukuwa na uhuru wa kutosha wa kujieleza kwa wananchi.
Nyerere aliwadhibiti hata wale walioonekana kuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa nje ya Serikali yake.
Mfano mzuri ni Mwenyekiti wa Chama cha Chausta, James Mapalala ambaye aliambulia kutiwa vizuizini. Mwingine ni kada wa UDP, Lameck Bugohe ambaye pia alishiriki kuanzisha TANU; na wengineo wengi. Haikushangaza mwaka 1983 kwa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe akapoteza urais wake kwa kuhoji tu Muungano.
Mwalimu aliendelea na msimamo wake huo hata baada ya kung’atuka mwaka 1984, na baadaye alipostaafu uenyekiti wa CCM.
Hata mwaka 1993, Nyerere alipambana na kundi la Wabunge (G55) waliotaka Serikali ya Tanganyika.

Mwalimu aliandika kitabu cha ‘Uongozi wetu na hatima ya Tanzania’ akimlaumu aliyekuwa Waziri Mkuu, John Malecela na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba akidai kuwa hawakumshauri vizuri Rais Ali Hassan Mwinyi kuhusu suala hilo.
Hadi anafariki, Nyerere hakuwahi kulegeza msimamo, na sasa umeshikiliwa na CCM. Ni wakati wa wananchi kuamua wanachokitaka bila kufungwa na historia, itikadi za vyama wala dini.

Maskini CCM wanakumbuka shuka asubuhi?





Lauden Mwambona 

  • Hata mwenyekiti wake ambaye ndiye alikuwa Rais, hakuwa na ubavu wa kutamka mambo hadharani kabla ya kufikishwa kwenye Kamati Kuu na hatimaye Halmashauri Kuu.


Tangu CCM ifanye mabadiliko ya viongozi ngazi ya juu kwa kumteua Abdulrahman Kinana kuwa Katibu Mkuu imeonekana kurudi kwenye mstari wa utendaji kazi ulioanishwa kwenye nyaraka mbalimbali za chama.
Nyaraka za CCM ikiwamo Katiba zinatamka wazi kwamba jukumu lake kubwa ni kushika dola kwa kuunda Serikali. Zinasisitiza kwamba chama hicho kitaisimamia Serikali yake ili iweze kutenda haki na kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi.
Ni kawaida kwa chama kinachounda Serikali  kinatakiwa kuwa na nguvu kuliko Serikali yenyewe.
Ni kwa msingi huo, CCM tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa ya kwanza  katika kujadili mambo muhimu ya kitaifa na kuweka msimamo imara kabla Serikali haijaanza kufanya lolote.
Hata mwenyekiti wake ambaye ndiye alikuwa Rais, hakuwa na ubavu wa kutamka mambo hadharani kabla ya kufikishwa kwenye Kamati Kuu na hatimaye Halmashauri Kuu. Enzi hizo, pamoja na kwamba walikuwapo viongozi ndani ya CCM au serikalini waliokuwa watoaji wa hoja za msingi, lakini CCM ilikuwa imara kuwaita mara moja na kuzijadili hoja zao kabla ya kutoa uamuzi.
Ndiyo maana kwa ngazi za mikoa na wilaya, wakuu wa mikoa na wilaya waliwajibika kutoa taarifa za kazi kwa Halmashauri ya CCM ngazi husika.
Viongozi wa CCM ngazi ya wilaya na mikoa walikuwa na nguvu kuliko wakuu wa mikoa  kwani enzi hizo chama kikiazimia kukuondoa mkuu wa idara kutokana na utendaji mbaya, ilikuwa ni mara moja unaondoka.
Hata hivyo baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi, CCM ilianza kuyumba kiutendaji na kusababisha watendaji Serikali kushika hatamu. Tangu mwaka 1995 hadi mwaka jana, CCM ilishakubali Serikali iongoze chama badala ya yenyewe kuiongoza Serikali.
Vigogo wengi wa Serikali na wabunge walituhumiwa kwa wizi, rushwa, ufisadi wa kutisha, lakini CCM haikuchukua hatua zozote badala yake iliafikiana na Serikali yake watuhumiwa wote waendelee na kazi na ubunge.
Wapo walioshtakiwa mahakamani kuisababishia hasara Tanzania, lakini badala ya CCM kukaa vikao na kuwasimamisha  uanachama , iliogopa na kuwafanyia kampeni waendelee kuwa wabunge.
Wapo walioundiwa tume kwa ufisadi, badala ya CCM kukaa na kuwajadili kwa kina ili kutoa ufafanuzi mbele ya Watanzania, ilikaa kimya bila kauli yoyote. Mambo yalipozidi kipimo, ndipo mwaka jana CCM ilipoamua kuwarudisha kwenye uongozi wakongwe wa siasa na kutoa maelekezo kwamba CCM lazima iisimamie Serikali yake.
Maelekezo hayo yameanza kutekelezwa katika baadhi ya wilaya ambapo baadhi ya watendaji wameanza kuitwa na kuhojiwa kwa makosa mbalimbali.
Nao Watendaji wa CCM kitaifa  wakiongozwa na Kinana wamekuwa wakizunguka mikoa mbalimbali kufafanua utendaji wa kazi kati ya CCM na Serikali yake.
Wanasisiti za kwamba CCM lazima iisimamie Serikali yake kwa kuwaita kwenye vikao vya ndani watendaji wenye matatizo. Hatua hiyo inaanza kutekelezwa wakati watendaji wengi wa Serikali wameshajenga kiburi cha kwamba CCM haina nguvu kuliko Serikali.
Msimamo wa kutaka CCM iisimamie Serikali hauwatishi wakurugenzi wa halmashauri, watendaji wa idara ngazi za mikoa bali unawatisha wakuu wa mikoa  na wilaya pekee.

Ijumaa, 21 Juni 2013

Mimi nasema muwapige tu


: Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda.

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda.
Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda.
 
Kauli ya waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda bungeni Dodoma katika mabishano kuhusu matumizi ya nguvu yanayofanywa na jeshi la Polisi nchini  humo ilitolewa bungeni alhamisi wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa mbunge wa Kilwa Kaskazini Murtaza Mangungu .

Waziri mkuu huyo alijibu  “Ukifanya fujo umeambiwa usifanye hiki ukaamua wewe kukaidi utapigwa tu maana hakuna namna nyingine maana wote lazima tukubaliane nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria sasa kama wewe umekaidi hutaki unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi watakupiga tu na mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine  maana tumechoka sasa”.


Nao wanaharakati wa haki za binadamu wamezungumza juu ya kauli hiyo Sauti ya Amerika ilizungumza na mtetezi  wa haki za binadamu Prugensi Massawe wa kituo cha sheria na  haki za binadamu  ambaye amehoji kauli hiyo ya waziri mkuu. Akielezea kila kitu kimeainishwa kwenye sheria kwasababu Tanzania ni nchi yenye utawala wa sheria.


Ripoti ya Mwamoyo Hamza

Nao wanaharakati wa haki za binadamu wamezungumza juu ya kauli hiyo Sauti ya Amerika ilizungumza na mtetezi  wa haki za binadamu Prugensi Massawe wa kituo cha sheria na  haki za binadamu  ambaye amehoji kauli hiyo ya waziri mkuu. Akielezea kila kitu kimeainishwa kwenye sheria kwasababu Tanzania ni nchi yenye utawala wa sheria.
Mahojiano na Prugensi Massawe

kansa ya kizazi

Argentina na hatua za kukinga watoto wa kike dhidi ya kansa ya kizazi


Mtoto wa kike akipatiwa chanjo dhidi ya kirusi cha HPV

Nchini Argentina, utoaji wa chanjo dhidi ya kirusi cha Human Papillomavirus, HPV kwa watoto wa kike kuanzia umri wa miaka 11 ili kuhakikisha pindi wanapobalehe wanakuwa tayari wameshapatiwa kinga dhidi ya kirusi hicho kinachosababisha kansa ya kizazi. Mpango huo uliopendekezwa na pia kuungwa mkono na shirika la afya duniani, WHO umekuwa wa mafanikio katika nchi hiyo ambayo utoaji wa chanjo yoyote haungalii hadhi ya mtu katika jamii bali kila mtu ana haki ya kupatiwa chanjo ili kuepusha magonjwa. Mkuu wa ofisi ya WHO kanda ya Amerika, Pier Paolo Balladeli amesema wanatumia ili kuhakikisha kila mtoto wa kike anapata chanjo hiyo hususan maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo ambako kiwango cha ugonjwa wa kansa ya kizazi ni cha juu. Argentina ilijumuisha chanjo ya HPV katika mpango wa kitafai mwaka 2011 ambapo watoto wa kike huchanjwa mara tatu na katika miaka miwili ya mwazoni dozi ya kwanza imeshafikia asiilmia 80, dozi ya pili asilimia 60 na dozi ya tatu asilimia 50. Kirusi aina ya HPV husababisha zaidi ya wagonjwa wapya Elfu Tatu kila mwaka wa kansa ya kizazi nchini Argentina na kati yao Elfu Moja Mia Nane hufariki dunia.

Hapa na pale

Tanzania na harakati za kutokomeza ajira za watoto majumbani


Mfanyakazi wa nyumbani

Wiki hii dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ajira za watoto. Siku hiyo ilifanyika huku mkutano wa kimataifa wa 102 wa shirika la kazi duniani, ILO ukiendelea hukoGeneva, Uswisi. Maudhui ya mwaka huu ni kutokomeza ajira za watoto majumbani. ILO inasema kuwa watoto zaidi ya Milioni 10 na nusu wameajiriwa majumbani duniani kote na wengine wana umri wa hata miaka mitano na idadi kubwa ni watoto wa kike. Ajira hizo zinawanyima hakiyaoya msingikamaile ya kuendelezwa inayojumuisha pia kupata elimu. Je nchiniTanzania haki iko vipi?

Hali inatokota nchini Brazil



Raia wanpinga gharama ya kuandaa kwa kombe la dunia
Maandamano ya kupinga kupanda kwa nauli ya mabasi ,ufisadi na gharama ya kuandaa michuano ya kombe la dunia nchini Brazil sasa yameenea hadi takriban miji mia moja nchini humo.
Katika maeneo mengi, maandamano hayo yametibuka na kuwa ghasia ukiwemo mji wa Rio De Jeneiro ambapo waandamanaji waliwarushia mawe polisi, huku maafisa hao nao wakijibu kwa kurusha mabomu ya kutoa machozi.
Waandamanaji hao pia wameyavamia majengo ya bunge na wizara ya masuala ya kigeni katika mji mkuu wa Brassilia.
Zaidi ya watu milioni moja wameshiriki maandamano hayo katika hatua ya hivi karibuni kuhusiana na mandamano ya kulalamika kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha.
Ghasia zilizuka katika maeneo mengi na kusababisha kifo cha kijana mmoja mwenye umri wa miaka 18 mjini Sao Paulo.
Maandamano yalianza zaidi ya wiki moja iliyopita kulalamikia kupandishwa kwa nauli ya usafiri pamoja na kukithiri kwa rushwa huku wakilalamika pia kuhusu gharama ya maandalizi ya kombe la dunia mwaka ujao.
Rais Dilma Rousseff alisitisha safari yake nchini Japan ili kushughulikia mzozo huo.
Ameitisha mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri utakaofanyika leo ili kujadili mzozo huo.
Yote haya yanakuja wakati Brazil inajiandaa kuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia mwaka ujao.

Meya wa Kampala 'apigwa' na polisi




Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa Lukwago huku wakimjeruhi
Meya wa mji mkuu wa Uganda, Kampala anasema amepigwa na polisi waliofyatua risasi za mipira kuutawanya umati wa wafuasi wake.
Akizungumza na BBC akiwa kitandani hospitalini, meya huyo Erias Lukwago, anasema alizirai baada ya gesi ya kutoa machozi ilipotupwa ndani ya gari lake.
Anaeleza kwamba maafisa wa polisi walimpiga kifuani na kuzirarua nguo zake wakimshutumu kwa kuchochea ghasia.
Meya huyo ni mpinzani wa rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.
Mtu mmoja anaripotiwa kufariki na wengine kadhaa kukamatwa wakati wa ghasia hizo.
Hata hivyo polisi wamekanusha madai ya kumpiga meya huyo , ambaye pia ni mkoasji mkubwa wa rais Museveni.
Upinzani unasema kuwa serikali inajaribu kukandamiza kilio cha mageuzi nchini humo.
Katika tukio lengine, kiongozi wa upinzani Kizza Besigye alikamatwa kwa kuandaa mkutano ambao polisi hawakuuidhinisha.
Bwana Lukwago, jana alikuwa anaelekea kwenye jopo maalum kwa mara ya kwanza ambayo huenda ikamwondolea wadhifa wake kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi.
Mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga mjini Kampala anasema kuwa polisi walizingira nyumba yake na kisha kumpeleka ambako jopo lilikuwa linaendesha vikao vyake.
Lakini akiwa anapelekwa polisi walirusha vikebe vya gesi ya kutoa machozi, ndani ya gari lake.
Alisema kuwa polisi walimgonga kifuani na kumrarulia nguo zake.
"walinipiga kifuani na kudai kuwa nachochea ghasia , walinirarulia nguzo zangu na kunitesa kwa kila njia. Nilijaribu kuwaambia waniache lakini sikufanikiwa,'' alisema Lukwago.
Kizza Besigye amedaiwa na polisi kuchochea umati wa watu mjini Kampala ili kumuunga mkono bwana Lukwago, kosa ambalo ofisi yake imanusha .

MWANAJESHI WA JESHI LA ANGA AFARIKI

Mnadhimu mkuu wa jeshi la anga la Nicaragua afariki kwenye ajali ya ndege

(GMT+08:00) 2013-06-21 18:21:08
 
Msemaji wa jeshi la Nicaragua Orlando Palacios amethibitisha kuwa, ajali ya helikopita ya jeshi la nchi hiyo aina ya Mi-17 iliyotokea jana imesababisha vifo vya watu 10 akiwemo mnadhimu mkuu wa jeshi la anga.
Palacios amesema waokoaji wamepata baadhi ya miili ya watu waliofariki kwenye ajali hiyo katika ziwa Managua, kaskazini mwa mji mkuu Managua. Miili iliyopatikana ni pamoja na maofisa waandamizi 7 wa jeshi la anga, wakiwemo mnadhimu mkuu wa jeshi la anga Manuel Lopez, na mkurugenzi wa ujasusi wa jeshi la anga.
Jeshi la anga limeunda kikundi maalum kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.

Alhamisi, 20 Juni 2013

Michezo-- Ribery na Benzema wakabiliwa na kesi ya ngono

Wachezaji wawili wa kandanda wa timu ya taifa ya Ufaransa Franck Ribery na Karim Benzema wameshtakiwa mahakamani hii leo mjini Paris kwa kutoa malipo ili kushiriki ngono na kahaba mwenye umri mdogo
Mshambuliaji wa Bayern Munich Ribery na mwenzake wa Real Madrid Karim Benzema wanakabiliwa na adhabu ya hadi miaka mitatu gerezani na faini ya juu ya kiasi cha euro 45,000 kama watapatikana na hatia ya uhalifu huo.
Ribery na Benzema wanakanusha
                                            Zahia Dehar ambaye aliondoa kesi hiyo mahakamani
 
Wachezaji hao wote wawili wanakanusha mashtaka, na msichana aliyehusika, Zahia Dehar, ametoa ushahidi kuwa wanasoka hao wawili hawakujua kuwa alikuwa na umri wa chini ya miaka 18 wakati walipofanya naye kitendo cha ngono mwaka wa 2008 na 2009.
Ijapokuwa umri unaoruhusiwa kisheria nchini Ufaransa wa mtu kuwa na ufahamu ni miaka 15, kumlipa yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18, ili kushiriki naye ngono ni uhalifu. Dehar kwa sasa na umri wa miaka 21. Ribery mwenye umri wa miaka 30, alikiri kufanya mapenzi na Dehar, lakini anasisitiza kuwa hakujua kuwa alikuwa na umri mdogo. Benzema naye anakanusha kabisa kufanya kitendo hicho.
Ribery na Benzema hawakustahili kufika mahakamani, huku wakili wa Ribery akisema kuwa kesi hiyo haikuwa na “mwathriwa”, ikizingatiwa kuwa Dehar, aliondoa mahakamani malalamishi yake na “bila mashitaka yoyote”.
Waendesha mashtaka wa serikali waliitaka mahakama hiyo ya Paris itupilie mbali kesi hiyo, wakihoji kuwa wanasoka hao wawili hawakujua kuhusu umri wa Zahia wakati wa uchunguzi wa mwanzo. Jaji hata hivyo aliamua kuwacha kesi hiyo wazi, akisema walistahili kuwa na uwezo wa kutambua kuwa msichana huyo alikuwa na umri mdogo. Kesi hiyo inastahili kudumu kwa takriban wiki moja, na hukumu yoyote huenda ikachukua muda mrefu.
Mwandishi: Bruce Amani/DW
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman

Urusi na China wahusika wakuu kusafirisha binaadamu kwa magendo

Ripoti ya kila mwaka inayotolewa na serikali ya Marekani hapo jana imeitaja China na Urusi ni miongoni mwa wakiukaji wakubwa kabisa katika mapambano ya kupiga vita kutumikishwa watu kwa nguvu na kusafirishwa binaadamu kwa ajili ya biashara ya ngono.
Ripoti hiyo imesema Urusi imeshindwa kutowa ulinzi kwa wahanga wa biashara ya kusafirisha binaadamu. Imesema China haikuchukuwa hatua kubwa za kupiga marufuku aina zote za usafirishaji wa binaadamu kwa magendo na kuwaadhibu wahusika. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani katika repoti yake hiyo huziorodhesha nchi kwa mujibu wa juhudi zao za kupambana na usafirishaji wa binaadamu kinyume na sheria.
Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imetowa taarifa inayosema ripoti hiyo imetumia utaratibu usiokubalika kwa kuziweka nchi kwa mujibu zinavyojipendekeza kwa serikali ya Marekani.
  

Brazil yatengua ongezeko la nauli

Miji mikubwa miwili ya Brazil,Sao Paulo na Rio de Janeiro imetengua upandishaji wa nauli kwa usafiri wa umma.
Uamuzi huo unakidhi dai muhimu la waandamanaji ambao wamekuwa wakiaandamana katika maandamano makubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa katika nchi hiyo kwa miaka ishirini.  Gavana wa jimbo la Sao Paulo Geraldo Alckmin amesema hapo jana anatumai hatua hiyo ya kubatilisha ongezeko la gharama za usafiri itarudisha utulivu  unaohitajika ili kujadili masuala hayo kwa utulivu.Brazil imekumbwa na maandamano tokea wiki iliopita wakati watu walipoingia barabarani katika mji wa Sao Paulo kupinga ongezeko la nauli za mabasi na treni. Mitandao ya kijamii ilisaidia kuyageuza maandamano hayo kuwa vuguvugu la nchi nzima ambapo hapo Jumatatu zaidi ya waandamanaji 200,000 walijitokeza nchini kote Brazil na kutanuwa kilio chao kutoka suala la nauli na kujumuisha rushwa na gharama kubwa zinazotumika kwa maandalizi ya michuano ya soka Kombe la Dunia mwaka 2014.

Obama aacha gumzo Berlin


Matukio ya Kisiasa


Akikumbushia historia kali ya mji wa Berlin uliyogawika wakati mmoja, rais Barack Obama amezitahadharisha Marekani na Ulaya dhidi ya kuridhika kunakosababishwa na amani, huku akiapa kupunguza silaha za nyuklia.
Rais Obama pia alitangaza kuwa programu yake ya udukuzi wa mawasiliano iliyozua zogo duniani, imenusuru maisha katika pande zote za Atlantiki. Akihutubia umati uliokusanyika katika lango kuu la Brandenburg, Obama alisema ipo haja ya kupunguza kwa sana tu, silaha za nyuklia za Marekani na Urusi, ili kuondoka katika hali ya kivita inayoendelea kuchochea kutoaminiana baina ya serikali za mataifa hayo.
Rais Barack Obama na Meya wa Berlin Claus Wowereit wakimsikiliza Kansela Angela Merkel.  
 
Rais Barack Obama na Meya wa Berlin Claus Wowereit wakimsikiliza Kansela Angela Merkel.
"Tunaweza tusiishi katika hofu ya maangamizi ya nyuklia, lakini maadam silaha za nyuklia bado zinaendelea kuwepo, hatuna usalama wa kweli," alisema Obama wakati akihitimisha ziara ya siku tatu barani Ulaya, ambayo ndiyo ya kwanza tangu aliposhinda muhula wa pili.

Jinamizi la udukuzi wa mawasiliano lamfuata Berlin
Obama anakabiliwa na migogoro ya ndani pamoja na changamoto za sera ya kigeni, ambavyo vinamvurugia malengo yake ya muhula wa pili. Masuala mawili - vita vikali vinavyoendelea nchini Syria, na program ya udukuzi wa mawasiliano - vilimzonga Obama wakati wa ziara yake nchini Ujerumani, na vile vile katika mkutano wa kundi la mataifa nane yalioendelea kiviwanda, G8 mjini Belfast, Ireland ya Kaskazini mapema wiki hii.

Ujerumani, nchi inayolinda sana faragha, ilitaka hasa majibu kutoka kwa Obama kuhusiana na Programu hiyo inayoendeshwa na shirika la usalama wa taifa la Marekani NSA. Kansela Angela Merkel, alitumia mkutano wake na Obama kwa waandishi wa habari, kutaka kuwepo na uangalifu, katika kutathmini wasiwasi kuhusu faragha, inagwa aliepuka kukwaruzana hadharani na rais.
"Kunahitajika kuwepo uwiano, haya ni mapambano ambayo yataendelea," alisema Merkel. Obama alitoa utetezi mrefu wa programu hiyo iliyoidhinishwa na mahakama, akiielezea kama juhudi makhsusi ambayo imesaidia kunusuru maisha. "Tunafahamu kuhusu mashambulizi yasiyopungua 50 ya kigaidi yaliyozuiwa kwa kutumia taarifa hizi, si tu nchini Marekani, bali pia katika maeneo mengine kama hapa Ujerumani."
 
Rais Obama akiwahutubia wakaazi wa Berlin, Juni 19.2013.
Tukio kuu la ziara ya Obama lilikuwa hotuba ya mchana katika lango la Brandenburg, ambako kulikuwa na ukuta wa Berlin uliyougawa mji huo kati ya mashariki na magharibi. Obama, aliesimama nyuma ya kidirisha cha bilauri isiyopita risasi, alizungumza kutoka upande wa mashariki wa lango hilo, eneo ambalo enzi hizo haikuwa rahisi kwa rais wa Marekani kukanyaga.

Alinganishwa na Kennedy
Hotuba ya raia Obama ililinganishwa na ile maarufu ya John F. Kennedy ya "Ich bin ein Berliner" (Mimi ni mkaazi wa Berlin), aliyoitoa miaka 50 iliyopita, na vile vile mapokezi ya kihitoria aliyoyapata Obama mwenyewe alipowasili mjini humo akiwa mgombea wa urais mwaka 2008. Zaidi ya watu 200,000 walifurika katika eneo la karibu na uwanja huo kusikiliza hotuba hiyo, iliyoakisi matarajio makubwa waliokuwa nayo raia wa Ulaya kwa mwanasiasa chipukizi wa Marekani.
Wakati huu akiwa katika mwaka wake wa tano kama rais, Obama bado anaendelea maarufu barani Ulaya. Lakini umati uliokusanyika kumsikiliza siku ya Jumatano ulikuwa mdogo sana ikilinganishwa na mwaka 2008. Hotuba yake iligusia masuala kadhaa yanayotoa changamoto kwa dunia, ambapo alitoa wito kwa mataifa ya magharibi kuwasha upya mzuka uliyoonyesha na Berlin wakati ambapo raia wengi walikuwa wakipambana kuunganisha tena mji huo wakati wa vita baridi.
 
  Rais Obama na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin.
"Vitisho vya sasa siyo kama ilivyokuwa nusu karne iliyopita, lakini mapambano yanaendelea," alisema. "Na nimekuja hapa katika mji huu wa matumaini kwa sababu mitihani ya wakati wetu inatutaka tuwe na roho ya kupambana ambayo mji wa Berlin ulikuwa nayo nusu karne iliyopita."

Mkutano wa nyuklia mwaka 2016
Obama alisema Marekani inaandaa mkutano mwaka 2016, kuhusu juhudi za usalama wa silaha za nyuklia zisizo hifadhiwa vizuri duniani kote, na kuongeza kuwa utawala wake utajitahidi kutafuta uungwaji mkono nchini Marekani, kuridhia Mkataba wa unaopiga marufuku majaribio ya silaha za nyuklia.
Umati wa wageni waalikwa karibu 6000 walivumilia jua kali kushangilia mapendekezo ya Obama kuhusu silaha za nyuklia, na dhamira yake ya kuongeza mara mbili, juhudi za kufunga gereza la Guantanamo lililoko nchini Cuba.
Obama aliondoka mjini Berlin kwa ndege yake ya Air Force One majira ya saa nne usiku, na kuhitimisha ziara iliyodumu kwa masaa 25, katika jiji ambalo wakati mmoja lilikuwa mahali pa hatari kati ya muungano wa kisovieti na mataifa ya magharibi, na ambako vita baridi vilitisha mara nyingi kuripuka katika vita vingine vya dunia. Utawala wa Kikomunisti wa Ujerumani Mashariki ulijenga ukuta wa Berlin, ambao uliugawa mji huo kati ya mashariki na magharibi mwaka 1961.
Wanaharakati wa Amnesty International walifanya maandamano kupinga kuendelea kuwepo kwa gereza la Guantanamo.  
Wanaharakati wa Amnesty International walifanya maandamano kupinga kuendelea kuwepo kwa gereza la Guantanamo.
Lango la Brandenburg, ambako Obama alitoa hotuba yake, ni jengo la tao lenye njia tano, ambalo wakati mmoja lilisimama karibu na ukuta wa Berlin. Ukuta huo ulifunguliwa Novemba mwaka 1989, na ulivunjwa katika miezi iliyofuata, na Ujerumani iliungana tena mwaka 1990.
Mwaka 1994 rais Bill Clinton alikuwa wa kwanza kutoa hotuba kwa Berlin iliyoungana, na kama Obama, yeye pia alizungumza katika uwanja wa Pariser, katika upande wa mashariki wa lango hilo, akiahidi kuwa ubalozi mpya wa Marekani ungejengwa katika upande wa pili. Ubalozi huo ulinfunguliwa mwaka 2008.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/dpae
Mhariri: Josephat Nyiro Charo

Wanawake wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa

                                                       Matibabu ya Ugonjwa wa Kisonono
Hamjambo  wapenzi na karibuni tena kujumuika nami katika kipindi cha Ijue Afya Yako.Kama mnakumbuka wiki iliyopita nilizungumzia magonjwa ya zinaa yaani sexually transmitted diseases (STD) na tulianza kuzungumzia ugonjwa wa kisonono. Tutaendeleza kipindi chetu cha leo kwa kuelezea matibabu ya ugonjwa huo, karibuni.
&&&&
Kabla ya kueleza tiba ya ugonjwa wa kisonono ni muhimu kufahamu kuwa, wanawake wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa huu kwa asilimia 60 hadi 80, huku wanaume wakiwa katika hatari ya kupata ugonjwa huo kwa asilimia 20. Hii ni katika hali ambayo, kama tulivyoashiria huko nyuma dalili za ugonjwa huo huwa hazijitokezi kwa uwazi kwa wanawake ikilinganishwa na wanaume na pia ugonjwa huu una madhara zaidi kwa wanawake kwani hata huweza kuwaletea madhara watoto wao wachanga pale wanapojifungua. Hayo yote yanaonyesha umuhimu wa kutibiwa ugonjwa huo mapema hasa kwa wanawake. Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unaowapata watu wengi na Shirika la Afya Duniani WHO linakadiria kuwa watu milioni 106 duniani huambukizwa ugonjwa huo kila mwaka. Lakini je, tiba ya ugonjwa wa kisonono ni ipi? Tiba ya gono inahusishwa na tiba ya ugonjwa wa chlamydia kwani mara nyingi magonjwa haya mawili ya zinaa huambatana pamoja, na ili kuujua ugonjwa wa chlamydia usikose kutegea sikio kipindi chetu kijacho inshaallah. Matibabu ya kisonono pia hutegemea umri wa mgonjwa na kama ni mwanamke, ni mjamzito au la. Kwa bahati mbaya kuhusiana na matibabu ya ugonjwa huo kumeripotiwa ongezeko la kutosikia dawa vijidudu na hivyo baadhi ya dawa zilizokuwa zikitumika huko nyuma hivi sasa zimekuwa hazina tena athari na hivyo hazitumiki tena. Kisonono ambacho sio sugu kilicho kwenye shingo ya kizazi (cervix), urethra na puru, hutibiwa kwa dawa za cephalosporin, ambapo mgonjwa hupewa dozi moja ya dawa hizo pamoja na dawa aina ya macrolide kwa mfano azithromycin, na za jamii ya penicillin kwa mfano doxycyclin kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa chlamydia. Mara nyingi kwa wagonjwa walio na umri wa chini ya miaka 18 na wanawake wajawazito, hutibiwa kwa kuchomwa sindano. Mgonjwa hutakiwa kufuata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizo kwani dawa nyingi huwa na madhara kwa wajawazito kwa mfano doxycyclin. Kwa kawaida ushauri nasaha hutolewa kwa washirika wote wawili wa ngono, na ni vizuri wote wawili watibiwe hata kama mmoja wao hatakuwa na dalili za ugonjwa huu. Mara nyingi madaktari huwapatia wale wanaosumbuliwa na kisonono dozi pia kwa ajili ya wapenzi wao hata bila ya kupimwa.
&&&&&
Baada ya kufahamu namna ya kutibu gono, sasa tuangalie madhara ya ugonjwa huo. Moja ya madhara anayoweza kupata mtu kutokana na ugonjwa wa kisonono ni, mwanamke kutoweza kuzaa yaani kuwa mgumba au mimba kutoweza kutunga. Tunaelezwa kuwa magonjwa ya zinaa ya chlamydia na gono yana mchango katika kusababisha wanawake kutozaa kwani magonjwa hayo kwa asilimia 10 hadi 15 huweza kusababisha uvimbe katika fupanyonga au Pelvic Inflammatory Disease (PID) na hasa kwa kuwa wanawake wengi wenye kisonono huwa hawaonyeshi dalili. Ugonjwa wa PID husababisha makovu katika mirija ya uzazi hali ambayo husababisha kushika mimba kuwa kugumu na matatizo wakati wa ujauzito. PID ni ugonjwa unaopaswa kutibiwa haraka. Kwa upande wa wanaume ugonjwa wa kisonono pia huweza kuwafanya wanaume wasipate watoto kwani huwasababishia uvimbe katika sehemu ya mbele ya korodani ambako mbegu za kiume hutengenezwa.  Uvimbe huo usipotibiwa husababisha utasa.
Ugonjwa wa gono pia huweza kuathiri moyo, ubongo, ngozi na kadhalika kwa hivyo ni hatari sana kwa mtu yoyote na unahitaji kutibiwa mapema. Pia ugonjwa huo huleta madhara au uvimbe kwenye maungio ya viungo, ambapo vimelea vinavyosababisha kisonono huweza kusambaa kwenye damu na kuleta maambukizo kwenye sehemu nyinginezo mwilini. Maambukizo hayo huleta homa, vipele, vidonda kwenye ngozi, maumivu ya viungo na uvimbe. Vilevile wanawake ambao ni wajawazito na wameambukizwa gono wako kwenye hatari ya mimba kutoka au kuzaa mapema kabla mimba haijatimiza umri wake (preterm labor). Kwa wale wanaoambukizwa gono kipindi cha kukaribia kujifungua, wanaweza kuwaambukiza watoto wao na hivyo watoto kupata ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), kuwa vipofu, homa ya mapafu (pneumonia) na ugonjwa wa mifupa (septic arthritis).

Mnaendelea kupata habari na kuelimika kia- Afya kinachowajia kupitia blog hii ya habari za ulimwengu
Bila shaka baada ya kuona hayo niliyoyaeleza kuhusu ugonjwa wa kisonono, unajiuliza tunawezaje kujikinga na ugonjwa huo. Mpenzi msomaji unaweza kujikinga na gonjwa hili la zinaa kwa njia zifuatazo. Kwanza kabisa ni kuwa mwaminifu katika ndoa na kujiepusha na uasherati. Kuchukua tahadhari na kuzungumzia juu ya ugonjwa huo na dalili zake ili kuweza kufahamu kuwa mshirika wako wa ngono ana ugonjwa huo au la, na iwapo anao hatua inayofuata ni kutibiwa na kupata ushauri wa daktari. Njia nyingine ya kujikinga ni kuepuka kufanya ngono na mtu aliyeambukizwa gono. Vilevile kutumia mipira ya kiume wakati wa kujamiiana, na wanawake wajawazito wanapaswa kuhakikisha kuwa wanahudhuria kliniki mapema ili waweze kuchunguzwa na kupatiwa tiba muafaka iwapo watagundulika kuwa na ugonjwa wa gono au ugonjwa mwingine wowote. Wanawake wajawazito wanashauriwa kujifungua hospitalini ili kama mtoto ameathirika na gono apate matibabu ya haraka baada ya kuzaliwa ili kuepusha kuwa kipofu.
&&&&&
Na nihitimisha kwa kuwajuza kuwa aina mpya ya kisonono imesambaa duniani. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, aina mpya ya vimelea vya ugonjwa wa gono ambavyo vinahimili dawa zinazotumika duniani kutibu ugonjwa huu vimegunduliwa. Taarifa hiyo iliyotolewa na WHO inasisitiza hatari ya kuwa sugu ugonjwa huo unaowaathiri mamilioni ya watu duniani. Shirika la Afya Duniani limetoa wito kwa serikali na madaktari kuongeza ufuatiliaji wa aina hii ya kisonono kutokana na ugonjwa huo kuwa na madhara mengi kama ugumba, matatizo wakati wa ujauzito na hata vifo vya kina mama wajawazito. Dakta Manjula Lusti-Narasimhan, mmoja wa wanasayansi wa Shirika la Afya Duniani katika kitengo cha magonjwa ya zinaa amesema kuwa, aina hii mpya ya vimelea vya kisonono inaonyesha usugu dhihi ya dawa zote za antibiotiki tunazotumia kuviangamiza, zikiwemo dawa jamii ya cephalosporin ambazo ni dawa za mwisho katika kutibu ugonjwa wa kisonono. Dakta Manjula Lusti-Narasimhan aidha ametahadharisha kwamba, katika miaka michache ijayo, aina hii mpya ya kisonono huenda ikawa sugu kwa dawa zote ambazo zinapatikana kwa sasa na kwamba ugonjwa sugu wa kisonono sio tatizo la bara la Ulaya au Afrika pekee bali ni tatizo la dunia nzima. Kwa mara ya kwanza, vimelea sugu vya ugonjwa wa kisonono dhidi ya dawa za cephalosporin viliripotiwa katika nchi ya Japan, ikifuatiwa na Uingereza, Hongkong na Norway. Wanasayansi wanaamini kuwa, matumizi holela ya dawa aina ya antibiotiki pamoja na uwezo wa vimelea vya ugonjwa huo  kubadilika na kuzoea mazingira mapya ndio chanzo kikuu cha kuwa sugu kisonono na hivyo muda si mrefu ugonjwa huu unaweza kuwa janga kubwa dunia kama hatua za haraka hazitachukuliwa. Kuna uwezekano wa vimelea hivi sugu vya kisonono kusambaa kwa haraka duniani bila kugundulika kutokana na nchi nyingi kutokuwa na ufuatiliaji na utunzaji kumbukumbu mzuri wa wagonjwa wake. WHO imezitaka nchi zote kuongeza ufuatiliaji wa wagonjwa wake pamoja na kudhibiti matumizi holela ya dawa za antibiotiki mpaka pale taarifa kamili za ugonjwa huu zitakapojulikana.
Naam mpenzi msomajii, kumbuka kuwa, kuwa mwaminifu katika ndoa na kujiepusha na ngono zembe na uasherati ni suala linasisitizwa sana sio tu katika kujikinga na kisosono bali na magonjwa mengine ya zinaa au STD. Kwani kwa kawaida kama hujapimwa huwa vigumu kutambua iwapo wewe au mwenzako ameathirika au la, na kama una michibuko au umekatika kwenye ngozi unaweza kupata maambikizo ya magonjwa hayo. Njia pekee na nzuri ni kuacha ngono zembe au uasherati. Tunapaswa kufahamu kuwa mtu aliyepata gono mara moja anaweza kupata tena. Tunaishia hapa kwa leo, tudumu katika kheri na kwaherini.
F

Mwanamke Mwislamu mjamzito ahujumiwa Ufaransa


Katika siku za hivi karibuni nchini Ufaransa kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la hujuma dhidi ya wanawake Waislamu wanaovaa hijabu, mitandio au burka.
Hiyo juzi mwanamke Mwislamu aliyekuwa amevaa Hijabu alishambuliwa na magenge ya kibaguzi ya Wanazi mamboleo katika kitongoji cha Paris cha Argenteuil. Imearifiwa kuwa mwanamke huyo aliye na umri wa miaka 21 alikuwa na mimba ya miezi minne ambayo aliipoteza kufuatia hujuma hiyo. Wakili wake anasema alishambuliwa barabarani na watu ambao walijaribu kupasua mtandio wake huku wakimpiga mateke tumboni.
Kufuatia kitendo hicho cha kinyama, watu waliokuwa na hasira waliandamana mbele ya ofisi za meya wa Argenteuil kulalamikia ongezeko la hujuma za magenge ya Wanazi mambo-leo dhidi ya Waislamu. Meya wa mji huo amelaani hujuma hiyo na kusema hatakubali chuki kutekelezwa dhidi ya Uislamu au Islamophobia katika mji huo. Hata hivyo Waislamu wanasema makundi ya Wanazi mamboleo vipara yameonekana mjini humo na kwamba hakuna hatua zozote za kisheria zinazochukuliwa dhidi yao.


 

Machafuko yaendelea Misri

Ni matumaini yangu kuwa, hujambo mpenzi msomaji popote pale inapokufikia blog hii ya habari na uchambuzi, jumuika nami kwa kupata habari mhimu na uchabuzi wa habari mbalimbali
 
Watu wasiopungua 27 wamejeruhiwa katika mapigano baina ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammad Morsi wa Misri.
Machafuko hayo ya Jumatano katika mkoa wa Fayoum yaliibuka baada ya mkutano ulioitishwa na harakati ya Ikhwanul Muslimin kumuunga mkono Rais Morsi.
Machafuko yaliibuka pia katika eneo la Nile Delta baada ya rais Morsi kuwateua wanachama kadhaa wa harakati ya Ikanul Muslimin katika nyadhifa muhimu serikalini. Hivi karibuni Rais Morsi aliwateua magavana wapya ambao wote ni wanachama wa Ikhwanul Muslimin. Hii inamaanisha kuwa magavana 11 kati ya 27 kote Misri ni wanachama wa Ikhawanul Muslimin.
Weledi wa mambo wanasema Misri inakabiliwa na hitilafu kubwa za kimitazamo na mgawanyiko wa kijamii na kwamba iwapo masuala hayo mawili hayatotatuliwa haraka, yanaweza kuwaletea madhara Wamisri wenyewe.     

Maduka ya wahindi yashambuliwa.


Maduka yanayomilikiwa na wahindi yamevamiwa katika mashambulizi mjini Kinshasa DRC baada ya kukamatwa kwa wanafunzi wakongomani nchini India.
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema kuwa raia mmoja mhindi alijeruhiwa katika ghasia hizo na anatibiwa hospitalini.
Waandamanaji walighadhabishwa na hatua ya kukamatwa kwa wanafunzi 21 mjini Jalandhar, Kaskazini mwa India.
Kuna visa vya kutofautiana kuhusu sababu za kukamatwa kwa wanafunzi hao na kumekuwa na madai kuwa polisi wamewadhulumu.
Lakini balozi wa India katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Ram Manohar, aliambia BBC, kuwa polisi hawakuwadulumu wanafunzi hao, lakini wakasema kuwa kulikuwa na vurugu wakati wa maandamano.
Aliongeza kuwa wanafunzi hao waliachiliwa Jumatano nyakati za mchana.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa DR Congo, alitoa ombi kuwa wanafunzi hao waachiliwe mara moja.
Maafisa wa utawala pia walitaka wanafunzi hao watibiwe kufuatia madai kuwa waliteswa walipozuiliwa.
Mapema taarifa za vyombo vya habari zilisema kuwa wanafunzi hao walijaribu kujitoa uhai.
Mwandishi wa BBC, Emmanuel Derville mjini Delhi, anasema kuwa wengi wa wanafunzi hao, waliozuiliwa wanatoka Kinshasa, na wako nchini humo kusomea uhandisi na masomo ya biashara kwa miaka miwili iliyopita.
Kulingana na Polisi, wanafunzi hao walikamatwa baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya makundi hasimu ya wakongomani baada ya kuzuka mapigano katika kituo cha basi
mjini Jalandhar Jumamosi mchana.
Naibu wa polisi mjini Jalandhar, alisema kuwa wanafunzi hao walimpokonya mkoba wake mwathiriwa mmoja.
Lakini wanafunzi hao walisema kuwa purukushani lilianza baada ya mwanafunzi mmoja nusura kugongwa na basi
Baadaye alichapwa kwa bakora katika kile kilichoonekana kama shambulizi la ubaguzi wa rangi.

Ukurasa wa ajira


Ukurasa wa ajira

Hapa utapata fursa ya kuangalia na kuchagua ajira unayotaka kadri BBC inavyotangaza nafasi za kazi katika taaluma mbali mbali.
BBC ina aina tofauti za ajira, baadhi ni kwa watu ambao tayari wanafanya kazi ndani ya BBC na nyingine ni kwa ajili ya watu ambao hawajawahi kufanya kazi BBC – na ajira za aina hiyo hutangazwa nje ya BBC.
Kinyume na wengi wanavyodhani, BBC inatoa ajira kando na uandishi wa habari na utangazaji, kwa hiyo usijinyime nafasi kabla ya kujaribu kuingia katika tovuti ya BBC Jobs, (Bofya http://www.bbc.co.uk/jobs)

Jumatano, 19 Juni 2013

Obama ahutubia maelfu Berlin

Matukio ya Kisiasa

Rais Obama wa Marekani amehutubia umati wa watu zaidi 6,000 waliokusanyika katika uwanja wa lango la brandenburg, hotuba ya kihistoria iliyolengwa kufunga ukurasa wa vita baridi na kupunguza mbio za silaha za kimkakati.
Kijua chembamba kinapiga bado katika uwanja wa Paris katika lango la Brandenburg wakati diwani wa jiji la Berlin Klaus Wowereit, alipomkaribisha rais wa Marekani barack Obama na kusema, "Lango la Brandenburg liko wazi. Huu ni ushahidi kwamba hakuna kisichowezekana kwamba tawala za kiimla na kunyimwa watu uhuru vinaweza akushindwa".
Hata kansela Angela Merkel hajaiachia fursa iliyopatikana kutokana na hali nzuri ya hewa kumkaribisha rais huyo wa Marekani alisema "Tumeichagua hali nzuri kabisa ya hewa ili kukukaribisha Barack Obama. Na kushadidia uhusiano mzuri ulioko kati ya Marekani na ujerumani "Uhusiano wa dhati usiotetereka ndio msingi wa mustakbal wetu wa pamoja. Na hivyo ndivyo tutakavyoimarisha uhusiano wa nchi zinazopakana na bahari ya Atlantik katika karne hii ya 21".

                                                   Ujumbe wa Obama kwa umma

German Justice Minister Sabine Leutheusser-Schnarrenberger (FDP) German Interior Minister Hans-Peter Friedrich (CSU), German Foreign Minister Guido Westerwelle (FDP), German Economy Minister Philipp Roesler (FDP) and his wife Wiebke Roelser (L-R) wait for U.S. President Barack Obama's speech in front of Brandenburg Gate at Pariser Platz in Berlin June 19, 2013. Obama's first presidential visit to Berlin comes nearly 50 years to the day after John F. Kennedy landed in a divided Berlin at the height of the Cold War and told encircled westerners in the city Ich bin ein Berliner, a powerful signal that America would stand by them. REUTERS/Michael Kappeler/Pool (GERMANY - Tags: POLITICS)
Wageni waalikwa katika lango la Brandenburg, Berlin
Katika hotuba yake iliyokuwa ikisubiriwa akwa hamu mbele ya wageni zaidi ya elfu sita,miaka 50 baada ya ile ya rais wa zamani wa Marekani John F.Kennedy,rais Barak Obama alisema "Lakini ukweli kwamba tunasimama hapa tulipo hii leo katika mstari huu uliokuwa ukiugawa mji huu ni ushahidi kwamba hakuna anaeweza kushindana na kiu cha kudai haki,kiu cha kudai uhuru na kiu cha kudai amani kilichoko katika mioyo ya wanaadam

Rais Barack Obama amependekeza kupunguza idadi ya vichwa vya silaha za kinuklea kati ya Marekani na Urusi na kupendekeza pia kupunguzwa silaha za kimkakati za kinuklea bara Ulaya. Kuhusu Afghanistan rais Obama ameelezea azma ya kutaka uendelezwe utaratibu wa amani licha ya kuasisiwa na serikali ya Kabul. Na pia kuhusu Syria rais Obama ameshauri upatikana ufumbuzi wa kisiasa.
Kabla ya hapo rais Barack Obama alikuwa na mazungumzo pamoja na rais wa shirikisho Joachim Gauck na baadae na kansela Angela merkel. Amepangiwa kukutana tena na kansela Angela Merkel na pia mgombea kiti cha kansela kutoka chama cha upinzani cha SPD Peer Steinbrück.
Rais Barack Obama, mkewe Michell na binti zao wataondoka Berlin leo usiku kurejea Washington.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir
Mhariri:Josephat Charo